Profesa Mkenda aapa kutotoa vibali vya kuagiza sukari

Lakini kwa nini wasitafute muwekezaji anaeweza kuziba hilo pengo hata kwa kumpa tax holiday?

Afu wakajifunze Uganda,Malawi na Zambia
Dangote ndiye mwekezaji pekee mwenye uwezo mkubwa wa kujenga kiwanda kikubwa cha kuzalisha Sukari nchini lakini mambo yalivyo hivi sasa atapigwa vita na mamafia wabobezi wa kuagiza sukari kutoka nje - waagizaji hawa wa sukari wana mizizi na ushawishi mkubwa kwenye mission critical sectors nchini na hawajiwahi kushindwa kitu wakidhamilia na nawahakikishieni its a question of time kabla hawajapewa kibali kwa mara nyingine tena cha ku-import substandard na rebagged (huko Dubai) expired commodity/Sugar kutoka Brazil na India, pretending to import industrial sugar wanapewa rebate na Serikali halafu sukari inaiingizwa sokoni kama kawa kwa kukwepa kodi stahiki kwa kisingizio cha Industrial Sugar - wanahujumu viwanda vyetu visikuwe.

Big importers wa sukari wana generate matrillion of Tsh big time bila ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya Sukari - namkubusha Profesa kwamba kundi hili si lelemama litakujengea hoja nzito discretely halafu ujikute aidha anahamishiwa Wizara nyingine au anarudishwa kufundisha Chuo Kikuu. Kwa nini Profesa hajiulizi iweje hawa wafanya biashara wanakuwa na ujasiri wa kushikiza Bodi ya Sukari iwapatie vibali vya kuimport sukari, jeuri hii ya kukihuka maagizo ya the late Dr.Magufuli kupiga marufuku utoaji wa vibali - jeuri hii wafanya biashara hao wanaipata wapi? Binafsi naona kuna kitu wanajiamini si Bure. Mzalendo Prof.Mkenda weka uzalendo mbele historia ndiyo itakuhukumu huo ndio ushauri wangu - barikiwa sana.
 
Watu wanataka sukari kwa bei nzuri sio siasa, sasa kama viwanda haviwezi kuzalisha mzigo ndio mnapelekea wananchi, hiyo mikodi yenu,umeme usioeleweka, miundo mbinu mibovu, mikopo ya Bank isiyowezekana ndio issue inayoua viwanda vya ndani na sio sukari tuu, jiandaeni kula sukari guru
 
Dangote ndiye mwekrzaji pekee mwenye uwezo mkubwa wa kujenga kiwanda kikubwa cha kuzalisha Sukari nchinilakinimambo yalivyo hivi sasa atapigwa vita na mamafia wabobezi wa kuagiza sukari kutoka nje - waagizaji hawa wa sukari wana mizizi na ushawishi mkubwa kwenye mission critical sectors nchini na hawajiwahi kushindwa kitu wakidhamilia na nawahakikishieni its a question of time kabla hawajapewa kibali tena cha ku-import substandard na rebagged (huko Dubai) expired commodity/Sugar kutoka Brazil na India, pretending to import industrial sugar wanapewa rebate na Serikali halafu sukari inaiingizwa sokoni kama kawa - wanahujumu viwanda vyetu visikuwe. Wana generate matrillion of Tsh big time bila ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya Sukari - namkubusha Profesa kwamba kundi hili si lelemama ayajengewa hoja nzito aidha ajikutanahamishwa Wizara
Boss kuanzisha kiwanda kwa ule umeme wa TZ na ile mikodi ni kujitafutia umaskini tuu
 
Mkuu kinapo kuja suala la uzalishaji umeme mbona viwanda vya sukari vina uwezo was ku-generate umeme kwa kutumia super heated steam kuendeshea steam turbines za kuzungusha generator za kuzalisha umeme, wala viwanda haviitaji mafuta ya diesel,mkaa wa Mawe kama fuel ya kuendesha generators - wanatumia makapi ya miwa (bagasse) kama fuel, hivyo uzalishaji umeme sio wa gharama kubwa kivile. Suala LA kodi ni kiasi cha kuelewana na Serikali jinsi ya kurekebisha kiwango cha kodi - binafsi sijawahi kusikia kiwanda hats kimoja cha uzalishaji sukari nchini kikifungwa kutokana na kutozwa kodi kubwa - sija wahi?
 
Protectionism kwa gharama ya wananchi walio kuamini uwaongoze na kwa faida ya nani? Hii ni wananchi victimization sijui ndio tuite victimism.

Kuna wakati Museveni akitangaza sukari Uganda iko ya kumwaga viwanda vyao vimezalisha ziada. Wafanyabiashara wangeruhusiwa ili mradi wanatimiza vigezo na mashariti kuzingatiwa na kuingiza kwa masemi trela wakaileta na pengine bei ingeshuka. Lakini aah wapi mamilioni ya watumiaji sukari wanaumizwa ili kulinda kiwanda chenye wafanya pengine 2000 na tajiri wake. Viwanda venyewe havitosheleze soko na kufanya bei ya bidhaa kuwa juu.
Mkuu, kwa nini iwe "kwa gharama ya wananchi"? Hao miwa yao inayozea shambani bila kutumiwa kuzalisha sukari siyo wananchi?

Hiyo "gharama kwa wananchi" unayoizungumzia ni gharama ipi hasa, kama viwanda vyetu vinazalisha sukari ya kutosheleza soko la ndani kuliko kuvizia ruhusa ya kuagiza sukari nje ya nchi?

Nashindwa kabisa kuelewa mantiki ya hoja yako.

Museveni hazalishi sukari ambayo viwanda vyake vina ziada. Viwanda vinaagiza sukari nje ya nchi na kuifungasha ionekane imezalishwa Uganda. Ndiyo maana Kenya wameghairi kununua sukari yake, au hujui?

Ungeeleza sababu za viwanda vyetu kutozalisha sukari ya kutosha, pengine andiko lako lingekuwa na maana zaidi kuliko hili la kushangilia tu tununue nje kitu ambacho inawezekana kabisa kukizalisha hapa hapa nyumbani.
Zambia wao wanafanyaje hadi wawe na uwezo wa kuzalisha sukari ya ziada kuuza nje. Kwa nini sisi tukose uwezo walionao Malawi au e-Swatini, hadi itulazimu kuwa tunaagiza sukari nje. Haya ndiyo mambo muhimu ya kuongelea, siyo hilo la kulilia hiyo ya nje ije imwagwe hapa!
 
Inafaidisha matajiri wenye viwanda
"Matajiri wenye viwanda", ndio hao hao wanaofaidika na vibali vya kuingiza sukari toka nje kama hujui.
Viwanda vinaacha kuzalisha sukari, badala yake wanaagiza nje sukari na kuwauzia wananchi.

Hawa hawataki kuzalisha sukari ya kutosha hapahapa ndani ya viwanda vyao, wanapenda zaidi hiyo ya kuagizwa toka nje.
Kwa hiyo 'protectionism' haiwasaidii wao.
 
Huyu si Prof? Ngoja nione.
Huyu kuna mtu ameniaminisha ni kichwa kizuri, lkn kwa hili ngoja nisubiri kama bei hatapanda
 
Mkuu, kwa nini iwe "kwa gharama ya wananchi"? Hao miwa yao inayozea shambani bila kutumiwa kuzalisha sukari siyo wananchi?

Hiyo "gharama kwa wananchi" unayoizungumzia ni gharama ipi hasa, kama viwanda vyetu vinazalisha sukari ya kutosheleza soko la ndani kuliko kuvizia ruhusa ya kuagiza sukari nje ya nchi?

Nashindwa kabisa kuelewa mantiki ya hoja yako.

Museveni hazalishi sukari ambayo viwanda vyake vina ziada. Viwanda vinaagiza sukari nje ya nchi na kuifungasha ionekane imezalishwa Uganda. Ndiyo maana Kenya wameghairi kununua sukari yake, au hujui?

Ungeeleza sababu za viwanda vyetu kutozalisha sukari ya kutosha, pengine andiko lako lingekuwa na maana zaidi kuliko hili la kushangilia tu tununue nje kitu ambacho inawezekana kabisa kukizalisha hapa hapa nyumbani.
Zambia wao wanafanyaje hadi wawe na uwezo wa kuzalisha sukari ya ziada kuuza nje. Kwa nini sisi tukose uwezo walionao Malawi au e-Swatini, hadi itulazimu kuwa tunaagiza sukari nje. Haya ndiyo mambo muhimu ya kuongelea, siyo hilo la kulilia hiyo ya nje ije imwagwe hapa!

Kwa nini sukari iagizwe na wenye mashamba na hivyo viwanda vya sukari tu? Ili watumie vifungashio vyao kutuzuga ni sukari waliyo zalisha wao hapa nchini?! Na fikiri hili ni kosa la kugushi ambalo Prof Waziri anatakiwa ajiuzulu kulinda heshima yake.

Biashara ya sukari kwa nini ihitaji vibali kwa watu flani flani tu. Vibali vya nini kwenye soko huria huu si mchezo tu wakuwanufaisha wafanyabiashara wachache na washirika wao wa kificho huko waliko? Njia bora ni sukari iagizwe na mfanyabiashara yeyote anayetaka kuifanya hii biashara, kutoka popote ili mradia anatimiza masharti ya serikali likiwemo la ubora wa kumlinda mlaji. Sudecco ife kifo cha mende.
 
Dangote ndiye mwekezaji pekee mwenye uwezo mkubwa wa kujenga kiwanda kikubwa cha kuzalisha Sukari nchini lakini mambo yalivyo hivi sasa atapigwa vita na mamafia wabobezi wa kuagiza sukari kutoka nje - waagizaji hawa wa sukari wana mizizi na ushawishi mkubwa kwenye mission critical sectors nchini na hawajiwahi kushindwa kitu wakidhamilia na nawahakikishieni its a question of time kabla hawajapewa kibali kwa mara nyingine tena cha ku-import substandard na rebagged (huko Dubai) expired commodity/Sugar kutoka Brazil na India, pretending to import industrial sugar wanapewa rebate na Serikali halafu sukari inaiingizwa sokoni kama kawa kwa kukwepa kodi stahiki kwa kisingizio cha Industrial Sugar - wanahujumu viwanda vyetu visikuwe.

Big importers wa sukari wana generate matrillion of Tsh big time bila ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya Sukari - namkubusha Profesa kwamba kundi hili si lelemama litakujengea hoja nzito discretely halafu ujikute aidha anahamishiwa Wizara nyingine au anarudishwa kufundisha Chuo Kikuu. Kwa nini Profesa hajiulizi iweje hawa wafanya biashara wanakuwa na ujasiri wa kushikiza Bodi ya Sukari iwapatie vibali vya kuimport sukari, jeuri hii ya kukihuka maagizo ya the late Dr.Magufuli kupiga marufuku utoaji wa vibali - jeuri hii wafanya biashara hao wanaipata wapi? Binafsi naona kuna kitu wanajiamini si Bure. Mzalendo Prof.Mkenda weka uzalendo mbele historia ndiyo itakuhukumu huo ndio ushauri wangu - barikiwa sana.
Uchambuzi mzuri sana kaka. Nimekuelewa vizuri ila nakumbusha tuu hata anko Magu hili suala la sukari alipigwa ngumi za uso fasta sana akakaa chini bei ikapaa zaidi. Hadi anaingia kaburini sijawahi msikia popote anasema su su su sukari.
Sera yetu juu ya sukari ni mbovu sana na kibaya zaidi serikali ndo mbovu kuliko neno ubovu lilivyo. Unaweza kuta Libya hawana shamba la miwa hata la hatua mbili ila sukari kwao bei nzuri tuu kuliko tanzagiza.
 
Kwa nini sukari iagizwe na wenye mashamba na hivyo viwanda vya sukari tu? Ili watumie vifungashio vyao kutuzuga ni sukari waliyo zalisha wao hapa nchini?! Na fikiri hili ni kosa la kugushi ambalo Prof Waziri anatakiwa ajiuzulu kulinda heshima yake.

Biashara ya sukari kwa nini ihitaji vibali kwa watu flani flani tu. Vibali vya nini kwenye soko huria huu si mchezo tu wakuwanufaisha wafanyabiashara wachache na washirika wao wa kificho huko waliko? Njia bora ni sukari iagizwe na mfanyabiashara yeyote anayetaka kuifanya hii biashara, kutoka popote ili mradia anatimiza masharti ya serikali likiwemo la ubora wa kumlinda mlaji. Sudecco ife kifo cha mende.
Mkuu, naona hatuelewani.

Njia bora ni sisi kuzalisha sukari ya kututosheleza ndani na kuuza ziada nje, kwa sababu uwezo huo upo sana!

Swali muhimu ungeuliza kwa nini hao wenye viwanda hawataki kufanya hivyo?

Unakumbuka tatizo la simenti miaka michache iliyopita? Halina tofauti kubwa sana na hili la sukari. Viwanda vya simenti kwa maksudi mazima walikuwa hawazalishi simenti ya kutosha, na wala walikuwa hawajishughulishi kabisa na upanuzi wa viwanda waweze kuzalisha simenti ya kutosheleza soko la ndani na hata kuuza nje.
Sasa Dangote kawatia akili kichwani. Si unaona Twiga jinsi walivyochangamka?
 
Bakhresa atawafanya watie akili baada ya Azam sugar kuingia sokoni. Hata hivyo serikali haina sababu ya kutoa vibali maalumu na kwa watu baadhi tu kufanya biashara ya sukari. Kama wanaona kuna umuhimu wa kulinda walima miwa na wenye viwanda vya sukari wachukue hatua za kuwapa ruzuku na kuwasamehe kodi sio hii biashara ya vibali vya kibaguzi na inawezekana kwa faida za kificho.
 
Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema yuko tayari kuachia ngazi nafasi ya uwaziri kuliko kutoa kibali kwa wafanyabiashara cha kuagiza sukari kutoka nje ya nchi.

Profesa Mkenda amesema hayo leo Agosti 30 jijini Dodoma wakati akizindua ripoti ya sensa ya kilimo, mifugo na uvuvi ya mwaka wa kilimo 2019/2020.

Amesema kumekuwa na shinikizo toka kwa wafanyabiashara wanaokwenda kuisumbua Bodi ya Sukari kutaka kibali cha kuagiza sukari nje ya nchi.

“Unajua sukari ni kama dawa za kulevya, ina hela nyingi na kila mtu anataka kufanya biashara hiyo. Kuna mwaziri wa kilimo wameondoka kwa sababu ya kutoa vibali vya sukari. Mimi sitoi ng’o,” amesema Profesa Mkenda.

Amesema pamoja na fitina zinazofanywa kutaka kutolewa vibali vya sukari kwake hatotekeleza hilo.
Profesa Mkenda amesema viwanda vya sukari kwa muda mrefu vimeshindwa kupanuka viwanda vyao kuongeza uzalishaji wa sukari kwa sababu ya sukari inayoagizwa kutoka nje.

Amesema Tanzania inaagiza sukari toka Malawi, Uganda na Zambia wakati miwa mingi inazalishwa Tanzania.

Profesa Mkenda amesema kila mwaka katika bonde la Kilombero inatupwa miwa tani 350,000 huku wakulima wa Mtibwa wakiacha kulima miwa kabisa kwa sababu viwanda vya sukari uwezo wake wa uzalishaji ni mdogo na miwa ni mingi.

Amesema Serikali iliamua kupitisha sheria kwamba uagizaji wa sukari utafanywa na wenye viwanda vya sukari nchini wanazalisha kuanzia tani 10,000 na kuendelea.

Profesa Mkenda amesema uagizaji holela wa sukari umesababisha ukosefu wa ajira, ukosefu wa kodi ya Serikali na wakulima kukosa soko la miwa.

MWANANCHI
Yupo sahihi asilimia 200....Bravo Prof. Mkenda. Kwa hili tupo pamoja
 
Mbona yuko sahihi? Kama miwa inatupwa na wengine kuogopa kulima kutokana na ukosefu wa soko ni haki kabisa azuie uagizaji sukari nje ya nchi ili watu wawekeze hapahapa
 
Kuzuia sio suluhisho bali ni kufanya bei ya sukari isiweze kushuka na kumuumiza mlaji. Serikali haitakiwi kudhibiti biashara ya soko la sukari kwa namna hii ya kijinga kabisa.
 
Case study: Kiwanda cha baiskeli aina ya Swala hapa Tanzania...mwekezaji wa kiwanda hicho aliamua kuachana na uzalishaji na badala yake akawa muagizaji wa baiskeli za mitumba na kiwanda kikajifia.... Wenye viwanda vya sukari kupewa vibali kuagiza sukari tunarudi like kule kwenye kiwanda cha baiskeli!
Wasukuma tunapenda baiskeli asikwambie mtu, tunaikumbuka Sana Swala!
Phoenix ilikuwa chuma nayo!
 
Kuzuia sio suluhisho bali ni kufanya bei ya sukari isiweze kushuka na kumuumiza mlaji. Serikali haitakiwi kudhibiti biashara ya soko la sukari kwa namna hii ya kijinga kabisa.
Viwanda vilivyopo nchini vipanuliwe au tule sukari guru mpaka zitukae sawa
 
Bakhresa atawafanya watie akili baada ya Azam sugar kuingia sokoni. Hata hivyo serikali haina sababu ya kutoa vibali maalumu na kwa watu baadhi tu kufanya biashara ya sukari. Kama wanaona kuna umuhimu wa kulinda walima miwa na wenye viwanda vya sukari wachukue hatua za kuwapa ruzuku na kuwasamehe kodi sio hii biashara ya vibali vya kibaguzi na inawezekana kwa faida za kificho.
Ulipoanza kuona wafanya biashara wakubwa wanarundikana bungeni kwa tiketi ya CCM hapo ndipo ungeanza kuwaza hayo unayoandika hapa!
 
"Matajiri wenye viwanda", ndio hao hao wanaofaidika na vibali vya kuingiza sukari toka nje kama hujui.
Viwanda vinaacha kuzalisha sukari, badala yake wanaagiza nje sukari na kuwauzia wananchi.

Hawa hawataki kuzalisha sukari ya kutosha hapahapa ndani ya viwanda vyao, wanapenda zaidi hiyo ya kuagizwa toka nje.
Kwa hiyo 'protectionism' haiwasaidii wao.
Siyo kweli. Wengi tu huagiza sukari Malawi na hawana viwanda.
 
Back
Top Bottom