Profesa Kabudi: Tanzania kupokea ugeni mkubwa kutoka China ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje

Profesa Kabudi: Tanzania kupokea ugeni mkubwa kutoka China ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje

Urafiki ulikuwa enzi za nyerere si hawa wachina mabeberu waliopitiliza. Hapa wananchi inabidi tupambane mikataba iwasilishwe bungeni hakuna jinsi
 
Ahaaa ahaaa, nimecheka kwa nguvu, eti wapinzani hawataki wageni. Ni kipi wapinzani wanazuia kwa hao wageni. Nakumbuka ile mkutano wa SADC ulivyoandaliwa na propaganda na mikwara kibao. Mpaka Makonda akatoa amri mtu ambaye hajaoga asiingie mjini. Mara pap likazuka gonjwa la corona, mwenyekiti wa SADC akawa Chato hataki kukutana na wakuu wenzake wa nchi za SADC, wajadili namna ya kupambana na Corona! Kwa mtu asiyeijua serikali hii anaweza kudhani ni ugeni wa ajabu, kumbe propaganda tu ndio zinaikuza hiyo safari.
Mkuu! Umenikumbusha mbali Sana!!

Makonda alimarufu Daudi Bashite 😂
 
We unyamaze tu hakuna lolote la maana, ni sawa na mpiga ramli tu. Waziri wa mambo ya nje mwenyewe anakuja rasmi kumwona mwanaume wa shoka nyumbani kwake Chato, wewe unabwabwaja tu. Tanzania is better now under the leadership of JPM.

FYI Xi Jinping anatembelea Tanzania wakati wowote baada ya ziara hiyo. Ni maandalizi tu kwa sababu China na Tanzania ni dam dam, whether you like it or not. China hata siku moja hawawezi kuwasahau Watanzania hasa walivyowapigania kwenye UN enzi za baba wa taifa JKN.
Dah......
 
A free advice.
Badala ya kwenda na kurudi na hawa Wachina, Tanzania isipange kupata tumisaada-saada twa dola milioni 50, 100, 300, 5000.... Ipange karata zake iingie kichwa kichwa na Wachina katika 'strategic partnership'. Kila miaka miatano China iipatie TZ bilioni 10 $ kwa muda wa miaka 50 ijayo. Tanzania ianze kulipa baada ya miaka 20 kwa faida ya 2%
Wachina, wakielezewa vizuri, watakubali, maana wanatafuta mahali penye Amani na Rafiki pa kuhifadhi ma trilioni yao ya dola ambayo sasa yanatishiwa 'kutaifishwa' na Marekani inayofilisika. Tanzania imeisaidia sana China, bila ya faida yeyote ya kueleweka. China iko tayari kuingia na Iran mkataba kama huo, sembuse TZ? Halafu tuna Wachina wengi waliopo serikalini wa kututetea. Chukua kwanza mfano wa balozi aliyepita Dr. Lu Youqing.
Huku kukatiwa vijidola hamsini kila mara hakutatufanya tuendelee. Tunahitaji 'a huge infusion of capital' ku revamp kabisa elimu yetu na agriculture, kabla hatujaendelea. Hii maneno ya "Uchumi wa Kati" tulionao ni 'smokescreen' tu. Mwaka huu huu tutarudi kuwa uchumi maskini. Uchumi wa kati haumaanishi tumeshafika basi tutabaki hivyo hivyo. Kwanza uchumi wa kati wenyewe ni "Kati ya chini" siyo "Kati ya juu" kama Kenya. Ila hawawatangazii raia hivyo, wanawaacha waimbe tu!
Alas! Hatuna 'strategic thinkers' katika tabaka la viongozi wetu. Hatuna hata 'long-term mapping' ya maendeleo yetu. Twategemea matamko ya rais tu kuwa mwongozo! Chukua mfano kauli mbiyu ya 'Uchumi wa viwanda' Inasemwa tu. Hakuna aliyeuliza viwanda gani? Wapi watatokea wajenzi Watanzania wa viwanda hivyo? Tuna mainjinia, ma project managers, ma machine operators, ma programme builders........wa kutosha? Tunataka kiasi gani cha hao watoke kila mwaka katika Vyuo vyetu vikuu?
Hii siyo lele mama! Walioendelea walipanga!
Wapelekwe Ukanda wa Magharibi ya nchi:
1.wajenge kipande cha SGR kuelekea Kigoma.
2.Wajenge ofisi ya B.O.T kigoma
3.Wajenge EPZ Kigoma
4.Waunde meli 2 za mwendo kasi katika ziwa Tanganyika.
5.Wajenge "International Terminal" Kigoma Airport.
 
Jicho la tatu linaniambia haya:

Ile simu imeanza kufanyiwa kazi.

SGR hiyo kwa wachina

Bandari ya Bagamoyo nayo iko mbioni, na kadhalika.

JK atakuwa anechaka tu huko aliko na kujisemea kiko wapi sasa!

Baada ya Mungu, ni muda- imani yangu.
Huku mataga wameshasahau kwamba meko alichukua mkopo standard chartered bank usd 1.5Bil za kujenga sgr Dar-Makutupora..lakini reli haijafika Makutupora bado, sababu hakuna pesa..na za chini ya kapeti Mturuki anabwaga manyanga.
 
"Kati ya juu" kama Kenya. Ila hawawatangazii raia hivyo, wanawaacha waimbe tu!
Uliisikia wapi hii mkuu?

Basi ujue ulidanganywa. Hawapo "Uchumi wa kati Juu"; huenda unawapamba tu wafurahi, maana hupenda sana sifa hao jamaa.
 
Profesa Kabudi amesema Tanzania itapokea ugeni mkubwa kutoka China ukiongozwa na Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo.

Ziara hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa nchi yetu ambayo ina mkataba wa urafiki na China uliosainiwa na Mwalimu Nyerere miaka 55 iliyopita, amesema Prof Kabudi.

Chanzo: Eatv habari!

Maendeleo hayana vyama!
Pumbav.......uuuu
 
Simu ya Rais wa China kwa Rais Magufuli na sasa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo zina lengo moja: Kuwatoa katika Mahubusu za Tanzania, Viongozi Waandamizi zaidi ya 10 ambao wamekamatwa kwa kosa la kutakatisha fedha kwa kuitumia Benki ya Kichina, China Commercial Bank, CCB, ambayo imefungiwa kufanya kazi na Benki Kuu ya Tanzania, tangia Novemba 2020.
Habari zilizopo kwenye Vyombo vya Habari vya Kimataifa zinasema kwamba, Ukaguzi mahususi uliofanywa na BOT katika Benki hiyo ya Kichina ulikuta Vitabu vya Uhasibu vinasema kuwa 'mtaji' wa Benki hiyo ya Kichina ni TShs 20 bilioni na Yuan 2 bilioni.
Lakini 'physically' zilikutwa TShs. 250 bilioni na Yuan 20 bilioni ndani ya 'Safe' ya Benki hiyo.
Benki Kuu ya Tanzania iliwatia mbaroni Viongozi wakuu watano wa CCB, pamoja na Viongozi wengine watano wa Kampuni za Ujenzi za Kichina zinazofanya kazi nchini zenye akaunti 'tata' katika Benki hiyo.
Hali kadhakika, Benki Kuu ya Tanzania ilishangaa kukuta hakuna Mfanyakazi hata mmoja, Mtanzania, katika Benki hiyo. Wafanyakazi wote walikuwa Wachina, ili siri ya 'utakatishaji' fedha isitoke nje.
Jitihada za kuwatoa katika Mahubusu, Wachina hao zimekuwa ngumu na sasa Wakuu wa Kampuni hizo huko China wanakuja Nchini wakiambatana na Waziri wa Mambo ya Nje kuwaombea watoke katika Jela wanakoshikiliwa.
Sintashangaa kumuona DDP Biswalo Mganga akiwa kwenye ujumbe wa "mazungumzo" na baadhi ya Wajumbe wa 'msafara huo mzito' kutoka China.
TShs. 250 bilioni na Yuan 20 bilioni zilizokamatwa kwa utakatishaji ni pesa nyingi sana.
Ongezea Wachina viongozi 10 mahabusu.
Kuwagomboa, China inabidi ijikune kisawasawa.
Hii sikuipata! Asante kwa ku'share '
 
Hivi CHINA imewahi kuchangia BAJETI yetu kwa maana ya GBS support au wao hutekeleza Miradi yao moja kwa moja kwa ufadhili wa fedha zao? Kwa Takwimu zetu,Bajeti yetu ni tegemezi kwa 35% , sasa Je china wao hutuchangia asilimia ngapi katika hiyo 35% au hakuna? Hili linatakiwa kupewa majibu ili vijana wajue urafiki wetu ni wa kudumu na kusaidiana
 
Jicho la tatu linaniambia haya:

Ile simu imeanza kufanyiwa kazi.

SGR hiyo kwa wachina

Bandari ya Bagamoyo nayo iko mbioni, na kadhalika.

JK atakuwa anechaka tu huko aliko na kujisemea kiko wapi sasa!

Baada ya Mungu, ni muda- imani yangu.
Mkuu huu ndio ukweli, na hii mikopo ya wachina itakuja kutufanyia kitu mbaya kabisa!
Angalieni Zimbabwe, Zambia na Kenya.
 
Hivi waziri wa kawaida kuja Tz ni jambo kubwa?
Mbona tunafanyana mazwazwa?
Wamewahi kuja maraisi wakubwa sana, Mawaziri wakuu wa nchi kubwa mno, leo hii waziri kuna inakuwa ni ugeni mkubwa?
 
Urafiki ulikuwa enzi za nyerere si hawa wachina mabeberu waliopitiliza. Hapa wananchi inabidi tupambane mikataba iwasilishwe bungeni hakuna jinsi
China wa sasa ana malingo hata kuliko Marekani.
China wa sasa anadharau waafrika kama si watu vile,huko Kenya mwekezaji wa kichina alimlamba bakola mkenya kwa kuchelewa kazini.Hata huko Zambia mapambano hayaishi kati ya wazawa na machina.
Hapa kwetu wachina ndio watu wanaomiliki makolokolo ya kucheza kamali hadi vijijini wakiibia wazawa,wakati nchini kwao ni marufuku kucheza makolokolo kiholela.

Kama kweli wachina wanaupendo wa kweli mbona wao ndio wamehujumu kiwanda cha nguo cha Urafiki,Na kubadirisha matumizi ya kiwanda?
Mbona majirani zake China kama Japan,Vietnam, Philippines, Indonesia, Cambodia,Thailand hawana hamu na taifa hilo kwa njama na mambo yake machafu?

Japo uhusiano na taifa hilo haukwepeki lakini sio kila mikataba na China ikawa ya manufaa kwetu,tutaishia kusaga meno.
 
Yan Liprofesa Majalala aisee HOVYO KABISA...China na dunia wapo kwenye 4th Industrial Revolution, lenyewe na Jiwe lake bado linawaza mambo ya Miaka 55 iliyopita, Hovyo Kabisa!
 
Kuna watu wameshajisahau na kudhani kuwa hii nchi ni ya Magufuli na kwa sababu wanamchukia Magufuli basi wanachukia hadi vinavyo muhusu Magufuli. Mtu anaomba Tanzania ipatwe na janga lolote au isifanikiwe kwa kudhani kufanya hivyo inamkomoa mwenye Tanzania yake ambaye ni Magufuli.
 
Back
Top Bottom