Ni nani huyu jamaa uliyemtaja mara kadhaa ktk comment yako yenye ushauri murua kwa majina haya Mh. Hammed Salimu Hammed
Ni Mzanzibari, baada ya Muungano aliwahi kuwa Balozi wetu Nchini Misri akiwa na umri wa miaka 24, baadae akaja akateiliwa kuwa naibu wa katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, nadhani Bwana Uthant kama nakumbuka vizuri.
Mataifa mengi yalimukubali sana Hammed - yeye ndiye aliweka shinikizo kubwa Umoja wa Mataifa kwa Uchina kukubalika kurudushiwa u-membership wa Umoja wa Mataifa uliyo sitishwa mwaka 1949 kutokana na shinikizo la USA, tuliambiwa kwamba baada ya Uchina kukubaliwa Umoja wa Mataifa kutokana na shinikizo la Hammed na wenzake, nasikia siku hiyo Hammed alisakata dansi ndani ya ukumbi wa Umoja wa Mataifa akijipongeza, this goes to show how Hammed was emotionally attached kwa Taifa la Uchina, tangu siku hiyo Uchina ilimchukulia Hammed na Tanzania kuwa marafiki wa kweli, na kusema kweli China inamuheshimu sana Hammed, kama Serikali yetu ingemtumia Hammed kufanya mazungumzo na Serikali ya Uchina kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mbona sinto fahamu kuhusu uwekezaji huo ungetatuliwa kidiplomasia na kwa haraka without offending anyone kwa maneno ya kashfa, eti "Wachina wezi"
Harakati za Hammed kuitetea Uchina umoja wa Mataifa ulimgharimu sana alipo pendekezwa na mataifa mengi Duniani kuwania kiti cha Ukatibu mkuu umoja wa Mataifa (UN), Amerika ilitumia kura yake ya trufu kumkataa Hammed,lakini Balozi wa USA katika Umoja wa Mataifa aliomba msamaha kwa kusema yeye binafsi hana tatizo na Hammed alifanya hivyo kutokana na shinikizo la Serikali ya USA kulipiza kisasi.
Hammed aliwahi vile vile kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu wakati wa utawala wa Mwl. Nyerere na baadae kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa AU wenye makao makuu huko Addis kwa term mbili - Hammed aliwahi kushauriwa mara mbili na Mwl. Nyerere kwamba agombee kiti cha Urais Tanzania lakini Hammed declined/kataa diplomatically, sina shaka Kambarage alihafiki sababu zake za kukataa pendekezo la kuwania kiti cha Urais - wala tusishangae, tuliwahi kushuhudia kashfa alizo zushiwa Hammend wakati anawania kuteuliwa katika kinyanganyiro cha kiti cha Urais huko Zanzibar. Bottom line is: Tunapo toa ushauri kwa nia njema, mara nyingi huwa tuna angalia vitu kama hivyo, hatukurupuki. Sina shaka nime eleweka - Good day.