Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Ni aibu kubwa kwa mawanasheria nguli tena Profesa kukomaa bila hata aibu eti hii katiba ni madhubuti kisa tu baada ya msiba wa Hayati JPM hakukutokea rabsha.
Hivi kama tungekuwa na katiba inayohitaji uchaguzi ufanyike baada ya Rais kufariki kungetokea maasi? Watu wasingefuata katiba inavyotaka?
Ok achana na hilo Profesa Kabudi hajui kuna wananchi wa kawaida ambao wanaporwa haki zao sababu katiba ya sasa hairuhusu wao kudai haki zao. Mfano katiba ya sasa hairuhusu raia wa kawaida kudai haki za ndugu zao wanapouwawa na watu wanaojulikana au wasiojulikana wasiposhitakiwa na Jamhuri.
Profesa Kabudi hajui kuwa wananchi wa kawaida wanatakiwa kuwa na fursa ya kuwafuta kazi wabunge wazembe na wasiofaa kabla ya muhula wa miaka mitano kuisha?
Hii ni baadhi ya mifano tu ambayo Profesa Kabudi anatakiwa atambue kuwa hitaji ka Katiba mpya sio kwa ajiri ya kulinda maslahi ya taifa pale tunapopata misukosuko. Bali ni kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa.
Pia soma > Prof Kabudi: Katiba tuliyonayo ni madhubuti ndio maana imetuvusha tulipopata matatizo!
Chagu wa Malunde at Segese Khm.