Profesa Mkenda aapa kutotoa vibali vya kuagiza sukari

Profesa Mkenda aapa kutotoa vibali vya kuagiza sukari

Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema yuko tayari kuachia ngazi nafasi ya uwaziri kuliko kutoa kibali kwa wafanyabiashara cha kuagiza sukari kutoka nje ya nchi.

Profesa Mkenda amesema hayo leo Agosti 30 jijini Dodoma wakati akizindua ripoti ya sensa ya kilimo, mifugo na uvuvi ya mwaka wa kilimo 2019/2020.

Amesema kumekuwa na shinikizo toka kwa wafanyabiashara wanaokwenda kuisumbua Bodi ya Sukari kutaka kibali cha kuagiza sukari nje ya nchi.

“Unajua sukari ni kama dawa za kulevya, ina hela nyingi na kila mtu anataka kufanya biashara hiyo. Kuna mwaziri wa kilimo wameondoka kwa sababu ya kutoa vibali vya sukari. Mimi sitoi ng’o,” amesema Profesa Mkenda.

Amesema pamoja na fitina zinazofanywa kutaka kutolewa vibali vya sukari kwake hatotekeleza hilo.
Profesa Mkenda amesema viwanda vya sukari kwa muda mrefu vimeshindwa kupanuka viwanda vyao kuongeza uzalishaji wa sukari kwa sababu ya sukari inayoagizwa kutoka nje.

Amesema Tanzania inaagiza sukari toka Malawi, Uganda na Zambia wakati miwa mingi inazalishwa Tanzania.

Profesa Mkenda amesema kila mwaka katika bonde la Kilombero inatupwa miwa tani 350,000 huku wakulima wa Mtibwa wakiacha kulima miwa kabisa kwa sababu viwanda vya sukari uwezo wake wa uzalishaji ni mdogo na miwa ni mingi.

Amesema Serikali iliamua kupitisha sheria kwamba uagizaji wa sukari utafanywa na wenye viwanda vya sukari nchini wanazalisha kuanzia tani 10,000 na kuendelea.

Profesa Mkenda amesema uagizaji holela wa sukari umesababisha ukosefu wa ajira, ukosefu wa kodi ya Serikali na wakulima kukosa soko la miwa.

MWANANCHI
Lakini kwa nini wasitafute muwekezaji anaeweza kuziba hilo pengo hata kwa kumpa tax holiday?

Afu wakajifunze Uganda,Malawi na Zambia
 
Profesa mbona haeleweki!? Kwahiyo viwanda kuwa na uzalishaji duni usiokidhi mahitaji ya soko suluhisho ni kunyima vibali vya kuagiza nje?
Sukari si inaagizwa sababu kuna shortage au bei pengine ni kubwa?

Kwanini asiimize viwanda vizalishe zaidi ambapo bei lazima tu itashuka na automatically hakuna atakayeagiza sukari nje, cha zaidi sisi tutaanza kuexport.
 
Case study: Kiwanda cha baiskeli aina ya Swala hapa Tanzania...mwekezaji wa kiwanda hicho aliamua kuachana na uzalishaji na badala yake akawa muagizaji wa baiskeli za mitumba na kiwanda kikajifia.... Wenye viwanda vya sukari kupewa vibali kuagiza sukari tunarudi like kule kwenye kiwanda cha baiskeli!
Wasukuma tunapenda baiskeli asikwambie mtu, tunaikumbuka Sana Swala!
 
Prof ana point. Nimekuwa nikihoji mara nyingi kwa nini viwanda vya sukari havipanuliwi ili kuongeza uzalishaji? Kama tatizo ni mtaji si viende soko la hisa. Hakuna kiwanda cha sukari hata kimoja kiko kwenye soko la hisa.

Hata huu utaratibu wa kuwapa vibali vya kuagiza sukari wenye viwanda unatakiwa kuangalia upya.

Viwanda lazima vipewe malengo ya kuzalisha. Na idadi ya tani wanayoruhisiwa kuagiza ipungue kila mwaka ili kuwapa chachu ya kupanua uzalishaji. Kama mwaka huu wameagiza tani 10000 mwaka nunu yake hivyo hivyo hadi ifike 0
Kiwanda kinahitaji sera rafiki. Uzalishaji wa Tanzania umekabwa na tozo, kodi,na teknolojia duni mpaka unasababisha bei ya sukari zinazoagizwa ziwe nafuu sana kulinganisha na hapa kwetu.

Solution ni kuangalia comparatively kuanzia sera, kodi, ruzuku kwa wakulima, riba za mikopo, nk, tujione sisi tunakwama wapi.
 
Awe na akiba na maneno, sukari ikifika 5000 kwa kilo ndio atajua maana ya mdomo huponza kichwa
 
Sukari ikipanda bei tutadai kichwa chake. Angetuambia sukari inaoza kwenye maghala ya viwanda vya ndani kwa kukosa soko kwasababu ya sukari inayo toka nje kidogo ange eleweka.

Serikali iondoe huu ukiritimba wa kutoa vibali vya kuagiza sukari ijikite kusimamia ubora wa sukari inayoingizwa sokoni tuone kama kilo ya sukari siitakuwa 1,000/-, hili sharti la vibali vya sukari ndio linalo ipa sukari sifa isizokuwa nazo eti"white gold, mawee!" Ondoeni vibali wekeni masharti ya kulinda ubora wa sukari muone kama bei ya sokoni ya sukari haita poromoka na kuwanufaisha walaji. Kwani wanatoa vibali vya kuagiza chumvi? Chumvi si inazalishwa ndani ya nchi na nyingine inaagizwa nje?

Uamuzi huu wa Waziri si wakupongezwa bali ni wakutiliwa mashaka. Je Waziri ana nini na wanaodhibiti/ control soko la sukari?
 
Nitaendelea kumheshimu sana huyu waziri kwa misimamo kama hii. Kama nchi ina kila kitu cha kuwezesha kuzalisha sukari kwa wingi, kwa nini tuendelee kuagiza sukari.

Misimamo kama hii ilitakiwa ndiyo aisimamie Rais wa nchi, na sehemu ya matatizo yetu mengi tungeyamaliza.

Lile swala la ku'promote' mbolea ya kampuni moja liliniondolea uamini kwake, lakini huenda kulikuwepo na sababu ambayo haikuelezwa.
 
Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema yuko tayari kuachia ngazi nafasi ya uwaziri kuliko kutoa kibali kwa wafanyabiashara cha kuagiza sukari kutoka nje ya nchi.

Profesa Mkenda amesema hayo leo Agosti 30 jijini Dodoma wakati akizindua ripoti ya sensa ya kilimo, mifugo na uvuvi ya mwaka wa kilimo 2019/2020.

Amesema kumekuwa na shinikizo toka kwa wafanyabiashara wanaokwenda kuisumbua Bodi ya Sukari kutaka kibali cha kuagiza sukari nje ya nchi.

“Unajua sukari ni kama dawa za kulevya, ina hela nyingi na kila mtu anataka kufanya biashara hiyo. Kuna mwaziri wa kilimo wameondoka kwa sababu ya kutoa vibali vya sukari. Mimi sitoi ng’o,” amesema Profesa Mkenda.

Amesema pamoja na fitina zinazofanywa kutaka kutolewa vibali vya sukari kwake hatotekeleza hilo.
Profesa Mkenda amesema viwanda vya sukari kwa muda mrefu vimeshindwa kupanuka viwanda vyao kuongeza uzalishaji wa sukari kwa sababu ya sukari inayoagizwa kutoka nje.

Amesema Tanzania inaagiza sukari toka Malawi, Uganda na Zambia wakati miwa mingi inazalishwa Tanzania.

Profesa Mkenda amesema kila mwaka katika bonde la Kilombero inatupwa miwa tani 350,000 huku wakulima wa Mtibwa wakiacha kulima miwa kabisa kwa sababu viwanda vya sukari uwezo wake wa uzalishaji ni mdogo na miwa ni mingi.

Amesema Serikali iliamua kupitisha sheria kwamba uagizaji wa sukari utafanywa na wenye viwanda vya sukari nchini wanazalisha kuanzia tani 10,000 na kuendelea.

Profesa Mkenda amesema uagizaji holela wa sukari umesababisha ukosefu wa ajira, ukosefu wa kodi ya Serikali na wakulima kukosa soko la miwa.

MWANANCHI
Tatizo la baadhi ya viwanda kuna wakati tajiri mmoja anahodhi sukari karibu yote halafu anzuia mzunguko(uuzaji) na wakti huohuo kiwanda kinasimamisha uzalishaji hivyo kufanya sukari kuadimika mtaani na ghafla bei inakuwa juu, yaani baadhi ya viwanda ni usanii mtupu. Utashangaa kiwanda kinafungwa kwa muda wakati malighafi ambayo ni miwa imejaa kibao.
 
Kumbe Mkenda Ni mgeni sana hapa Tanzania.
Kwanza kabisa Tanzania uzalishaji wa white sugar Ni mdogo sana wakati viwanda vya soda vinatumia white sugar kutengeneza hiyo sumu yao.
Kuna matajiri hapa Tanzania ambao Hawa shout Kama boss wa mikia lkn kauli zao Ni very effective kwenye uendeshwaji wa wizara.
Namhakikishia Mkenda SIMU MOJA TUH ATASAINI VIBALI. NIMEGUNDUA HUYU MKENDA ATAKUA KAMA HAJI MANARA.
 
Prof ana point. Nimekuwa nikihoji mara nyingi kwa nini viwanda vya sukari havipanuliwi ili kuongeza uzalishaji? Kama tatizo ni mtaji si viende soko la hisa. Hakuna kiwanda cha sukari hata kimoja kiko kwenye soko la hisa.

Hata huu utaratibu wa kuwapa vibali vya kuagiza sukari wenye viwanda unatakiwa kuangalia upya.

Viwanda lazima vipewe malengo ya kuzalisha. Na idadi ya tani wanayoruhisiwa kuagiza ipungue kila mwaka ili kuwapa chachu ya kupanua uzalishaji. Kama mwaka huu wameagiza tani 10000 mwaka nunu yake hivyo hivyo hadi ifike 0
Sasa kiwanda kama Mtibwa, yaani choka mbaya maboiler wanatumia kuni karne hii? Wananchi wanaozunguka kiwanda wana uwezo mkubwa wa kuzalisha maelfu ya Tani za miwa na kuuza kiwandani but kiwanda hakuna uwezo. Angalau kiwanda ambacho wako serious ni TPC Moshi, wako very modern, umeme wanazalisha wenyewe mpaka wanawagawia vijiji jirani.
 
Hapo hapo utambue, hakuna nchi isiyokuwa na 'protectionism', kwa hiyo utambue umuhimu wake.

Protectionism kwa gharama ya wananchi walio kuamini uwaongoze na kwa faida ya nani? Hii ni wananchi victimization sijui ndio tuite victimism.

Kuna wakati Museveni akitangaza sukari Uganda iko ya kumwaga viwanda vyao vimezalisha ziada. Wafanyabiashara wangeruhusiwa ili mradi wanatimiza vigezo na mashariti kuzingatiwa na kuingiza kwa masemi trela wakaileta na pengine bei ingeshuka. Lakini aah wapi mamilioni ya watumiaji sukari wanaumizwa ili kulinda kiwanda chenye wafanya pengine 2000 na tajiri wake. Viwanda venyewe havitosheleze soko na kufanya bei ya bidhaa kuwa juu.
 
Sasa kiwanda kama Mtibwa, yaani choka mbaya maboiler wanatumia kuni karne hii? Wananchi wanaozunguka kiwanda wana uwezo mkubwa wa kuzalisha maelfu ya Tani za miwa na kuuza kiwandani but kiwanda hakuna uwezo. Angalau kiwanda ambacho wako serious ni TPC Moshi, wako very modern, umeme wanazalisha wenyewe mpaka wanawagawia vijiji jirani.

Kuni kwa level ya kiwanda! Waharibu misitu/ mazingira wanachekewa na kulindwa/ protectionism.
 
Juzi nimekunywa coca ina lad has ya miwa, na ile sugaring ya kupikia keki je?
 
Bei sukari mitaani ni Kati ya shs2,800 mpaka 3,000 kwa kilo hapa Dar es salaam.Waziri Kama hatoi vibali vya uagizaji sukari kutoka nje kwa wafanya biashara ni sawa,lakini akutane na wenye viwanda kuweka mkakati wa kuongeza uzalishaji sukari wa ndani, ili kuokoa tani 150,000 za miwa inayoharibika /kwa kuto nunuliwa na wenye viwanda,pili walaji wa mwisho wapate sukari kwa bei nafuu.
 
Sijui kwanini Bashe huwa hapewi Uwaziri kamili.
Kwa utaratibu tunaoenda nao Bashe atapewa huo uwaziri lakini Prof. Mkenda msimamo na kauli yake bado itaendelea kuwa na mashiko;
Wenye viwanda vya sukari wananunua sukari ilizoisha muda na ya viwango vya chini nje ya nchi na pia kupitia Zanzibar kwa gharama ya chini kufikia 40% ya gharama ya uzalishaji hapa nchini; kule Kilombero balozi Mpungwe amewasaliti ndugu zake kwa kutonunua miwa yao aidha wamiliki wa viwanda hivyo (waarabu na wahindi) wanaushawishi mkubwa serikalini siku hizi na Prof. Mkenda analifahamu hilo;
Namshauri Prof. Mkenda ashirikiane na mawaziri wenzake wa sekta shiriki (Viwanda & Biashara na Uwekezaji) chini ya Mhe. Waziri Mkuu ktk kusimamia na kudhibiti uzalishaji wa sukari viwandani!
 
Back
Top Bottom