Profesa Kabudi: Tanzania kupokea ugeni mkubwa kutoka China ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje

Urafiki ulikuwa enzi za nyerere si hawa wachina mabeberu waliopitiliza. Hapa wananchi inabidi tupambane mikataba iwasilishwe bungeni hakuna jinsi
 
Mkuu! Umenikumbusha mbali Sana!!

Makonda alimarufu Daudi Bashite 😂
 
Dah......
 
Wapelekwe Ukanda wa Magharibi ya nchi:
1.wajenge kipande cha SGR kuelekea Kigoma.
2.Wajenge ofisi ya B.O.T kigoma
3.Wajenge EPZ Kigoma
4.Waunde meli 2 za mwendo kasi katika ziwa Tanganyika.
5.Wajenge "International Terminal" Kigoma Airport.
 
Jicho la tatu linaniambia haya:

Ile simu imeanza kufanyiwa kazi.

SGR hiyo kwa wachina

Bandari ya Bagamoyo nayo iko mbioni, na kadhalika.

JK atakuwa anechaka tu huko aliko na kujisemea kiko wapi sasa!

Baada ya Mungu, ni muda- imani yangu.
Huku mataga wameshasahau kwamba meko alichukua mkopo standard chartered bank usd 1.5Bil za kujenga sgr Dar-Makutupora..lakini reli haijafika Makutupora bado, sababu hakuna pesa..na za chini ya kapeti Mturuki anabwaga manyanga.
 
"Kati ya juu" kama Kenya. Ila hawawatangazii raia hivyo, wanawaacha waimbe tu!
Uliisikia wapi hii mkuu?

Basi ujue ulidanganywa. Hawapo "Uchumi wa kati Juu"; huenda unawapamba tu wafurahi, maana hupenda sana sifa hao jamaa.
 
Pumbav.......uuuu
 
Hii sikuipata! Asante kwa ku'share '
 
Hivi CHINA imewahi kuchangia BAJETI yetu kwa maana ya GBS support au wao hutekeleza Miradi yao moja kwa moja kwa ufadhili wa fedha zao? Kwa Takwimu zetu,Bajeti yetu ni tegemezi kwa 35% , sasa Je china wao hutuchangia asilimia ngapi katika hiyo 35% au hakuna? Hili linatakiwa kupewa majibu ili vijana wajue urafiki wetu ni wa kudumu na kusaidiana
 
Jicho la tatu linaniambia haya:

Ile simu imeanza kufanyiwa kazi.

SGR hiyo kwa wachina

Bandari ya Bagamoyo nayo iko mbioni, na kadhalika.

JK atakuwa anechaka tu huko aliko na kujisemea kiko wapi sasa!

Baada ya Mungu, ni muda- imani yangu.
Mkuu huu ndio ukweli, na hii mikopo ya wachina itakuja kutufanyia kitu mbaya kabisa!
Angalieni Zimbabwe, Zambia na Kenya.
 
Hivi waziri wa kawaida kuja Tz ni jambo kubwa?
Mbona tunafanyana mazwazwa?
Wamewahi kuja maraisi wakubwa sana, Mawaziri wakuu wa nchi kubwa mno, leo hii waziri kuna inakuwa ni ugeni mkubwa?
 
Urafiki ulikuwa enzi za nyerere si hawa wachina mabeberu waliopitiliza. Hapa wananchi inabidi tupambane mikataba iwasilishwe bungeni hakuna jinsi
China wa sasa ana malingo hata kuliko Marekani.
China wa sasa anadharau waafrika kama si watu vile,huko Kenya mwekezaji wa kichina alimlamba bakola mkenya kwa kuchelewa kazini.Hata huko Zambia mapambano hayaishi kati ya wazawa na machina.
Hapa kwetu wachina ndio watu wanaomiliki makolokolo ya kucheza kamali hadi vijijini wakiibia wazawa,wakati nchini kwao ni marufuku kucheza makolokolo kiholela.

Kama kweli wachina wanaupendo wa kweli mbona wao ndio wamehujumu kiwanda cha nguo cha Urafiki,Na kubadirisha matumizi ya kiwanda?
Mbona majirani zake China kama Japan,Vietnam, Philippines, Indonesia, Cambodia,Thailand hawana hamu na taifa hilo kwa njama na mambo yake machafu?

Japo uhusiano na taifa hilo haukwepeki lakini sio kila mikataba na China ikawa ya manufaa kwetu,tutaishia kusaga meno.
 
Yan Liprofesa Majalala aisee HOVYO KABISA...China na dunia wapo kwenye 4th Industrial Revolution, lenyewe na Jiwe lake bado linawaza mambo ya Miaka 55 iliyopita, Hovyo Kabisa!
 
Kuna watu wameshajisahau na kudhani kuwa hii nchi ni ya Magufuli na kwa sababu wanamchukia Magufuli basi wanachukia hadi vinavyo muhusu Magufuli. Mtu anaomba Tanzania ipatwe na janga lolote au isifanikiwe kwa kudhani kufanya hivyo inamkomoa mwenye Tanzania yake ambaye ni Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…