Profesa Kabudi: Tanzania kupokea ugeni mkubwa kutoka China ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje

Profesa Kabudi: Tanzania kupokea ugeni mkubwa kutoka China ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje

Hawana lolote ni matapeli tu hao. Hakuna faida yoyote unayoweza kupata kwa kumtegemea mchina hata Mugabe amekufa akilifahamu hili na hata Maduro analifahamu hili.

Wazungu wakishakukataa ujue umekwisha, kwenda China ni kupoteza muda tu na kulitumbukiza taifa lako kwenye lindi la madeni. Magufuli angeacha udikteta ndio ingemsaidia lkn sio kwenda kujipendekeza kwa wachina.
 
Mwenzake Jakaya Kikwete alikuwa haogopi ziara za nje na akafika mpaka Beijing
Za-kuambiwa changanya na zako. Kuvumbua dunia kama ni ujasiri sawa, lakini JPM hana sababu ya kufanya hizo safari. Haogopwi mtu. Mwenye shida mguu njiani kwenda dukani.
 
Uliisikia wapi hii mkuu?

Basi ujue ulidanganywa. Hawapo "Uchumi wa kati Juu"; huenda unawapamba tu wafurahi, maana hupenda sana sifa hao jamaa.
Tanzania tumeanza na 'lower middle income' Kenya ni 'upper middle income' cheki. Tena wao wako hapo zamani. Kama huwapendi hilo haliwezi kubadilisha ukweli. Kufa na mfundo wako!
 
Profesa Kabudi amesema Tanzania itapokea ugeni mkubwa kutoka China ukiongozwa na Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo.

Ziara hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa nchi yetu ambayo ina mkataba wa urafiki na China uliosainiwa na Mwalimu Nyerere miaka 55 iliyopita, amesema Prof Kabudi.

Chanzo: Eatv habari!

Maendeleo hayana vyama!
Kuna mtu amewahi kufanya ushoga na china akatomboa?
 
Kina mangungo washaidalalia nje yetu kwa mabeberu wa kichina, soon naona mradi wa Bandari ya bagamoyo unarudi
 
Tanzania tumeanza na 'lower middle income' Kenya ni 'upper middle income' cheki. Tena wao wako hapo zamani. Kama huwapendi hilo haliwezi kubadilisha ukweli. Kufa na mfundo wako!
Lower middle income ni dhoofu Hali hawamudu milo 3 sababu ya kusomeshwa namba
 
Huwezi ukaendelea kwa kujitenga na dunia kwa kujifanya kisiwa. Huwezi endelea bila kushirikiana na mabeberu watazunguka zunguka we at the end ni lzm wampigie magoti beberu, ndie anaetawala dunia kwa kuweka mifumo yote ya pesa, uchumi, siasa kila kitu hata China bila kushirikiana na mabeberu angekuwa Kama sisi tu. Ukiogopa kuibiwa utoendelea kamwe. Maendeleo ni sawa na draft au bao unashindaje sasa bila kuliwa
 
Tanzania tumeanza na 'lower middle income' Kenya ni 'upper middle income' cheki. Tena wao wako hapo zamani. Kama huwapendi hilo haliwezi kubadilisha ukweli. Kufa na mfundo wako!
Sasa hili kweli nalo tuliweke hapa kama 'ubishi'?

Nakuambia bila kuwa na shaka yoyote kwamba Kenya haijawahi hata siku moja kuchungulia "upper Middle Income". Hivi unaelewa maana ya madaraja haya?

Mkuu 'Sijali', wewe ni mkenya?

Kama wewe ni mTanzania, basi unatia aibu sana kwa kuwa na elimu duni kiasi hiki. Sikutukani nakwambia ukweli mtupu.

Kama huna uhakika na jambo, usijifanye wewe unalijua jambo hilo kwa sababu tu ya kutaka kujionyesha nawe unajua kumbe unajiaibisha bure.

Ngoja nikusaidie tu kidogo ili ukatafute taarifa inayopatikana kwa haraka, hata dakika tatu haziishi kwa ku-google tu.
Madaraja haya ya nchi yanahusiana na kipato cha nchi husika. Kenya wapo mbali sana kabla ya kufikia hiyo 'Upper middle income' unayoandika hapa, pamoja na kwamba wao waliwahi (miaka michache iliyopita , nadhani 2018 hivi) kufikia hiyo 'lower middle income', kabla ya Tanzania.

Siwezi "kufa na mfundo" mahali ambapo hapana mfundo wowote. Tanzania itaipita Kenya kiuchumi, utake usitake, hilo ni swala la muda tu!
 
China sio beberu kwa kamusi ya ccm. Beberu ni yule anaepinga udikteta. China ni rafiki na mfadhili mkuu na kimbilio la madikteta ya afrika. China ni rafiki wa raslimali zetu na sio rafiki kwa maana ya rafiki. China hawajali kuhusu demokrasia nyie hata Kama mtauliwa wote na watawala hio haiwahusu wao muhimu ni raslimali zenu.
 
SGR on the move.

Mchina Domo la Mamba.

Ukishakosana na Mzungu, unakuwa huna alternative yeye anakuja na terms zake mezani.

Kwisha kazi. Hakuna ujanja tena
Siyo kama Mungu bado yupo hai...Just wait and see...Hii ngoma hamuijui wala hamuielewi...Mzungu na mchina wote ni viumbe...I still have stake to this and I know every detail about this...Just give it time...Something very beautiful coming into being...
 

The Point: Tanzania's unique relationship with China


30 Jun 2019
The first ever China-Africa Economic and Trade Expo opened in Changsha, capital of Central China's Hunan Province, on Thursday. How can local governments and businesses integrate into the China-Africa development plan? And how is the expo expected to enhance Africa's rapid industrialization and facilitating China's continued economic globalization? Guest: Prof. Palamagamba Kabudi, Tanzania's Minister of Foreign Affairs and East African Cooperation
Source : CTGN

Thanking God for this...Its like a dream but happening...Come on those who know their God shall mount like eagle...
 
Profesa Kabudi amesema Tanzania itapokea ugeni mkubwa kutoka China ukiongozwa na Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo.

Ziara hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa nchi yetu ambayo ina mkataba wa urafiki na China uliosainiwa na Mwalimu Nyerere miaka 55 iliyopita, amesema Prof Kabudi.

Chanzo: Eatv habari!

Maendeleo hayana vyama!
Wachina Tz si wageni tena Tz pashakuwa kwao, kila kona ni mchina na ndie anaelinda maslahi ya Tz kimataifa, Mmarekani akiitaja Tz vibaya jioni yake wachina ndio wanaojibu
 
Back
Top Bottom