Profesa Mkenda, tunaomba utupatie ufafanuzi

Profesa Mkenda, tunaomba utupatie ufafanuzi

Ratiba za Kijinga walimu wengi nchi hii wanafikiri kukaririsha mtoto muda mrefu ndio kufaulu, na shule nyingi sasa hivi hiziipi kipaumbele extra curricular activities ni mwendo wa masomo tu mtoto akirudi yuko hoi!! Mbona zamani hatukusota hivyo na tulifaulu!

Shule hata viwanja vya michezo haviipi kipaumbele, elimu yetu inahitaji sera thabiti na usimamiwaji wake.
 
Mtoto mdogo anatakiwa kupata muda wa kutosha wa kupumzika na kucheza pia ili aweze kukukua vyema.Hivi kweli mtoto ananza masomo saa kumi na mbili hadi saa tatu usiku anapata wapi muda wa kupumzika na kucheza ?je wewe binafsi ulipokuwa shule ya msingi ulisoma kwa pressure kubwa kiasi hiki?
Yan hujaelew me naomba kuelewa izo athari ambazo anaeza pata mtoto, ndo uniainishie hizo athar kaka nataka na me nizijue
 
Ratiba za Kijinga walimu wengi nchi hii wanafikiri kukaririsha mtoto muda mrefu ndio kufaulu, na shule nyingi sasa hivi hiziipi kipaumbele extra curricular activities ni mwendo wa masomo tu mtoto akirudi yuko hoi!! Mbona zamani hatukusota hivyo na tulifaulu!

Shule hata viwanja vya michezo haviipi kipaumbele, elimu yetu inahitaji sera thabiti na usimamiwaji wake.
Kabisa Dr ,zamani wathibiti ubora wa elimu walikuwa makini ndio maana hatukukarishwa na bado tulifaulu vizuri tu
 
Yan hujaelew me naomba kuelewa izo athari ambazo anaeza pata mtoto, ndo uniainishie hizo athar kaka nataka na me nizijue
Nadhani hutakia kuelewa ,hivi unahitaji degree ili kujua kuwa mtoto anatakiwa acheze na apumzike pia?
 
wasipokuwa moderated hawa wataliangamiza taifa!
Ndio maana tunamwomba Prof aingilie kati ,duniani kote sekata binafsi ni lazima isimamiwe vinginevyo wao wanaangalia faida tu
 
Nadhani hutakia kuelewa ,hivi unahitaji degree ili kujua kuwa mtoto anatakiwa acheze na apumzike pia?
Hao shuleni wanapewa mda wa mapumziko, hata hili kwan linahitaj degree ili ujue kama shule kuna mda wa mapumziko ??
Wewe unakwepa swali langu kwasbb ushagundua umeongea vitu ambavyo huna uthibitisho.
Swali linabaki, ni athari gani watakazopata hao watoto? Tuainishie hapa ili tufaidike kwa sote
 
Unajua kila mtu anapeleka mtoto Private ili apate matokeo mazuri katika mitihani. Walimu wakitumia mbinu za kiwafanya vihiyo wawe vipanga, tunaanza kulalamika. Si umtoe umpeleke shule ya serikali? Hatujui tunataka nini! No sweet without sweat bwashee
mtoto kuwepo drsn kutoka asubuh hadi tatu usiku huko sio kusoma ni kukaririshana.

Elimu haitaki huo upuuzi lazima mwalimu ajue mbinu za kumuelewesha mwanafunzi aelewe kwa wakati na sio kumkaririsha mwanafunzi.
 
Hao wanasoma kwa kupumzika si kuna break time ya kutosh tu
 
Waziri wa Elimu hakika umekuwa unajitahidi sana kutendea haki Wizara unayosimamia na kwa hakika hapa mheshimiwa Rais anastahili kupongezwa kwa kukuona kuwa unafaa kuongoza Wizara hii jeti sana kwa taifa kwa ujumla.
Mheshimiwa Waziri tunaomba dawati la wizara linalosimamia ubora wa elimu kutupia jicho swala la shule binafsi za msingi na haswa za bweni kwenye mambo yafuatayo:
1.Darasa la saba kuanza masomo saa kumi na mbili asubui hadi saa tatu usiku.
2: Hawa wanafunzi masomo bado ni watoto wadogo mno na miaka yao ni kati ya miaka 11-13
Tunatambua swala la shule husika kutaka kuhakikisha kuwa wanafunzi husika wanapata alama A kwenye mitihani ya taifa .Hata hivyo ,swala la Afya za hawa watoto ni muhimu kuliko kukaririshwa mwaka mzima kwa siku saba za wiki.
Prof toeni mwongozo ili kulinda afya za hawa watoto.Prof je wizara haina mwongozo wa ufundishaji kwa shule za msingi?ni sahihi mtoto wa miaka kumi na moja kuamka saa kumi usiku ili aweza kuanza masomo saa kumi na mbili hadi saa tatu usiku?
Mtoto anatakiwa asizidi saa 8 shule aondoke nyumbani akasaidie kazi ndogo ndogo nyumban na ajenge mahusiano na jamii..

Si ajabu tunatumia nguvu kubwa kuwakaririsha watoto kwa sababu hawajui mambo mengi kuhusu jamii zao.

Kwa sababu Kila kitu kwao watoto ni km kitu kipya kabisa.
 
Hao wanasoma kwa kupumzika si kuna break time ya kutosh tu
Haitakiwi mtoto hazidishe saa 8 shuleni si nzuri kwa afya ya akili ya mtoto. Ndani ya hizo saa nane kuwe na vipind vya mapumziko pia angalau viwili.
 
Acha kila mtu atumie mbinu zake kupata ubora.mbona sisi ilokua twalaza miguu m ma basen usik kucha
 
Acha kila mtu atumie mbinu zake kupata ubora.mbona sisi ilokua twalaza miguu m ma basen usik kucha
 
Hivi mkuu,uane mtoto ambae anamshwa saa kumi usiku ili aanze masomo saa kumi na mbili asubui hadi saa tatu usiku kwa siku saba za wiki?unadhani hata akipata alama A kwenye mitahani ya darasa la saba wakati tayari hakuwepewa muda mzuri wa kupumzika na kukua wakati sahihi si ni lazima ataathirika kiafya
Haathirik na kitu.
 
Haitakiwi mtoto hazidishe saa 8 shuleni si nzuri kwa afya ya akili ya mtoto. Ndani ya hizo saa nane kuwe na vipind vya mapumziko pia angalau viwili.
Huko ni uzunguni, hapa Africa na kwa elimu ya tanzania lazima uchoke nd ufaulu vzr, wengi wetu tulisoma kwa style hiyo mwisho wa siku tukafaulu na mpaka sasa tunapumua hatuja ugua hata mafua
 
Elimu imedorora hakun maarifa ,watu wanakaririshwa Review mnaita ni mbinu ,kama Taifa tunaunda bomu litakaloleta madhara makubwa mbeleni
 
Huko ni uzunguni, hapa Africa na kwa elimu ya tanzania lazima uchoke nd ufaulu vzr, wengi wetu tulisoma kwa style hiyo mwisho wa siku tukafaulu na mpaka sasa tunapumua hatuja ugua hata mafua
Wewe ulisoma mika gani labda?
 
Back
Top Bottom