Habari Watanzania,
Binafsi nimeamini Prof. Mbarawa hafai kuwa mtumishi katika kiwango cha Uwaziri katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni waziri muoga, waziri picha tu. Ni Profesa aina ya le profeseri, yani yupo kama hayupo, na mambo mengi ya kuudhi na kuuza nchi hufanyika akiwa tuli kama kunyoa kichwa cha mwendawazimu.
Sasa hivi naamini hata Marehemu JPM alikuwa sahihi kumtimulia mbali pasi hata na kueleza sababu za kumtimua.
Ufafanuzi wa TPA kuhusu kuuzwa bandari ya Dar es Salaam (usiniambia eti kukodisha). Ukishakuwa umepewa sehemu kwa miaka 99, hapo umeuziwa, ndio uhalisia. Yani two good generation gonna live with the same contract and ownership, hata Mangugo alikuwa anafikiria sawasawa.
Kwa msioijua bandari ya Dar es Salaam, nawamegea kidogo.
Hao DP World wamepewa gati namba 5 mpaka 8.
Hayo ndiyo magati ambayo tangu enzi za Kikwete na JPM yamekuwa yakiendelezwa sana. Tena kwa gharama kubwa za serikali. Ambacho hakikuwa kikifanyika ni uwekaji wa mitambo ya kisasa tu, ila upanuzi na ujenzi umetumia fedha nyingi sana za serikali.
Mfano gati namba 5, 6, 7, 8 huku ndio asilimia 90 ya mizigo yote ya bandari ya Dsm imekuwa ikishushwa miaka yote.
Ishu ya kusema eti hakuna mkataba, ni uongo, iweje tujue wamepewa eneo hilo. Hicho ni nini?
Kama hawa DP World ni wakombozi wetu hivyo, kwanini wasipewe gati namba 1 hadi 4?!
Waendelee hapo, tuone ukongwe wao.
Miaka 99, akili au matope?
Tupige kura hapa Prof. Makame Mbarawa atupishe kwanza.
Swali ambalo limeulizwa sana mkataba huu ni wa muda gani? Wapi palipoandikwa miaka 100? Au wapi palipoandikwa miezi 12 ambayo TPA wamesema? Jibu lipo kwenye kufungu cha 23(4) cha mkataba.
Kifungu hicho kinasema mkataba ukishasainiwa, pande mbili za mkataba (serikali ya TZ na serikali ya Dubai) hakuna upande utakaoruhusiwa kukosoa (denounce), kujitoa (withdraw), kuzuia (suspend) au kuvunja mkataba (terminate) kwa sababu yoyote ile.
Kifungu hicho kinasema hata ikitokea upande mmoja ukashindwa kutekeleza masharti ya mkataba, bado hairuhusiwi kuvunja, wala kujitoa kwenye mkataba huo. Maana yake ni kwamba, Mwarabu akisema atapanua bandari ya Dar iwe kubwa zaidi, halafu akashindwa kufanya hivyo, haturuhusiwi kuvunja mkataba. Sijui unaelewa?
Hawakuishia hapo, kifungu hichohicho kinaeleza kwamba hata tukiingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na Dubai, bado haturuhusiwi kuvunja mkataba (we can not terminate the agreement even in severance of diplomatic relation). Yani hata ikitokea sisi na UAE tumevunja uhusiano wa kibalozi, tukamfurusha balozi wao, bado wataendelea kuendesha bandari yetu. Hata ikitokea tukapigana vita, bado haivunji mkataba. Waaarabu wataendelea kuendesha bandari yetu, penda tusipende.
Kwa lugha rahisi huu mkataba ni wa MILELE. Kwahiyo wale waliokua wanauliza kifungu gani kinachoeleza muda wa mkataba? Ni kifungu cha 23(4). Kinasema mkataba huo ni wa MILELE na MILELE mpaka Kristo atakaporudi kulichukua Kanisa.
Hii ni zaidi ya ndoa ya Kikristo ambayo ukishaapa kanisani, hata kama ana matege, ni wako huyo mpaka kifo kiwatenganishe. Na huu mkataba kifungu cha 23(4) kinasema ukishasaini tu, ngoma ni MILELE. Hakuna namna ya kutoka. Bahati mbaya tumeshasaini tangu October 2022.
Halafu "mjinga" mmoja aliyekua ripota wa TBC huko Namtumbo leo kawa Msemaji wa serikali, amekaa kwenye V8 anatuona Watanzania wote wajinga. Anatuambia eti ni mkataba wa miezi 12. Shame.!
Mnataka kuharibu urithi wa vizazi vyetu sababu ya matumbo? Hivi Nyerere angechumia tumbo tungepata uhuru? Endeleeni kutetea matumbo yenu, sisi tunatetea watoto na wajukuu zenu. Lakini ipo siku mtajibu. Kama si hapa, basi hata mbinguni.