Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi

Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi

Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka

CCM acheni unafiki
ahahahaha hadi nimemkumbuka Msigwa kule twitter aliposema kweli Magu ni shujaa ila ni shujaa wa kizamani asiyeweza kwenda kasi na dunia ya sasa ya teckinolojia
 
mnapopoa kila alichokifanya magu!

marehemu atabakiwa na nini!?

ahahaha
 
Dooh nimecheka saana haya watu wanafufuka mmoja moja wanaaanza upya kuchomoa makucha yao.
Hawana tena cha kuhofia mana enzi za shamba la bibi zinarudi kila mtu anaanzisha ubunifu mpya wa kupiga pesa.

Huyu ni Muhongo bado namsubiri Ngereja naye atakuja na lipi.

Na muda si mwingi tutasikia Accacia nayo imefufuliwa upya na kupewa mgodi huko geita kwasababu nchi inahitaji zaidi wawekezaji kuliko wao wanavyo tuhitaji.
ahahaha hawataki kusubiri hata40 ya mzee,nakuambia huu ni mwanzo tutaona mengi amakweli ccm imekufa
 
Mm binafisi siitaki tena ccm baada tu ya magufuli kufariki wameanza kumgeuka wamesahau kabisa kabla ya 2015 walikua wakipita mjini na manguo yao kijani walikua wana zomewa wengine wana diriki kusema rais ali shauriwa vibaya, inaoneka walikua wana jali matumbo yao tu wa tz tuamukeni.
 
Kwa ripoti hii ya CAG, haikuwa hata shamba la bibi bali halikuwa la mtu kabisa!!
Hahaha sawa wenye akili nyingi wa nchi hii, haya futeni huo mradi kisha leteni umeme wa gas na upepo na jua ili Tanzania ipae tuendane na kasi ya dunia.
Futeni tu miradi yote mana ni ya kifisadi tu mkuu.

Dooh masikini nchi yangu mimi, nisamehe sana Dambisa Muoyo kumbe ulikuwa sahihi.
 
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi

Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati.

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti.

Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma

Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya Maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.

"Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.

Amesema dunia ya sasa imegeuka na madini mengi yanayotarajiwa Tanzania yapo lakini wengine wameelekeza kwenye dhahabu, Tanzanite na madini mengine ya zamani lakini wanaacha kuangalia madini mapya ambayo yataliingizia Taifa fedha nyingi.

NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi

Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka

CCM acheni unafiki
Profesa afanye utafiti zaidi kuhakiki ufahamu wake, umeme wa maji ni moja ya njia zinazopigiwa debe sasa duniani ikiwa ni katika sera za kutunza mazingira na kutupunguza emission of cabonidioxide gas kutokana kutumia fossils fuels ikiwemo natural gas..

Umeme wa gas inachangia kwa kiasi kikubwa katika janga la global warming.
 
Kusema ukweli Ni kwamba umeme unaozalishwa kwa kutumia maji huko kwa wenzetu wanaokimbia na muda hawana imani nao.

Ni bahati mbaya Sana sisi kwa kupitia viongozi wetu wakisiasa walituaminisha kua tu hu ndio mradi utakao tuvusha kumbe Ni vionjo vyao tu.
 
Tundu Lissu, Muhongo, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea .
Umma upi unaoongelea? Huu wa Tanzania uliochoka kwa ahadi hewa za CCM huku viongozi wakifaidi uchumi wa kati peke yao?
 
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi

Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati.

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti.

Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma

Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya Maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.

"Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.

Amesema dunia ya sasa imegeuka na madini mengi yanayotarajiwa Tanzania yapo lakini wengine wameelekeza kwenye dhahabu, Tanzanite na madini mengine ya zamani lakini wanaacha kuangalia madini mapya ambayo yataliingizia Taifa fedha nyingi.

NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi

Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka

CCM acheni unafiki
Prof. Mhongo umeibukia wapi? Jpm akiwa hai ulikuwa wapi na hili wazo lako?
 
Tundu Lissu, Muhongo, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea .
Kwahiyo mwendazake alitumia mshahara wake kufanya hayo?

Huyo mwendazake alitufanya watanzania wajinga.
 
Umeme wa maji ndiyo nishaji yenye gharama nafuu duniani. Ukisikia mtu anajiita profesa anauponda cha kutilia shaka ni vyeti vyake tu.

Kwa hesabu ndogo tu Megawati 2,100 ni sawa na kilowati 2,100,000 Unit za umeme ni kilowati moja ikitembea kwa saa moja.

Sasa ukiwa na kilowatt milioni mbili na laki moja zikatembeza mitambo kwa masaa 24 unapata unit za umeme milioni 50.4. Ukiuza umeme huu kwa wateja angalau kwa unit moja shilingi 100

Mtambo unaweza kutoa mapato ya bilioni 5 kwa siku. Ukitoa mwezi mmoja kwa mwaka kwa ajili ya "maintenance" ukatembea miezi 11 unaweza kupata trilioni 1.7 kwa mwaka Tumeujenga kwa shilingi trilioni 7. Almost 5 years mradi kama utakuwa full operational unarudisha gharama.

Kama taifa lazima tujue wataalamu wetu ndiyo wamekuwa wakitupotosha na tatizo ni elimu yetu ndiyo mbovu.

Ukichukua mtu aliyesoma miaka ya 70, nchi haina wataalamu huku kwenye elimu ya chini, wanasema nyumba ni msingi hivyo ukikosa basic education huko juu mtu anaenda tu. So unaweza kuta mtu ni profesa but anafanya maamuzi au ushauri wa ajabu.

Labda tujenge mradi but mashine tusifunge megawati zote 2100 kwa kuwa kwa sasa hatuna soko la kutosha.

Kadiri tunavyoongeza ndivyo tutakavyoongeza kufunga mashine.

Umeme wa maji unategemea jiografia hivyo wengi hawatumii kwa kuwa jiografia haziwaruhusu.

Chukua mfano mdogo tu wa gari, Gharama ya kuendesha gari kwa kunua mafuta ndiyo gharama ya juu kuliko gharama ya kununua gari lenyewe.

Mmfano umenunua gari la milioni 12 kama ukiweka mafuta ya 20,000 kwa siku ndani ya mwaka utaweka mafuta ya 7,300,000 (milioni saba na laki tatu)

Ukikaa nalo miaka 10 utatumia mafuta ya milioni 73.

Lakini sasa anakuja mtu ana gari anauza milioni 16 lakini unaedesha kwa kutumia maji.

Ndani ya miaka 10 la mafuta kununua na mafuta ya uendeshaji ni milioni 85 wakati la maji ni milioni 16.73

Hivi ndivyo umeme wa maji ulivyo nafuu kulinganisha na umeme wa mafuta au diezeli.

Mashine zinazungushwa na maji hahuhitaji kununua nishati ya kuendesha.
 
Sasa hii ndio serikali ya uwazi na uwajibikaji sio ile ya kidikteta na uporaji wa mali za umma huku wakitukemea wenye nchi
 
giphy.gif

Wabunge wa Viti Maalum wanaanza kuongea
 
Back
Top Bottom