Waziri wa Elimu hakika umekuwa unajitahidi sana kutendea haki Wizara unayosimamia na kwa hakika hapa mheshimiwa Rais anastahili kupongezwa kwa kukuona kuwa unafaa kuongoza Wizara hii jeti sana kwa taifa kwa ujumla.
Mheshimiwa Waziri tunaomba dawati la wizara linalosimamia ubora wa elimu kutupia jicho swala la shule binafsi za msingi na haswa za bweni kwenye mambo yafuatayo:
1. Darasa la saba kuanza masomo saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tatu usiku.
2. Hawa wanafunzi masomo bado ni watoto wadogo mno na miaka yao ni kati ya miaka 11-13
Tunatambua swala la shule husika kutaka kuhakikisha kuwa wanafunzi husika wanapata alama A kwenye mitihani ya taifa. Hata hivyo, suala la Afya za hawa watoto ni muhimu kuliko kukaririshwa mwaka mzima kwa siku saba za wiki.
Prof toeni mwongozo ili kulinda afya za hawa watoto.Prof je wizara haina mwongozo wa ufundishaji kwa shule za msingi? Ni sahihi mtoto wa miaka kumi na moja kuamka saa kumi usiku ili aweza kuanza masomo saa kumi na mbili hadi saa tatu usiku?