Profesa Kabudi, nenda Madagascar ukatuletee miche ya Vanilla

Pia mkuu mrangi ,naomba niweke wazi kuwa moja ya watu ambao wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuizunguka Tanzania kwa kufanya biashara nyingi halali,wewe ni mmojawapo kati ya wachache ninao wafahamu,na mmoja kati ya mmoja humu JF.
Ombi langu kwako,tafadhali, tafadhali, tafadhali mkuu,anzisha uzi wa kuelekeza fursa kulingana na maeneo na uzoefu wako,hakika utawasaidia wengi na Mungu atakubariki sana.
Kongole mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wanunuzi wa vanilla toka Uganda kuna wakati wananunua bei kubwa inafikia laki au inazidi kidogo kutokana na daraja la ubora wa vanilla na mwishoni mwa msimu.
Ila kangomba za wabongo inauzwa hadi 40,000/- au pungufu ya hapo kama unavyojua kangomba na ulaliaji wa wabongo.
Nina uhakika wa bei nilizotaja sababu nilijihusisha kidogo na hayo mambo.
 
Hekari moja miche mingapi?
Spacing yake inakuwaje?
Mkuu funguka zaidi, ndiyo elimu hii tunapeana.
Nenda SUA Moro utapata maelekezo na mbegu pia.
Kama upo Kilimanjaro na jirani yake wapo jamaa wanatoa mafunzo na wanauza mbegu ni mradi ambao unafadhiliwa na sirika flani la kwa Trump.
Mimi nina manual lakini siwezi ku-share hapa ni Proprietary Document mambo ya haki miliki nisije ingia matatizoni na wachapishaji.
Pia nenda mitandaoni maelezo kibao ya kila hatua.

Pia ukitangaza kununua mbegu hapa atakaye kuuzia atakupa na maelekezo jinsi ya kupanda na mengineyo.
 
Hivi katika nchi zinazolima vanilla Unaweza kusema Tanzania nayo imo, Hata cocoa tunalima sehemu za Maramba mkoani Tanga lakini siwezi nikajisifia , Najua Kagera wanalima lakini sio large scale farming
 
Hivi katika nchi zinazolima vanilla Unaweza kusema Tanzania nayo imo, Hata cocoa tunalima sehemu za Maramba mkoani Tanga lakini siwezi nikajisifia , Najua Kagera wanalima lakini sio large scale farming
Akafuate mbegu Madagascar mbali kote kwanini wakati hapa ipo kibao tu?
Wewe kama una hela unataka kulima sema tu mimi nikupe contact za mtu akuletee hata za hekari 20.
 
Macadamia (Katanga miti) nalo ni zao zuri sana lenye faida nalo linalimwa Mbeya Tukuyu na Kilimanjaro.
 
Ahsante sana kwa maelezo hayo...
Je mtu akitengeneza kivuli artificial (shading) bila hayo mazao mama kuwepo itaathiri production?
Halafu akaweka/kusimika miti (mfano wa kichanja) ambayo kwayo vanilla itatambaa...hapo vipi?
 
Ndio maana bukoba wakulima wengi wanaiuza kwa waganda
 
Standard 6kg za vanilla mbichi inatoa 1kg ya vanilla kavu (cured vanilla).
 
Kwahiyo tani sita ndiyo unapata tani moja ya hiyo kavu...
Kitu kama hicho.
Lakini bei ya soko la dunia hiyo kavu inafika USD 500 hadi $600. Mbegu pia unauza bei nzuri tu kama alivyo kuambia mdau Sting

Tafuta bei mtandaoni uone.
 
Ahsante sana kwa maelezo hayo...
Je mtu akitengeneza kivuli artificial (shading) bila hayo mazao mama kuwepo itaathiri production?
Halafu akaweka/kusimika miti (mfano wa kichanja) ambayo kwayo vanilla itatambaa...hapo vipi?
Mkuu sina jibu la kitaalamu hapo ila ninachojua ni kuwa inastawi zaidi ikiwa pamoja na mazao mengine hasa kahawa na migomba.
 
Nasikia hadi leo hii maambukizi ni 10,000.huku watu 96 washa wahishwa kwa Israel
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…