Profesa Kabudi: Katiba tuliyonayo ni madhubuti ndio maana imetuvusha tulipopata matatizo!

Profesa Kabudi: Katiba tuliyonayo ni madhubuti ndio maana imetuvusha tulipopata matatizo!

View attachment 1838966
Hapa Prof.Kabudi akiwa mjumbe wa Tume ya Katiba. Akisukuma ajenga za kudai katiba mpya na serikali 3.

View attachment 1838967
Hapa akiwa waziri wa sheria.

My Take
Hawa jamaa wanatupa taabu sana kuirudisha nchi kwenye reli
Nilikuwa Kilosa last week, shule aliyosoma inaitwa Madudu Primary School, nilipoona hilo jina la shule yake nilimwombea msamaha kwa Mungu
 
Namuelewaga sana huyo mzee jinsi anavyowasilishaga hoja zake kwa msisitizo!
 
Tatizo siyo kifo kweli! Lakini kumbuka aliyefariki ni Rais,tena ndiyo yuko Madarakani,Kama kungetokea wale wavamizi wa Mirathi ya Mama unazani saa hizi hali ingekuwaje!?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
As long as jeshi lilikuwepo kutheshimu katiba hao wagombea mirathi wangetoka wapi? Besides mama naye alichaguliwa na alikuwepo kwenye karatasi la kupigia kura, hakuteuliwa na magufuli......muwe mnajiongeza maarifa
 
Katiba yetu nzuri inaelekeza wananchi kupitia wawakilishi wao bungeni ndiyo wenye mamlaka ya kumu impeech rais kwa kura za 2/3 kutoka kila pande za muungano kwani rais anachaguliwa na wananchi wote na madaraka yake kakabidhiwa na wananchi wote. Ikitokea bunge likapitisha kura ya kumu impeanch rais, bunge huvunjika na Tume ya Uchaguzi huandaa na kuendesha uchaguzi mkuu mpya wa rais na wabunge. Yaani katika uchaguzi huo wananchi ndiyo hutoa maamuzi ya kurudi au kutorudi kwa rais huyo na wabunge hao. Hii ndiyo peoples power ya katiba yetu na si ile peoples power fake ya chadema.
Hao walioko bungeni sio wawakilishi wa wananchi. Katiba iliyopo na tume yake ya uchaguzi viliwezesha watu wasio wawakilishi wawe huko mjengoni. Lazima unafahamu hili.
 
Hao walioko bungeni sio wawakilishi wa wananchi. Katiba iliyopo na tume yake ya uchaguzi viliwezesha watu wasio wawakilishi wawe huko mjengoni. Lazima unafahamu hili.
Mlishasema hamuutambui uchaguzi mkuu uliopita. Kwa hiyo hamulitambui wala kulikubali bunge lililopo. Maana yake hata rais aliyepo madarakani kutokana na uchaguzi huo hamumutambui wala hamumukubali.

Sasa mbona munahangaika kumuomba rais kumuomba katiba mpya? Atawapaje hiyo katiba mpya wakati yeye siyo rais (kwa akili yenu) maana hamumutambui kama yeye ni rais, amiri jeshi mkuu na mkuu wa nchi? Si muendelee tu kutunga hiyo katiba yenu mpya peke yenu na tuone mtakachokipata. Kelele za nini?

Mungalikuwa na akili sasa hivi mungekuwa mmekazana kuweka mikakati ya kushika dola ifikapo 2025 (kwa katiba hii hii - Lowassa alibakiza kidogo tu kuwavusha uchaguzi wa 2015). Baada ya kuchukua dola ndipo sasa mungalileta hiyo katiba yenu mpya munayoitamani. It is that simple but not now when you are nobody.
 
Namshukuru sana JPM kwa kutuonyesha rangi halisi za hawa wanasiasa.
 
Hivyo ulitegemea aendelee kudai katiba mpya akiwa kiongozi katika serikali?

Umeshawahi kusikia waziri anauliza swali bungeni? Unafikiri ni kweli mawaziri hawana maswali kwa serikali?

Kabudi yuko sahihi tu, hayuko kwenye nafasi ya kudai katiba
Hoja kama hizo unazikwepa kiaina sio kujiabisha, unapokuwa mwajiriwa sio kwamba makosa ya boss huyaoni, unayaona ila unayakwepa kiaina.Kabudi anadharau kwa wananchi.
 
Njaa hainaga adabu wala baunsa! Ndipo profesa Assadi akasema 60% ya viongozi tulionao hawafai kabisa.
Tokashule mpaka majumbani hatukufundishwa kuwa na misimamo wala kujiheshimu!! Hao ndomajembe ya mwendazake kindakindaki sasa, mtafute bashiru akiongelea katiba kabla ya tonge na baada... naye utashika kichwa, ndoujue hawa wote ni wasakatonge tuu wanaojificha kwa kujidai wazalendo wapinga mabeberu!!
 
Ukiwa ndani ya chama huwezi kufikiri sawa sawa hamwoni katibu mkuu mstafishwa alivyokuwa nje ya chama na alivyokuwa ndani ya chama, na wakienda chama kingine hutamini wanavyo ongea, watz kuna shida kidogo hapo nadhani.
Ndiyo maana wasomi wetu wabobezi wanatukanwa na kudharauliwa na wa darasa la saba kuwa si lolote si chochote na hawana hoja mbele ya wa darasa la saba!
 
Angetafuta namna nzuri ya kueleza badala ya kuikataa kabisa katiba maana hata Rais hajasema katiba mpya siyo agenda bali muda ni bado kwakua haikuwa planned for kwa muda huu baada ya mara ya kwanza kuachwa
Ni bahati mbaya kuwa Prof.Kabudi hajaacha koti la ualimu na kila aliye mbele yake ni Mwanafunzi.Hatulii akawaza cha kuzungumza na hii ilimletea matattizo kwenye suala la Azory Gwanda.Yeye ni mwanasaiasa sasa kama ana conflict of interest na issue iliyopo mezani amwachie mwingine azungumze!!
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Katiba ya Tanzania ni nzuri, inapaswa kuheshimiwa kwa kuwa imeivusha nchi katika kipindi kigumu.

Alisema uzuri wa Katiba na umadhubuti wake huonekana wakati wa matatizo yasiyo ya kawaida, hivyo inafaa kuheshimiwa.

Profesa Kabudi alisema mabadiliko mengi ya Katiba yalifanyika mwaka 1984, hivyo ni vyema kuendelea kuienzi kwa sasa wakati utaratibu mwingine unasubiriwa.

Kauli hiyo inakuja zikiwa zimepita takribani siku tatu tangu viongozi wa dini nchini kueleza umuhimu wa Katiba Mpya, huku Chadema kupitia kongamano maalumu lililoandaliwa na Baraza la Vijana wa chama hicho (Bavicha), likieleza umuhimu wa suala hilo juzi.

Profesa Kabudi alitoa kauli hiyo jana katika maadhimisho ya saba ya siku ya utetezi wa haki za binadamu, yaliyofanywa na asasi za kiraia nchini pamoja na uzinduzi wa utekelezaji wa mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano wa azaki hizo.

Alisema baada ya Rais John Magufuli kufariki dunia, makamu wake (Rais Samia Suluhu Hassan) aliapishwa kushika wadhifa huo kwa matakwa ya Katiba kupitia Ibara ya 9 na sasa nchi ina Rais mtendaji mwanamke na mwenye uwezo.

“Hili lilikuwepo ndani ya Katiba, limeivusha nchi yetu katika kipindi hiki kigumu na uzuri wa Katiba na umadhubuti wake unauona wakati wa matatizo yasiyokuwa ya kawaida. Tanzania imevuka mtihani huo kwa katiba hii na tumshukuru sana Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kutuwekea misingi ambayo imetufikisha hapa, nchi nyingine za Afrika kwa hili lililotokea ni vita, dhahama na migogoro, sisi salama salimini, Samia Suluhu Hassan amepokewa vizuri na raia wote wa Jamhuri ya Muungano bila maswali,” alisema Profesa Kabudi.

Pia, alisema mbali na hayo, Katiba ya sasa imekuwa msaada mkubwa kiutendaji na inalinda haki za binadamu na utawala bora.

“(Katiba ya sasa) Inalinda haki za kiraia, kisiasa, uchumi na za kiutamaduni na ndiyo maana Serikali imeridhia kwanza Katiba yetu,” alisema.

Katika kongamano la Bavicha, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitaka Rais Samia Suluhu Hassan kuunda Tume ya Katiba ili kusimamia mchakato wa kupata Katiba Mpya.

Mbowe alisema Watanzania wanahitaji Katiba Mpya, bora na shirikishi, huku akipendekeza makundi mbalimbali ya kijamii yashirikishwe.

Alisema hatua ya pili iwe ni kuunda Bunge Maalumu la Katiba litakalozingatia masilahi ya makundi yote.

Awali, akizindua mkutano huo, Profesa Kabudi alizitaka asasi hizo za kiraia kuacha kutegemea wahisani, bali wajitegemee kutafuta vitu vya kuwaingizia kipato pamoja na kufuata sheria za nchi wanapofanya kazi zao.

“Wakati umefika asasi za kiraia kuanza kufikiria kutafuta njia nyingine za kuziwezesha asasi hizi kifedha kuliko kuendelea kusaidiwa, siwezi kusema tuache kusaidiwa, ila tuanze kufikiria kwenda mbali,” alisema Profesa Kabudi.

“Asasi nyingi bado zinajikita katika dhana ya Serikali kama mvunjifu mkuu wa haki za binadamu na matokeo yake hazielekezi nguvu kubwa katika kupambana na uvunjifu wa haki za binadamu unaofanywa na raia au kampuni na mashirika makubwa ya kiuchumi duniani.”

Mwananchi
 
Back
Top Bottom