Profesa Kabudi, nenda Madagascar ukatuletee miche ya Vanilla

Profesa Kabudi, nenda Madagascar ukatuletee miche ya Vanilla

Hujui kama Kuna watu wanalima vanilla hko kagera na bukoba tena Kuna wakati wakulima ikifika karibia
Na kuvuna wanalinda mashamba yao kwa ulinzi mkali sna....
Wewe labda ungeishauri serikali iwasisitize na kuweka nguvu kubwa watu walime zao Hilo
Kwani hata mbeya, tukuyu, moro vijijini zao Hilo likilimwa linakubali
Nna ushahidi kna mtu alienda kijiji cha rubale na alichkua miche ya vanilla na alienda kujaribu kupanda tukuyu mbeya na ilikubali, jamaa alikuwa na plan ya kufanya mradi huo huko mbeya ila bahati mbaya jamaa alikujaga kufariki
Tatizo watz siyo watu wa kufatilia mambo na kutekeleza
We washauri serikali ikazanie watu walime vanila
Maana Kuna maeneo mengi inakubali

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Pia mkuu mrangi ,naomba niweke wazi kuwa moja ya watu ambao wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuizunguka Tanzania kwa kufanya biashara nyingi halali,wewe ni mmojawapo kati ya wachache ninao wafahamu,na mmoja kati ya mmoja humu JF.
Ombi langu kwako,tafadhali, tafadhali, tafadhali mkuu,anzisha uzi wa kuelekeza fursa kulingana na maeneo na uzoefu wako,hakika utawasaidia wengi na Mungu atakubariki sana.
Kongole mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vanilla inalimwa maeneo mengi ya Tanzania hasa Kagera, Kilimanjaro na Morogoro. Hapa Tanzania wakulima wengi wanalima vanilla kama zao la ziada na wengi wanakuwa na miche michache ni nadra kukuta mkulima ana miche (pods) zaidi ya mia mbili. Bei ya vanilla kwa kilo haifiki laki moja kama mnavyotaka kutuaminisha, ni zao rahisi sana kulima kwasababu linaota sambamba na miti hasa kahawa, ugumu wake ni kwenye curing process hivyo kufanya wakulima wengi wauze ikiwa mbichi ambapo bei yake inakuwa ndogo kulinganisha na vanilla iliyokaushwa. Kwa hapa Tanzania kuna kiwanda cha ku process Vanilla kiko Moshi kinaitwa Natural extracts industries (NEI) na hao ndio wanunuzi pekee kwa sasa. Vanilla inayolimwa Kagera nyingi inauzwa nchini Uganda ambao pia ni wazalishaji wakubwa kwa hapa Afrika Mashariki.
Mkuu wanunuzi wa vanilla toka Uganda kuna wakati wananunua bei kubwa inafikia laki au inazidi kidogo kutokana na daraja la ubora wa vanilla na mwishoni mwa msimu.
Ila kangomba za wabongo inauzwa hadi 40,000/- au pungufu ya hapo kama unavyojua kangomba na ulaliaji wa wabongo.
Nina uhakika wa bei nilizotaja sababu nilijihusisha kidogo na hayo mambo.
 
Hekari moja miche mingapi?
Spacing yake inakuwaje?
Mkuu funguka zaidi, ndiyo elimu hii tunapeana.
Nenda SUA Moro utapata maelekezo na mbegu pia.
Kama upo Kilimanjaro na jirani yake wapo jamaa wanatoa mafunzo na wanauza mbegu ni mradi ambao unafadhiliwa na sirika flani la kwa Trump.
Mimi nina manual lakini siwezi ku-share hapa ni Proprietary Document mambo ya haki miliki nisije ingia matatizoni na wachapishaji.
Pia nenda mitandaoni maelezo kibao ya kila hatua.

Pia ukitangaza kununua mbegu hapa atakaye kuuzia atakupa na maelekezo jinsi ya kupanda na mengineyo.
 
Mtu kama wewe ambae hauna taarifa za mambo mengi ya nchi yako kuhusu kilimo huna moral authority ya kumshambulia na kumkosoa Prof. Kabudi kama ulivyofanya hapa.

FYI, aina ya Vanilla inayolimwa Madagascar ipo kwa wingi tu inalimwa mkoani Kagera. Hakuna haja ya kwenda kufuata mbegu za vanilla nchi nyingine.
Na vanilla kabila hiyo ndiyo bora zaidi duniani, inalimwa kwa wingi pia nchi jirani ya Uganda kiasi kwamba wanunuzi wakubwa wa vanilla ya Kagera wanatoka Uganda. Labda mshauri waziri wa kilimo akafanye hamasa ya miradi mikubwa ya kulima vanilla kibiashara zaidi kule Kagera. Ukitaka vanilla tuber cuttings kwa ajili ya mbegu wewe sema tukuuzie.
Pia ungeshauri watanzania wasiuze vanilla pods mbichi bali wafanye vanilla cure and vanillin extraction process hapa hapa nchini na kuuza bei ya soko la dunia.
Hivi katika nchi zinazolima vanilla Unaweza kusema Tanzania nayo imo, Hata cocoa tunalima sehemu za Maramba mkoani Tanga lakini siwezi nikajisifia , Najua Kagera wanalima lakini sio large scale farming
 
Hivi katika nchi zinazolima vanilla Unaweza kusema Tanzania nayo imo, Hata cocoa tunalima sehemu za Maramba mkoani Tanga lakini siwezi nikajisifia , Najua Kagera wanalima lakini sio large scale farming
Akafuate mbegu Madagascar mbali kote kwanini wakati hapa ipo kibao tu?
Wewe kama una hela unataka kulima sema tu mimi nikupe contact za mtu akuletee hata za hekari 20.
 
Macadamia (Katanga miti) nalo ni zao zuri sana lenye faida nalo linalimwa Mbeya Tukuyu na Kilimanjaro.
 
Vanilla hailimwi peke yake kwasababu ni mmea pori unahitaji sana kivuli ndio maana vanilla inalimwa kwenye mashamba ya kahawa na migomba au mashamba ya kokoa au miembe. Ni mmea unaotambaa kama passion fruit kwa hiyo unahitaji support ya miti mingine yenye kivuli ili uweze kustawi vizuri. Huu mmeq hauchukui nafasi kubwa kwasababu unaota kuelekea juu hivyo spacing yako inategemea zao mama kama ni kahawa au mikokoa.
Ahsante sana kwa maelezo hayo...
Je mtu akitengeneza kivuli artificial (shading) bila hayo mazao mama kuwepo itaathiri production?
Halafu akaweka/kusimika miti (mfano wa kichanja) ambayo kwayo vanilla itatambaa...hapo vipi?
 
Vanilla ina pesa nyingi sana lakini kwa kuwa serikali ina chuki na wananchi basi tu hakuna namna. Haina mpango wowote wa kumsaidia mkulima. Kahawa na vanilla zingeingiza pato la taifa. Kuna parachichi na ndizi pia hizo zina angalau kwa vile ni mazao ya chakula.
Ndio maana bukoba wakulima wengi wanaiuza kwa waganda
 
Mche mmoja wa mita mbili unauzwa kwa kati ya tshs 4,000 na tshs 6,000. Mche mmoja unachua miezi 9 au zaidi kuanza kuzaa na unatoa kati ya kilo 1 hadi tatu z ya vanilla mbichi ambayo ikikaushwa inaweza kuleta takribani nusu au robo tatu ya kilo. Vanilla inatoa matunda mfano wa maharage ndiyo ambayo huvunwa, mche wenyewe unaendelea kubaki na kukua ukiongezeka urefu. Miche yako ikiwa mirefu zaidi unaeza kuiuza kwa kukata kama unafanya prunning maana vanilla unapanda kipande cha mti wa vanilla yenyewe na sio mbegu.
Standard 6kg za vanilla mbichi inatoa 1kg ya vanilla kavu (cured vanilla).
 
Kwahiyo tani sita ndiyo unapata tani moja ya hiyo kavu...
Kitu kama hicho.
Lakini bei ya soko la dunia hiyo kavu inafika USD 500 hadi $600. Mbegu pia unauza bei nzuri tu kama alivyo kuambia mdau Sting

Tafuta bei mtandaoni uone.
 
Ahsante sana kwa maelezo hayo...
Je mtu akitengeneza kivuli artificial (shading) bila hayo mazao mama kuwepo itaathiri production?
Halafu akaweka/kusimika miti (mfano wa kichanja) ambayo kwayo vanilla itatambaa...hapo vipi?
Mkuu sina jibu la kitaalamu hapo ila ninachojua ni kuwa inastawi zaidi ikiwa pamoja na mazao mengine hasa kahawa na migomba.
 
Nchi ya Madagscar inasifika sana kwa ulimaji wa zao la vanilla. Zao hili linawaongezea kipato kikubwa sana raia wa Madagascar kwani kilo moja inafika karibu dola 600 za Kimarekani.

Nakumbuka sana Profesa Kabudi aliporudi na mitishamba ya Corona toka Madagascar kwa mbwembe nyingi sana na kulihutubia Taifa.

Alikusanya jopo la maprofesa na madaktari kwamba watashughulikia utafiti wa mitishamba hiyo toka Madagascar kama inatibu Corona.

Mpaka leo hakuna taarifa za matokeo ya uchunguzi huo. Kwa kifupi Mitishamba hiyo haitibu kwani Madagascar sasa hivi wanalia na maambukizi ya Corona.

Naomba Profesa Kabudu urudi tena Madagascar ukatuletee miche ya Vanilla ili wananchi tuinue kipato chetu, tutakukumbuka sana ukituletea miche ya vanilla.
Nasikia hadi leo hii maambukizi ni 10,000.huku watu 96 washa wahishwa kwa Israel
 
Back
Top Bottom