Profesa Mussa Juma Assad agombee urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Profesa Mussa Juma Assad agombee urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

CHEF

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2013
Posts
222
Reaction score
122
Profesa Mussa Assad ni mtu sahihi kuwa Rais wa Jamhuri Ya muungano wa Tanzania, kwa weledi aliouonesha ni kweli Tanzania tuna wasomi na watu makini sana na wasiogopa mtu, Kauli ya Baba wa Taifa ya kwamba tunahitaji vijana jeuri basi huyu ni miongoni mwa zao la baba wa taifa.

Ukimtathimini huyu Profesa Mussa Assad kuwa Rais ama hakika kodi za wananchi zitatumika vizuri sana, katiba nzuri ya kuwajibishana wenyewe yaani wananchi kumuwajibisha kiongozi itapatikana, nafikiri tutafurahia si ndio jamani,

Nimekaa, nikamtafakari huyu mzee na weledi wake, nikaamua kuandika huu uzi.

Kazi nikuanza kumshawishi huyu mzee ili ajiandae kuchukua fomu ya Urais au wapinzani wata "take advantage" ? maana huyu mzee ni CCM pure.

Nawaza tu,
 
Ameshashindwa hata kabla hajagombea ,ameshindwa kuficha siri za ofisi ndogo ya CAG akipewa ikulu si nchi itabaki uchi

State agent
Hamna siri aliotoa...yeye ni mwana taaluma sio mwanasiasa.. kumhusisha na siasa ni utoto....
 
Profesa amesema anaenda kufuga Kuku kwanza

maana hamkawii kumwingiza chaka LA kugombea kama yule Jaji Mchungaji na mwishowe kutoswa kirejareja
 
Usimtakie matatizo mzee wa watu. Watamuuua bure
 
Aiseee!!
"ufafanuzi murua"!!!!????
Kila mtanzania mwenye vigezo vya kuwa Rais anafaa kuwa rais Wa
JMT ila katika wote wenye vigezo ni mmoja tu atachaguliwa kuwa Raid. Nadhani nimeeleweka kwa ufafanuzi huo murua
 
Ameshashindwa hata kabla hajagombea ,ameshindwa kuficha siri za ofisi ndogo ya CAG akipewa ikulu si nchi itabaki uchi

State agent
Nani kakudanganya kuwa kuna siri katika anayo yagundua CAG katika ofisi yake na kutolea taarifa?
 
Hata mimi ninafaa kuwa rais wa nchi kwa kuwa ninajua kusoma na kuandika kwa mjibu wa katiba yetu, tatizo nafasi iko moja na anaetakiwa ni mtu mmoja na hatuwezi tukawa rais wote ila tunaweza tukawa rahisi wa kutawaliwa.
 
Kila mtanzania mwenye vigezo vya kuwa Rais anafaa kuwa rais Wa
JMT ila katika wote wenye vigezo ni mmoja tu atachaguliwa kuwa Raid. Nadhani nimeeleweka kwa ufafanuzi huo murua
Uko sahihi kabisa mkuu. Kasoro tuu ni kwa mwaka 2015 ugomvi wa wanasiasa na migongano iliyoambatana na wizi wa kura(to be specific uporaji) ulisababisha mtu aliye beep akasukumiziwa ilihali hakujiandaa kisaikolojia na kimipango.
 
Ameshashindwa hata kabla hajagombea ,ameshindwa kuficha siri za ofisi ndogo ya CAG akipewa ikulu si nchi itabaki uchi

State agent
siri gani mkuu ameshindwa kuficha? mapato na matumizi ya kodi sio siri mkuu
 
Back
Top Bottom