Profesa Mkenda, tunaomba utupatie ufafanuzi

Unajua kila mtu anapeleka mtoto Private ili apate matokeo mazuri katika mitihani. Walimu wakitumia mbinu za kiwafanya vihiyo wawe vipanga, tunaanza kulalamika. Si umtoe umpeleke shule ya serikali? Hatujui tunataka nini! No sweet without sweat bwashee
Kuna mambo ambayo yanaenda kwenye extremes, tusitake kutetea vitu visivyoteteeka, mambo kama haya yanayolalmikiwa hapa.
Tuseme kwa mfano, mtoto wa kindergatten kuonekana kituoni saa 11 asubuhi akiwa anasubiria gari la shule kumchukua aende shule, ni sahihi? Matokea mazuri kila mmoja anayahitaji ndiyo lakini swala la usalama na afya za wototo ni la muhimu kuzidi hayo matokeo mazuri yanayoweza kupatikana kwa njia hii
 
Na kibaya zaidi hizi shule zinajenga mazingara ambayo taka usitake mtoto lazima utampeleka boarding,imagine wanahakisha mtoto awepo darasani saa kumi na mbili asubui na jioni unaambiwa umfuate saa tatu usiku.Jamani huyu mtoto ana miaka kumi na moja tu anapelekeshwa kama vile ameanza kusomea degree ya engineering
 
Kuhusiana na hiyo michango, mnatakiwa mkae chini wazazi na kamati zenu za shule, mwishowe sasa tutamchangaya Waziri. Waziri tumwachie yale tu ambayo sisi hatuyawezi

Mbali na hilo, kama hiyo michango siyo mikubwa sana, funika kombe mwanaharamu apite. Jaribu kufanya ulinganifu kati ya uthamani wa kile unachotafuta mtoto wako apate, na kiasi hicho cha fedha ambacho walimu wanakuhitaji utoe.

Tuacheni kukaa tunawalalamikia walimu, wao pia ni wazazi na hawawezi kupanga kitu ambacho si cha maufaa kwa mzazi, always walimu wanapanga kitu kwa mtoto; kwa ajili ya faida ya mzazi wa mtoto
 
Unajua kila mtu anapeleka mtoto Private ili apate matokeo mazuri katika mitihani. Walimu wakitumia mbinu za kiwafanya vihiyo wawe vipanga, tunaanza kulalamika. Si umtoe umpeleke shule ya serikali? Hatujui tunataka nini! No sweet without sweat bwashee
Mkuu ndio maana kuwa wathibiti ubora kwenye swala nzima la utaoaji elimu na haswa shule za msingi .Duniani kote watoto wanayo mazingira ambayo yatawafanya wakue kwa afaya njema ikiwa ni pamoja na kupata muda wa kupumzika .Hivi kweli wewe ulisoma primary kama mwanafunzi wa chuo kikuuu?
 
Wazazi wengi wa mjini ndio wanapenda hivyo pia! Ni ulimbukeni haswa.
 
Me nafkr ingekua vzr ungetuainishia hapa madhara ambayo wanaweza kuyapata kwa kuamka saa 10 kuanz kusom saa 12 mpk saa3 ili tuelewe athar zake
Una hakika yeye ni Daktari?

Wewe mwenyewe unajua kabisa kuwa mtu akishika kaa la moto ni lazima ataungua; ila to what extent atapata madhara kwenye mwili wake, hilo sasa llinakuwa ni swala la kitaalamu ambalo linamhitaji Daktari.

Huyu yeye anajua kuwa madhara yapo kwa mtoto, isipokuwa extent ya madhara hayo ni swala jingine la kitaalamu ambalo linamhitaji Daktari!
 
wasipokuwa moderated hawa wataliangamiza taifa!
Ni kweli.

Halafu huu ufaulu wa mtoto kupata A kwa sababu ya kutumia muda mwingi sana akiwa anasoma tu; siyo sahihi na hizi shule zinazosababisha watoto kupata A kwa mtindo huu, nafhani ndiyo shule ambazo ni mbovu kuliko shule zote

Kawaida, KATIKA MAZINGIRA YA KAWAIDA, shule nzuri na bora inatakiwa kumsabbisha mtoto apate A kwa kutumia muda wa kusoma ambao ni REGULAR na ambao umepangwa na SERIKALI
 
Kabisa na sio kusomesha vitoto kama vile wanasomea fani ya udaktari wa binadamu
 
Unajua kila mtu anapeleka mtoto Private ili apate matokeo mazuri katika mitihani. Walimu wakitumia mbinu za kiwafanya vihiyo wawe vipanga, tunaanza kulalamika. Si umtoe umpeleke shule ya serikali? Hatujui tunataka nini! No sweet without sweat bwashee
Mtoto huyo huyo anayesoma saa 12 hadi saa 3 ukimpeleka shule za International wanaosoma saa 2 hadi saa 9,, anapwaya [emoji1787]
 
kama mtoto wako yuko katika shule za hivyo mhamishe mpeleke kwa aina ya shule unazotaka za kusoma somo moja kwa siku maana hata huyo waziri si ajabu watoto wake wanasoma shule kama hizo unazolalamikia.
 
Mtoto huyo huyo anayesoma saa 12 hadi saa 3 ukimpeleka shule za International wanaosoma saa 2 hadi saa 9,, anapwaya [emoji1787]
hujui unachosema wewe. Hakuna international school inayofuata mtaala wa elimu ya Tanzania.
sasa unamhamishaje mtoto kwenye mtaala wa tz kisha umpeleke kwa mtaala mwingine utegee atafaulu. Hata huyo wa international ukimleta kwenye mtaala wa tz atafeli sanasana atafaulu kiingereza tu
 
Mtoto huyo huyo anayesoma saa 12 hadi saa 3 ukimpeleka shule za International wanaosoma saa 2 hadi saa 9,, anapwaya [emoji1787]
Sio hiivyo tu hawa watato bado hata zipe shule bora wakifanya entrance exams bado wanafeli
 
Tuonyeshe mahali mtaala wa tanzania unaonyesha kuwa masomo yanatakiwa kuwnza saa kumi na mbili asubui hadi saa tatu usiku?
 
kama mtoto wako yuko katika shule za hivyo mhamishe mpeleke kwa aina ya shule unazotaka za kusoma somo moja kwa siku maana hata huyo waziri si ajabu watoto wake wanasoma shule kama hizo unazolalamikia.
Swala si kuhammisha mtoto ,swala hapa ni swala nzima la uhalisia kwa watoto wadogo kuanza masomo saa kumi na mbili asubui hadi saa tatu usiku.Sisi ni wazalendo haswa ndio maana pamoja na kutokuwa na watoto wanaosoma hizi shule bado kama mtanzania ni lazima kupiga kelele nyingi tu pale ambapo mambo yanaenda sivyo
 
Tuonyeshe mahali mtaala wa tanzania unaonyesha kuwa masomo yanatakiwa kuwnza saa kumi na mbili asubui hadi saa tatu usiku?
nionyeshe wapi mtaala wa necta unafundishwa international school. Na utaje ni international school ipi.
 
Wewe ni mwalimu?
 
Atafeli kiswahili sio otherwise acha kuropoka,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…