Profesa Muhongo huna credibility ya kuwashauri watanzania kuachana na mradi wa JNHPP na usidanganye watu kuwa Hydro power zimepitwa na wakati

Profesa Muhongo huna credibility ya kuwashauri watanzania kuachana na mradi wa JNHPP na usidanganye watu kuwa Hydro power zimepitwa na wakati

Kuna weza kuwa na mafuriko mwaka huu mwakani kukawa ukame kupita maelezo
Uhakika wa umeme wa maji uende sambamba na matunzo ya vyanzo vya maji, iwapo kutakuwa na mkakati wa kutunza vyanzo vya maji nyanda za juu kusini na kuwapunguzia gharama za gas wananchi wa kule ili wapunguze matumizi ya kuni na mkaa, itasaidia sana kuwepo kwa maji ya uhakika Rufiji
 
Kuwekeza kwenye Umeme wa maji ni bahati nasibu.Kila siku tunaongelea mabadiliko ya tabia nchi.Kuna weza kuwa na mafuriko mwaka huu mwakani kukawa ukame kupita maelezo.Umeme wa uhakika ni gas ,makaa ya mawe ,nguvu ya nyuklia!
You are right na gesi Tanzania tunayo nyingi...50% ya Tanzania ina gesi
 
Mleta mada unachanganya concepts za “renewable” na “sustainable”. Umeme wa maji ni salama kwa mazingira kwa maana hauna carbon footfrint lakini sio sustainable kwa kuwa maji yanapungua kadiri muda unavoenda (global warming). Mradi ule umeleta uharibifu mkubwa wa mazingira na kwa kuwa mazingira ni chanzo cha maji - huenda mradi mzima ukaja kuwa ni hasara kubwa sana.

Tulipaswa kujikita kwenye gesi! Prof. Muhongo yuko sahihi.
Maji yatakapopungua sababu ya mazingira wala hatutahofu kukosa umeme..., sababu matumizi ya maji / uhai yatakuwa yemeshatuondoa kabla ya hio Nishati...

Point labda angesema Hii Rufiji specifically ina madhara ya kimazingira na sio kupitwa na wakati.., ingawa hata extraction ya gesi pia sio environmental friendly be it natural au petrolium...

HEP ni renewable inatumia natural cycle ya maji kutengeneza umeme (hakuna conversion / mabadiliko yoyote ya hayo maji) ni ile force ya maji kuzungusha turbines Force = Height x Density x Gravitational Force..., (cha maana hapo ni variable ya height / kimo) peleka maji juu zaidi unaongeza force..., kwahio kama kuna sehemu yenye natural flow yenye kina cha kutosha (automatically HEP is the way to go) Na badala ya kuogopa kukosa maji yakikauka tutakosa umeme tungepanic kwanza kukosa maji ya kutumia as we all know maji ni uhai
 
Gas alishauziwa mchina tuna chini ya asilimia 40 kwenye gas yetu anachotaka huyu mpuuzi ni tuingie mikataba na wachina watuuzie gas YETU naona ashaitwa pembeni na macho kengeza ...GAS TULISHALIWA KICHWA KITAAAMBO
Gas haijauzwa kwa mchina, wala mchina hajawekeza kwenye gas Tanzania wala hana kampuni lolote la gas Tanzania
 
Hahahah nyie wote hamjui Tanzania mpaka sasa umeme tunaotumia yaani National grid asilimia 50 (50%) ni gesi asilia iliyobakia ndo uweke maji,upepo na vingine...na Kinyerezi 1 na 2 zikizimwa tunarudi kwenye giza kama ilivyokuwa before 2004,mimi naongea kama mtaalamu wa mafuta na gesi,quote me!
Tuliahidiwa Kinyerezi zitashusha gharama ya umeme nchini, tuliambiwa umeme hautakatikakatika, tujibu kuanzia hapa
 
Nimeisikiliza hotuba yote ya Muhongo leo. Hakuna popote aliposhauri kuwa mradi wa bwawa la umeme la Nyerere haufai au uachwe. Na watu wengi humu wamerukia kumlaumu hata bila kujua alichosema. Amesema kuwa umeme wa maji kwa ujumla wake hautabiriki kwa sababu ya kutegemea mvua na kuathiriwa na shughuli zingine za binadamu. Kinachotakiwa ni kuendeleza vyanzo vyote vya umeme, ikiwemo gasi asilia ambayo inaonekana kutelekezwa. Rudi ukamsikilize tena.
Mkuu kuna watu wana kipaji cha kukurupuka, huwezi kuwa na akili mgando kushindwa kufanya diversification ya vyanzo vya nishati ukae ukitegemea bwawa la maji ambalo linaathiriwa muda wowote na changamoto za kimazingira, haya mambo ndo yamefanya maendeleo ya miradi inayotumia gesi kusuasua ikiwemo gesi ya kwenye magari, nchi nzima sehemu ya kujaza gesi kwenye magari ni moja tu! gesi ya kutumia kupikia majumbani nayo inasuasua, tunaagiza arabuni wakati tunayo deposit ya gesi kubwa sana, huu ni upumbavu ambao aliwaaminisha mwendazake na nyinyi kumeza kama mazuzu...
 
Tuliahidiwa kinyerezi zitashusha gharama ya umeme nchini, tuliambiwa umeme hautakatikakatika, tujibu kuanzia hapa
Tanzania tuna gesi nyingi mpaka sasa inazalishwa mpaka inakosa matumizi, umeme kukatika ni miundombinu mibovu na ya zamani inachangia matengenezo kila kukicha. Bei ya umeme kwa sasa ipo chini ukifananisha na miaka ya zamani.

Watu wanalipa tsh 9,300 kwa unit 78+,ukiona umeme kwako upo juu basi matumizi yenu ni makubwa pia sawa na viwandani
 
Kwa hiyo wewe profesa ulietetea wizi wa fedha za Escrow kwa nguvu nyingi mpaka ukatukana watu ni matumbili leo hii unapata wapi ujasiri wa kutuambia watanzania kuwa umeme maji unachelewa kuanza kuzaa faida na umepitwa na wakati?

Kwa hiyo huko Usa na China ambazo ni nchi zilizoendelea kwa kila namna wanapojenga Hydropower stations au kuendelea kutumia HEP kuzalisha umeme ni watu wasio na uelewa wa mambo?

Lini ilishawahi kutokea kupata nishati kama umeme ikawa ni fasheni ya kudai HEP imepitwa na wakati na sasa tutumie gas? Au unaleta dharau zako?

Hasira za wewe kufukuzwa uwaziri kisa tu ulishazoea kupiga madili makuwa hapo wizara ya nishati isiwe sababu ya kutuharibia mipango ya kukamilisha JNHPP. Kaaa kimya uendelee kutafuna posho za Escrow.
Profesa Ngwale alikuwa anatumia 'foolish professor' for full professor. JPM alikuwa very genius kwa kumfanya Prof Muhongo miongoni mwa watu wa kutumbuliwa mapema. Huyu Muhongo hajajisumbua hata kujua kuws ktk uwekezaji lazima kuingia gharama na hasara kabla ya kuanza kuvuna faida.

Vv
 
Electricity in Tanzania is generated using gas; hydropower is also a significant source of power.Tanzania has a capacity of 1,601.84 megawatts (MW) as of April 2020, Natural Gas contributes 892.72MW, Hydroelectric Power contributes 573.70MW, while heavy oil and biomass make up of 88.80MW and 10.50MW, respectively. Quoted!
Will the move from Gas dependent to HEP lower costs to end user?
 
Prof. Hili la kukebehi ujenzi wa mradi wa umeme wa Maji umetudanganya.

Umeme wa Maji bado ni tegemezi duniani, unaposhauri weka mbali maslahi yako.

Upo Tanzania mwanzo wa huu mradi mpaka sasa ulikua wapi kusema haya mwanzo wa mchakato.
 
Kwa hiyo wewe profesa ulietetea wizi wa fedha za Escrow kwa nguvu nyingi mpaka ukatukana watu ni matumbili leo hii unapata wapi ujasiri wa kutuambia watanzania kuwa umeme maji unachelewa kuanza kuzaa faida na umepitwa na wakati?

Kwa hiyo huko Usa na China ambazo ni nchi zilizoendelea kwa kila namna wanapojenga Hydropower stations au kuendelea kutumia HEP kuzalisha umeme ni watu wasio na uelewa wa mambo?

Lini ilishawahi kutokea kupata nishati kama umeme ikawa ni fasheni ya kudai HEP imepitwa na wakati na sasa tutumie gas? Au unaleta dharau zako?

Hasira za wewe kufukuzwa uwaziri kisa tu ulishazoea kupiga madili makuwa hapo wizara ya nishati isiwe sababu ya kutuharibia mipango ya kukamilisha JNHPP. Kaaa kimya uendelee kutafuna posho za Escrow.
Wabunge wengi na watumishi waandsmizi kwenye sera,ni watu wakuchumia tumbo,anaongea hivyo kumbe amenunuliwa kapewa wimbo aimbe
 
Mnamjadili mtu ambae nimesha attend lecture zake mwaka mzima

Mzee huyo ni smart sana kichwan..na ni mwalimu mzur sana na amebobea kwenye hiko anachoongea

Ni mmoja ya watu walioandaa geological map ya Tanzania miaka hyo

Enewei...alichoongea ni sawa kabisa.

Tatzo ni moja tu.Tanzania haijawa tayar kwa mirad hyo ya gas ili kuweza faida kama nchi.watafaidika wachache sana na ni hao walioko huko juu

Sabab miundombinu ya energy kwa gas inahusisha mambo meng.mikataba mikubwa mikubwa miing kias kwamba kupigwa ni rahis sana na ndomana magu aliachana nayo

Ila ku manage HEP ni rahis na tayar tuna experience nayo tofaut ma gas.....

Gas kupigwa ni rahis sana..na ndo chanzo cha kuletewa alshabab...wazungu wale ukiona wanachimba gas au mafuta lazima wahakikishe wanakuletea kakikund cha kigaidi katakacho kutoa kwenye reli huku wenyew wakichkua mali..

We are not ready for that....bora hyo HEP tuna uzoefu nayo
 
Gas alishauziwa mchina tuna chini ya asilimia 40 kwenye gas yetu anachotaka huyu mpuuzi ni tuingie mikataba na wachina watuuzie gas YETU naona ashaitwa pembeni na macho kengeza ...GAS TULISHALIWA KICHWA KITAAAMBO
Yaani nyie watu mlikuwa mnafanywa kama mazuzu! Bandari ya Bagamoyo mliambiwa maneno sawa na hayo; na leo hii hao hao waliokuwa wanawalisha ujinga ndio wamewageuka ni kuwaeleza umuhimu wa Bandari ya Bagamoyo!
 
Leo nimeshituka kusikia maneno ya Professor Muongo (Mtaalamu wa Nishati) akisema umeme wa Maji sasa Umepitwa na wakati na Uchumi ni Umeme wa Gesi.

Huenda ni kweli ujenzi wa Hydro Electric Power Plant ukawa na gharama mwanzoni na sio kila nchi / sehemu inaweza ikawa na HEP sababu lazima kuwe na viable infrastructure.

Ila ni ukweli usiopingika kwamba umeme wa maji ni renewable (yaani unaweza ukazalishwa tena na tena na tena) Gesi unless otherwise ni Biogas basi uchimbaji wa gesi sio renewable... Nisiwachoshe kuna hii article hapa chini kuhusu gharama ya renewables na umeme wa maji bado ni cheaper... as of 2017 nadhani hii 2021 hali haijabadilika sana

Mitaro ya kwenu ulishakagua kwenye mifereji, ukimaliza kupata comment
 
Kwa CV yake tu huyu Profesa, Uweledi wake, Uzoefu wake na Uwezo wake mkubwa wa Akili nakubaliana nae tena kwa 100% juu ya huu Mtazamo wake.

Ni Rais Mpumbavu tu pekee ndiyo hatotaka kufanya Kazi na Mtu very competent kama Profesa Muhongo ambaye hata Mataifa Makubwa na yaliyotuzidi kila Kitu hadi Akili walifanya nae Kazi na sasa wanamtumia pia kama Independent Consultant katika Masuala ya Madini na Jiolojia pia.

Majungu dhidi yake hayasaidii ni Upuuzi.
Google tu gapo uone umeme wa gas na mafuta mwisho wake ni lini huku duniani siyo Tanzania...Nadhani yeye ndiyo kapitwa na wakati tena anatisha...Watu wanaondoka kwenye magari ya mafita walete ya mvuke na betri yeye anawaza hizo dirty energy sources? Tena bila aibu hadharani mchana kweupe! Kweli nimeamini elimu haitusaidii
 
Will the move from Gas dependent to HEP lower costs to end user ?
Consumer costs depends on many factors all in all TANESCO has to be monitored and regulated with close eyes to lower those costs.Government intervention in cost lowering by putting standards openly like in Petrol,diesel will contribute a lot.

It is the same as telecommunication company like halotel using fibres and airtel using signal poles they charges same consumer costs also HEP and Gas all should deliver cheap and affordable charges.
 
Back
Top Bottom