Profesa Mkenda aapa kutotoa vibali vya kuagiza sukari

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema yuko tayari kuachia ngazi nafasi ya uwaziri kuliko kutoa kibali kwa wafanyabiashara cha kuagiza sukari kutoka nje ya nchi.

Profesa Mkenda amesema hayo leo Agosti 30 jijini Dodoma wakati akizindua ripoti ya sensa ya kilimo, mifugo na uvuvi ya mwaka wa kilimo 2019/2020.

Amesema kumekuwa na shinikizo toka kwa wafanyabiashara wanaokwenda kuisumbua Bodi ya Sukari kutaka kibali cha kuagiza sukari nje ya nchi.

“Unajua sukari ni kama dawa za kulevya, ina hela nyingi na kila mtu anataka kufanya biashara hiyo. Kuna mwaziri wa kilimo wameondoka kwa sababu ya kutoa vibali vya sukari. Mimi sitoi ng’o,” amesema Profesa Mkenda.

Amesema pamoja na fitina zinazofanywa kutaka kutolewa vibali vya sukari kwake hatotekeleza hilo.
Profesa Mkenda amesema viwanda vya sukari kwa muda mrefu vimeshindwa kupanuka viwanda vyao kuongeza uzalishaji wa sukari kwa sababu ya sukari inayoagizwa kutoka nje.

Amesema Tanzania inaagiza sukari toka Malawi, Uganda na Zambia wakati miwa mingi inazalishwa Tanzania.

Profesa Mkenda amesema kila mwaka katika bonde la Kilombero inatupwa miwa tani 350,000 huku wakulima wa Mtibwa wakiacha kulima miwa kabisa kwa sababu viwanda vya sukari uwezo wake wa uzalishaji ni mdogo na miwa ni mingi.

Amesema Serikali iliamua kupitisha sheria kwamba uagizaji wa sukari utafanywa na wenye viwanda vya sukari nchini wanazalisha kuanzia tani 10,000 na kuendelea.

Profesa Mkenda amesema uagizaji holela wa sukari umesababisha ukosefu wa ajira, ukosefu wa kodi ya Serikali na wakulima kukosa soko la miwa.

MWANANCHI
 
Mi nakuletea mpunga mrefu nione kama utakataa
Nalog off
 
Okay....
Sasa kama hatoi vibali, then nini solution aliokujanayo kwa sukari kuadimika?
Anyway, najararibu kuwaza kwamba badala yake nini sasa kifanyike?
 
Prof ana point. Nimekuwa nikihoji mara nyingi kwa nini viwanda vya sukari havipanuliwi ili kuongeza uzalishaji? Kama tatizo ni mtaji si viende soko la hisa. Hakuna kiwanda cha sukari hata kimoja kiko kwenye soko la hisa.

Hata huu utaratibu wa kuwapa vibali vya kuagiza sukari wenye viwanda unatakiwa kuangalia upya.

Viwanda lazima vipewe malengo ya kuzalisha. Na idadi ya tani wanayoruhisiwa kuagiza ipungue kila mwaka ili kuwapa chachu ya kupanua uzalishaji. Kama mwaka huu wameagiza tani 10000 mwaka nunu yake hivyo hivyo hadi ifike 0
 
Okay....
Sasaama hatoi vibali, then nini solution aliokujanayo kwa sukari kuadimika?
Anyway, jararibu kuwaza kwamba badala yake nini sasa kifanyike?
Alisema atawapa vibali wazalishaji wa ndani kuagiza..

Lakini bado naona kuna siasa kwenye sukari..kwanini viwanda visiongeze uzalishaji?..miwa hailimiki?
 
Prof. Mkenda kwa kweli ni Waziri muadilifu na ameweza ile Wizara ya Kilimo. Alipokuwa Katibu Mkuu wizara ya maliasili na Waziri wake kwa kusimamia ukweli. Huyu anatakiwa apandishwe cheo na kupewa Wizara nyeti.
 
Prof ana point. Nimekuwa nikihoji mara nyingi kwa nini viwanda vya sukari havipanuliwi ili kuongeza uzalishaji? Kama tatizo ni mtaji si viende soko la hisa. Hakuna kiwanda cha sukari hata kimoja kiko kwenye soko la hisa.

Hata huu utaratibu wa kuwapa vibali vya kuagiza sukari wenye viwanda unatakiwa kuangalia upya.

Viwanda lazima vipewe malengo ya kuzalisha. Na idadi ya tani wanayoruhisiwa kuagiza ipungue kila mwaka ili kuwapa chachu ya kupanua uzalishaji. Kama mwaka huu wameagiza tani 10000 mwaka nunu yake hivyo hivyo hadi ifike 0
Ila sukari isiadimike wala kupanda bei. Ila tatizo kubwa liko kwa watanzani,kuna nchi waliandamani sababu mikate ilipanda bei.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Prof ana point. Nimekuwa nikihoji mara nyingi kwa nini viwanda vya sukari havipanuliwi ili kuongeza uzalishaji? Kama tatizo ni mtaji si viende soko la hisa. Hakuna kiwanda cha sukari hata kimoja kiko kwenye soko la hisa.

Hata huu utaratibu wa kuwapa vibali vya kuagiza sukari wenye viwanda unatakiwa kuangalia upya.

Viwanda lazima vipewe malengo ya kuzalisha. Na idadi ya tani wanayoruhisiwa kuagiza ipungue kila mwaka ili kuwapa chachu ya kupanua uzalishaji. Kama mwaka huu wameagiza tani 10000 mwaka nunu yake hivyo hivyo hadi ifike 0
Kwa vile viwanda vya Serikali ,Mbigili MVOMERO na pwani Kibaha vikefikia wapi?
 
Prof. Mkenda kwa kweli ni Waziri muadilifu na ameweza ile Wizara ya Kilimo. Alipokuwa Katibu Mkuu wizara ya maliasili na Waziri wake kwa kusimamia ukweli. Huyu anatakiwa apandishwe cheo na kupewa Wizara nyeti.
Unamaanisha hiyo yenye sukar si nyeti
 
Atatoa tu bana wafanyabiashara watamuhujumu tu afukuzwe
Kweli kabisa. Kwa Tanzania ya huyu bibi watanzania wote washaota sharubu kama kambale.

Wafanyabiashara wa gesi wamemgomea aziri Kalemani kwenye katazo lake la kuzuia kupanda kwa bei ya gesi. Hata huyu hili la vibali atalegeza tu.
 
Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema yuko tayari kuachia ngazi nafasi ya uwaziri kuliko kutoa kibali kwa wafanyabiashara cha kuagiza sukari kutoka nje ya nchi.

Profesa Mkenda amesema hayo leo Agosti 30 jijini Dodoma wakati akizindua ripoti ya sensa ya kilimo, mifugo na uvuvi ya mwaka wa kilimo 2019/2020.

Amesema kumekuwa na shinikizo toka kwa wafanyabiashara wanaokwenda kuisumbua Bodi ya Sukari kutaka kibali cha kuagiza sukari nje ya nchi.

“Unajua sukari ni kama dawa za kulevya, ina hela nyingi na kila mtu anataka kufanya biashara hiyo. Kuna mwaziri wa kilimo wameondoka kwa sababu ya kutoa vibali vya sukari. Mimi sitoi ng’o,” amesema Profesa Mkenda.

Amesema pamoja na fitina zinazofanywa kutaka kutolewa vibali vya sukari kwake hatotekeleza hilo.
Profesa Mkenda amesema viwanda vya sukari kwa muda mrefu vimeshindwa kupanuka viwanda vyao kuongeza uzalishaji wa sukari kwa sababu ya sukari inayoagizwa kutoka nje.

Amesema Tanzania inaagiza sukari toka Malawi, Uganda na Zambia wakati miwa mingi inazalishwa Tanzania.

Profesa Mkenda amesema kila mwaka katika bonde la Kilombero inatupwa miwa tani 350,000 huku wakulima wa Mtibwa wakiacha kulima miwa kabisa kwa sababu viwanda vya sukari uwezo wake wa uzalishaji ni mdogo na miwa ni mingi.

Amesema Serikali iliamua kupitisha sheria kwamba uagizaji wa sukari utafanywa na wenye viwanda vya sukari nchini wanazalisha kuanzia tani 10,000 na kuendelea.

Profesa Mkenda amesema uagizaji holela wa sukari umesababisha ukosefu wa ajira, ukosefu wa kodi ya Serikali na wakulima kukosa soko la miwa.

MWANANCHI
Ajiapushe tuu ila sukari isije kupanda bei hatuta muelewa na viapo vyake.
 
Back
Top Bottom