Profesa Makame Mbarawa anatushinda kumng'oa?

Mtoa Mada, umeongea kwa hisia sana kuhusu ubinafsishaji wa Bandari zetu.

Huyo Prof. Mbarawa tunaweza kuwa tunamuonea, huyo anapewa Maelekezo na Boss wake.....

Kwa maoni yangu, jambo la uuzaji/ubinafsishaji wa Bandari tulitakiwa Wananchi wote kusimama na kupinga ili Serikali iachane na mpango huo.

Pia kuna haja ipatikane Katiba Mpya itakayo wapunguzia Mamlaka hawa Viongozi, haiwezekani Kiongozi mwenye miaka 60+ afanye maamuzi ya kuligharimu Taifa kwa miaka 99 zaidi wakati huo Yeye atakuwa ameshapumzika kwa Amani.

Hii sio sahihi, alianza Ben akabinafsisha migodi, Viwanda, Benki n.k na sasa hayupo ila Wanaoumia ni Watanzania

Na huyu naye anafata njia ya Ben na JK vile vile.

Kuna haja wenzetu wa Usalama watusaidie kutuondolea hawa Viongozi kabla hawajashika madaraka makubwa na kutuumiza. Hii ni aibu kwa Nchi.

Wale watakoishi kufika 2050 huko watakuwa na maswali ya kujibu wa Watoto wetu.
Ukimuona kobe juu ya mti kapandishwa. Tumng'oe aliyemweka
 
Swali ambalo limeulizwa sana mkataba huu ni wa muda gani? Wapi palipoandikwa miaka 100? Au wapi palipoandikwa miezi 12 ambayo TPA wamesema? Jibu lipo kwenye kufungu cha 23(4) cha mkataba.

Kifungu hicho kinasema mkataba ukishasainiwa, pande mbili za mkataba (serikali ya TZ na serikali ya Dubai) hakuna upande utakaoruhusiwa kukosoa (denounce), kujitoa (withdraw), kuzuia (suspend) au kuvunja mkataba (terminate) kwa sababu yoyote ile.

Kifungu hicho kinasema hata ikitokea upande mmoja ukashindwa kutekeleza masharti ya mkataba, bado hairuhusiwi kuvunja, wala kujitoa kwenye mkataba huo. Maana yake ni kwamba, Mwarabu akisema atapanua bandari ya Dar iwe kubwa zaidi, halafu akashindwa kufanya hivyo, haturuhusiwi kuvunja mkataba. Sijui unaelewa?

Hawakuishia hapo, kifungu hichohicho kinaeleza kwamba hata tukiingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na Dubai, bado haturuhusiwi kuvunja mkataba (we can not terminate the agreement even in severance of diplomatic relation). Yani hata ikitokea sisi na UAE tumevunja uhusiano wa kibalozi, tukamfurusha balozi wao, bado wataendelea kuendesha bandari yetu. Hata ikitokea tukapigana vita, bado haivunji mkataba. Waaarabu wataendelea kuendesha bandari yetu, penda tusipende.

Kwa lugha rahisi huu mkataba ni wa MILELE. Kwahiyo wale waliokua wanauliza kifungu gani kinachoeleza muda wa mkataba? Ni kifungu cha 23(4). Kinasema mkataba huo ni wa MILELE na MILELE mpaka Kristo atakaporudi kulichukua Kanisa.

Hii ni zaidi ya ndoa ya Kikristo ambayo ukishaapa kanisani, hata kama ana matege, ni wako huyo mpaka kifo kiwatenganishe. Na huu mkataba kifungu cha 23(4) kinasema ukishasaini tu, ngoma ni MILELE. Hakuna namna ya kutoka. Bahati mbaya tumeshasaini tangu October 2022.

Halafu "mjinga" mmoja aliyekua ripota wa TBC huko Namtumbo leo kawa Msemaji wa serikali, amekaa kwenye V8 anatuona Watanzania wote wajinga. Anatuambia eti ni mkataba wa miezi 12. Shame.!

Mnataka kuharibu urithi wa vizazi vyetu sababu ya matumbo? Hivi Nyerere angechumia tumbo tungepata uhuru? Endeleeni kutetea matumbo yenu, sisi tunatetea watoto na wajukuu zenu. Lakini ipo siku mtajibu. Kama si hapa, basi hata mbinguni.
Hapa umeeleza jambo kubwa sana. Huu ni mkataba wa maisha.
 
Twende mdogo mdogo..

Wezi washughulikiwe kama wezi. Na uwekezaji wowote uzingatie manufaa kwa nchi.

Sasa kama umekiri hao ni wezi, mbona unakubali wao kuwa sehemu ya negotiation team kupata muwekezaji mpya.! Ridiculous!
Tuwe wapole sio tunalalamika wakati hakuna mkataba uliosainiwa. Hizi fitina za kutaka hawa jamaa waonekane ni wabovu ni zile zile za miaka yote.

Lakini uzoefu wa ufanisi wetu ni mbovu sana. Bandari yetu inao uwezo wa kuingia pesa hata mara nne ya hiki kinachopatikana tatizo ni wizi wetu na mambo mengi ya kienyeji tuliyonayo.
 
Haisaidii kumlaimu marehemu mjomba wako wew sasa piga kazi, wew si uko Hai? Piga mzigo
Kama marehemu aliiharibu kila kitu asisemwe kisa amekufa?Pengine mzazi alikuwa na mashamba ,nyumba mbalimbali,ng'ombe,mbuzi,maduka halafu akatokea mtoto kwenye familia hiyo mchawi na mwenye roho mbaya akavimiliki vyote hivyo na kuviuza bila utaratibu mwisho wake anapokufa bila kuacha kitu chochote ndugu zake watulie tu kisa amekufa waendelee kupambana na hali zao?
 
Ukimuona kobe juu ya mti kapandishwa. Tumng'oe aliyemweka
Shida ni Katiba yetu iliyompa Rais wa Nchi madaraka makubwa.

Haiwezekani Katiba impe Rais umiliki wa Ardhi na vilivyomo, utasema Rais amekuwa Mungu 🙌
 
Tatizo sio yeye,wa kumng'oa ni huyo aliyemteua

#sa100mustgo
 
Habari Watanzania,

Binafsi nimeamini Prof. Mbarawa hafai kuwa mtumishi katika kiwango cha Uwaziri katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni waziri muoga, waziri picha tu. Ni Profesa aina ya le profeseri, yani yupo kama hayupo, na mambo mengi ya kuudhi na kuuza nchi hufanyika akiwa tuli kama kunyoa kichwa cha mwendawazimu.

Sasa hivi naamini hata Marehemu JPM alikuwa sahihi kumtimulia mbali pasi hata na kueleza sababu za kumtimua.

Ufafanuzi wa TPA kuhusu kuuzwa bandari ya Dar es Salaam (usiniambia eti kukodisha). Ukishakuwa umepewa sehemu kwa miaka 99, hapo umeuziwa, ndio uhalisia. Yani two good generation gonna live with the same contract and ownership, hata Mangugo alikuwa anafikiria sawasawa.

Kwa msioijua bandari ya Dar es Salaam, nawamegea kidogo.

Hao DP World wamepewa gati namba 5 mpaka 8.

Hayo ndiyo magati ambayo tangu enzi za Kikwete na JPM yamekuwa yakiendelezwa sana. Tena kwa gharama kubwa za serikali. Ambacho hakikuwa kikifanyika ni uwekaji wa mitambo ya kisasa tu, ila upanuzi na ujenzi umetumia fedha nyingi sana za serikali.

Mfano gati namba 5, 6, 7, 8 huku ndio asilimia 90 ya mizigo yote ya bandari ya Dsm imekuwa ikishushwa miaka yote.

Ishu ya kusema eti hakuna mkataba, ni uongo, iweje tujue wamepewa eneo hilo. Hicho ni nini?

Kama hawa DP World ni wakombozi wetu hivyo, kwanini wasipewe gati namba 1 hadi 4?!

Waendelee hapo, tuone ukongwe wao.

Miaka 99, akili au matope?

Tupige kura hapa Prof. Makame Mbarawa atupishe kwanza.
Mshukuru sana mnaongoza nguruwe pori maana hii jamhuri imejaa mapoyoyo tu[emoji1787][emoji1787][emoji1787] tunaojua kusoma na kwandika[emoji1787][emoji1787][emoji1787] ooh samahani tunajua na kuvaa suti tu ikifika maswala ya nchi wote tunakuwa misukule [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
JPM hakupandisha mishahara kwa wafanyakazi kazi, kuijenga bandari!
JPM alipora pesa za wafanyabiashara wakwepa kodi kuijenga bandari!
Mwarabu ambaye babu zake waliwafanya watumwa babu zetu anakuja kula keki, yeye kisha kuwarithisha wana, wajukuu na vitukuu vyake!

Salaleee! [emoji848][emoji848]
 
Tuwe wapole sio tunalalamika wakati hakuna mkataba uliosainiwa. Hizi fitina za kutaka hawa jamaa waonekane ni wabovu ni zile zile za miaka yote.

Lakini uzoefu wa ufanisi wetu ni mbovu sana. Bandari yetu inao uwezo wa kuingia pesa hata mara nne ya hiki kinachopatikana tatizo ni wizi wetu na mambo mengi ya kienyeji tuliyonayo.
 
Attachments

  • FB_IMG_1686228048677.jpg
    FB_IMG_1686228048677.jpg
    42.7 KB · Views: 4
Upuuzi.
Wakati Kikwete anagawa gesi kwani wabunge wa upinzani hawakuwepo kututetea?

Wakati Kikwete anataka kugawa bagamoyo kwani hao wapinzani hawakuwepo bungeni? Kwa nini wasingetutetea wakati huo?

Ni ufinyu wa mawazo kumlaumu Magufuli (rip) kwa kosa linalofanywa na Samia. Let's be logical.
Tena nalumbuka zitto alitetea mno mradi wa gesi kwa maneno mengi ya kitapeli.Leo hayajatokea kimyaaa!
 
Swali ambalo limeulizwa sana mkataba huu ni wa muda gani? Wapi palipoandikwa miaka 100? Au wapi palipoandikwa miezi 12 ambayo TPA wamesema? Jibu lipo kwenye kufungu cha 23(4) cha mkataba.

Kifungu hicho kinasema mkataba ukishasainiwa, pande mbili za mkataba (serikali ya TZ na serikali ya Dubai) hakuna upande utakaoruhusiwa kukosoa (denounce), kujitoa (withdraw), kuzuia (suspend) au kuvunja mkataba (terminate) kwa sababu yoyote ile.

Kifungu hicho kinasema hata ikitokea upande mmoja ukashindwa kutekeleza masharti ya mkataba, bado hairuhusiwi kuvunja, wala kujitoa kwenye mkataba huo. Maana yake ni kwamba, Mwarabu akisema atapanua bandari ya Dar iwe kubwa zaidi, halafu akashindwa kufanya hivyo, haturuhusiwi kuvunja mkataba. Sijui unaelewa?

Hawakuishia hapo, kifungu hichohicho kinaeleza kwamba hata tukiingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na Dubai, bado haturuhusiwi kuvunja mkataba (we can not terminate the agreement even in severance of diplomatic relation). Yani hata ikitokea sisi na UAE tumevunja uhusiano wa kibalozi, tukamfurusha balozi wao, bado wataendelea kuendesha bandari yetu. Hata ikitokea tukapigana vita, bado haivunji mkataba. Waaarabu wataendelea kuendesha bandari yetu, penda tusipende.

Kwa lugha rahisi huu mkataba ni wa MILELE. Kwahiyo wale waliokua wanauliza kifungu gani kinachoeleza muda wa mkataba? Ni kifungu cha 23(4). Kinasema mkataba huo ni wa MILELE na MILELE mpaka Kristo atakaporudi kulichukua Kanisa.

Hii ni zaidi ya ndoa ya Kikristo ambayo ukishaapa kanisani, hata kama ana matege, ni wako huyo mpaka kifo kiwatenganishe. Na huu mkataba kifungu cha 23(4) kinasema ukishasaini tu, ngoma ni MILELE. Hakuna namna ya kutoka. Bahati mbaya tumeshasaini tangu October 2022.

Halafu "mjinga" mmoja aliyekua ripota wa TBC huko Namtumbo leo kawa Msemaji wa serikali, amekaa kwenye V8 anatuona Watanzania wote wajinga. Anatuambia eti ni mkataba wa miezi 12. Shame.!

Mnataka kuharibu urithi wa vizazi vyetu sababu ya matumbo? Hivi Nyerere angechumia tumbo tungepata uhuru? Endeleeni kutetea matumbo yenu, sisi tunatetea watoto na wajukuu zenu. Lakini ipo siku mtajibu. Kama si hapa, basi hata mbinguni.
Iwekenihapa hiyo article 20 ya mkata ili tuone
 
Siyo kulishana matango pori,
 
Habari Watanzania,

Binafsi nimeamini Prof. Mbarawa hafai kuwa mtumishi katika kiwango cha Uwaziri katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni waziri muoga, waziri picha tu. Ni Profesa aina ya le profeseri, yani yupo kama hayupo, na mambo mengi ya kuudhi na kuuza nchi hufanyika akiwa tuli kama kunyoa kichwa cha mwendawazimu.

Sasa hivi naamini hata Marehemu JPM alikuwa sahihi kumtimulia mbali pasi hata na kueleza sababu za kumtimua.

Ufafanuzi wa TPA kuhusu kuuzwa bandari ya Dar es Salaam (usiniambia eti kukodisha). Ukishakuwa umepewa sehemu kwa miaka 99, hapo umeuziwa, ndio uhalisia. Yani two good generation gonna live with the same contract and ownership, hata Mangugo alikuwa anafikiria sawasawa.

Kwa msioijua bandari ya Dar es Salaam, nawamegea kidogo.

Hao DP World wamepewa gati namba 5 mpaka 8.

Hayo ndiyo magati ambayo tangu enzi za Kikwete na JPM yamekuwa yakiendelezwa sana. Tena kwa gharama kubwa za serikali. Ambacho hakikuwa kikifanyika ni uwekaji wa mitambo ya kisasa tu, ila upanuzi na ujenzi umetumia fedha nyingi sana za serikali.

Mfano gati namba 5, 6, 7, 8 huku ndio asilimia 90 ya mizigo yote ya bandari ya Dsm imekuwa ikishushwa miaka yote.

Ishu ya kusema eti hakuna mkataba, ni uongo, iweje tujue wamepewa eneo hilo. Hicho ni nini?

Kama hawa DP World ni wakombozi wetu hivyo, kwanini wasipewe gati namba 1 hadi 4?!

Waendelee hapo, tuone ukongwe wao.

Miaka 99, akili au matope?

Tupige kura hapa Prof. Makame Mbarawa atupishe kwanza.
Bado yupo ofisini, anadunda tu..
 
Back
Top Bottom