Profesa Muhongo huna credibility ya kuwashauri watanzania kuachana na mradi wa JNHPP na usidanganye watu kuwa Hydro power zimepitwa na wakati

Wanasiasa wanafiki kweli kweli.
DC SABAYA LENGAI anaongea🤣🤣🤣
 
Aliyemtusi David Kafulila ni mwanasheria mkuu sio prof Muhongo, pili ni kweli siku hizi nishati mbadala ya uhakika ni 1: Solar 2: Upepo, 3: Nishati ardhi 4: Gesi 5: na Uranium, sio hydropower kwa sababu upatikanaji wa maji umeathiriwa vibaya sana na tabia nchi. Umeona ripoti ya CAG anasema ujenzi wa stieglers gorge wametumia andiko la mradi la mwaka 70/72; hawakupata muda wa kulihuisha, kwa hiyo hakuna uhakika kwamba kutakuwa na maji ya kutosha kulifanya bwawa liwe endelevu na lenye faida na kuzalisha umeme kwa gharama nafuu!
 
Tatizo lako ni mtu wa kukurupuka, unadhani Source ya mto rufiji ilivyo ni wakati wa kufikiria maji kupungua?
NAKAZIA

Stiglers Gorge (Mto rufiji)
  • Inalishwa na maji ya kwenye mito kutoka mikoa minne ambayo ni Pwani, Mbeya, Morigoro na Iringa.
  • Kuna mito mikubwa mitatu inayomwaga maji stiglers ambayo ni Kilombero, Luwegu na Ruaha Mkuu
  • Mto Ruaha Mkuu ni tawi mama la Mto Rufiji(stiglers), Mto huu Umeanzia Mbeya sehemu inaitwa Mbarali na unapita Iringa halafu Dodoma katikati ya bwawa kubwa la mtera halaf unaenda Morogoro unapita katikati ya bwawa kubwa la kidatu halafu unakwenda kuungana na mto kilombero na Luwegu kutengeneza Mto Rufiji(stiglers)
  • Mito inayomwaga maji katika mto Ruaha Mkuu ni Lukosi, Yovi,kitete,sanje,Ruaha mdogo,kisigo,mbarali,kimani,chimala,umrobo,mkoji,kubwa,mlomboji,ipatagwa,mama, na mswiswi(KAMA WAKULIMA WA MCHELE HUKU MBEYA WATAPUNGUZWA MTO HUU UTAKUWA NA MAJI MENGI SANA NA PIA STIGLERS) Inapaswa wakulima waamie kulima chini au downstream yaani baada ya maji kutoka stiglers sio kabla Hayajaingia

  • Mto mwingine mkubwa unaopeleka maji stiglers ni Mto kilombero,limto hili ni likubwa linatokea baada ya kuunganika mito mingi midogo midogo kutoka milima ya udzungwa na mahenge na kupita bonde la ulanga, pia maji ya Mto kihansi yakishazalisha umeme yanamwagwa kilombero. Japo pia huku Kuna walima MCHELE wanaopunguza Flow
  • Mto mwingine mkubwa kabisa unaomwaga maji stiglers ni Mto Luwegu, una maji MENGI SANA,
  • Licha ya hiyo mito mikubwa mitatu pia Kuna mito midogo midogo kutoka mkoa wa Pwani inamwaga maji stiglers.
 
Ishi kumbe jamaa lina ilimu kuu kuu aisee !
 
Wewe ni mpumbavu pia, full stop
 
Mkuu sikatai ila hao Mawaziri vimeo design ya Muhongo ndiyo wanatufanya tusi feel hayo unayosema, naamini hizo changamoto unazotajwa zilichangiwa kwa kiasi kikubwa na wao, ndiyo maana tunalalamika
 
Tangu lini power plants zimepunga matumizi ya nishati? Wanaupunguza matumizi ni watumiaji na wasambazaji (kwa kuongeza efficiency). Labda unamaanisha deficit?

Amandla...
Atuambie kwanini uwepo wa Kinyerezi plants haujapunguza maumizu yetu na yeye alikuwa waziri huko? hatumwamini kwakuwa ana ndimi nyingi sana huyo

Nimemaanisha tulitarajia kufeel punguzo la bei na hata uwepo wa uhakika wa umeme
 
SSH ameshatoa muongozo wakubali ili tu mradi uendelee, haijalishi una faida kwetu au lah...
Tutegemee kupigwa tu hapo.
 
Sasa turudi kwa MUHONGO NA GESI YAKE YA TUMBONI
 
Duniani kote mabwawa yanajengwa. China, Ethiopia, Uganda, Brazil etc. Hawa wanajiita wasomi ndiyo wamefanya hadi leo tupo kwenye umaskini. Si wakusikilizwa.
Tuwasikilize wasio wasomi au sio.
 
Bora uwizi uliofanywa na kina kigwangala pesa zitabaki ndani, hasara ya atcl ni ya ndani. Wakija mabeberu kuchota rasilimali zetu wanapeleka kujenga kwao hata hivyo Vita vya ww2 ilikuwa ni Vita ya kiuchumi Hitler alitaka kuiteka Soviet Union achukue ardhi yenye rutuba na resource za mafuta na gas
 
Nimemaanisha tulitarajia kufeel punguzo la bei na hata uwepo wa uhakika wa umeme
Sio lazima patokee punguzo la bei. Bei inatokana na gharama za uzalishaji, usambazaji na kodi ya serikali. K.m. ingawa wanaotoa huduma za simu na mtandao wameongezeka sana lakini bei haishuki bali inazidi kupanda.

Kuto kuwepo wa uhakika wa umeme ni kwa sababu bado hatujitoshelezi na umeme kwa mwaka mzima, hali ya vyanzo vyetu vya umeme ( mabwawa kujaa matope, turbines kuharibika, mafuta kukosekana kwenye vinu vinavyotumia mafuta n.k.), hali ya mtandao wa usambazaji wa umeme n.k.

Kwa mfano wakulima wa Sumbawanga wanaweza kulima sana mahindi lakini bei isishuke kwa sababu barabara za kuwafikia ni mbovu sana na sehemu nyingine uzalishaji umeshuka kwa sababu ya nzige.

Amandla....
 
Mkuu sikatai ila hao Mawaziri vimeo design ya Muhongo ndiyo wanatufanya tusi feel hayo unayosema, naamini hizo changamoto unazotajwa zilichangiwa kwa kiasi kikubwa na wao, ndiyo maana tunalalamika
Tatzo sio mawaziri ,ni KATIBA na ccm
 
Wizi ni wizi tu. Hasara ya ATCL itaathiri uwezo wa kuhudia ndege zake. Mabeberu watachota rasilimali zenu kama mtaingia nao mikataba mibovu kama ambavyo hata wawekezaji wa kitanzania watakavyozichota ( na kuwekeza nje) kama mikataba nao itakuwa mibovu. Mwizi ni mwizi, hamna tofauti kati ya Beberu na Mmatumbi.

Amandla...
 
Kweli mkuu
 
Ulimsikiloza vizuri? Amesema Kuwepo na energy mix hao US na China wana hydro lakini wana wind turbines, Geothermal, Coal, Gesi, n.k. na ndio alichoshauri.
Mkuu hata hayati JPM hizo zote ulizozitaja za Wind turbines (Umeme utokanao na upepo-Singida, Dodoma na Shinyanga), Geothermal energy (Umeme utokanao na joto la ardhi), Coal (Umeme utokanao na makaa ya mawe-Dangote anatumia kwa sasa) na Gesi (yenye unafuu kwa Tanzania ni ile inayotoka Songas huko Lindi sio ya Msimbati na Mnazi bay (GPF-Gas Processing Facility) ambayo ni ya wawekezaji ambao huiuzia TANESCO inapofikishwa kwenye kituo chao hapo Mtwara mjini (GRF-Gas Receiving Facility) ambao huichakata kwa matumizi ya umeme kwenye viwanda, nyumbani kwa ajili ya gari-magari ya Dangote mengi yanatumia nishati ya mfumo wa gesi kuzalisha umeme wa kuendesha mashine na mitambo pamoja na matumizi ya kupikia nk. (rejea hotuba yake wakati wa ufunguzi wa bunge la 12 lakini hata kwenye ilani ya chama chake hayo yote yameelezwa sio kitu kigeni anachokieleza Muhongo ijapokuwa anajaribu kuonesha umeme wa maji hauna manufaa kitu ambacho sio kweli.
 
Mbona tumeingia uchumi wa Kati bila yeye kuwepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…