Profesa Ndalichako aagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwachukulia hatua viongozi wa serikali ya wanafunzi

Mungu awasaidie wapate haki yao, japo maandamano si mazuri
 
Mkuu zama zimebadilika.
Enzi zile hata wanafunzi wa sekondari wanagoma na kuchoma moto shule kirahi rahisi tu.
Kitu ambacho kwa primitive society kama yetu ni sifa kumbe ujinga mkubwa mno.

Zama hizi jaribu kupimana ubavu na dola utajuta kusoma chuo cha umma na kudai upewe mkopo kama unadai mdeni wako.
Serikali itumie busara waongee na wanafunzi ikibidi ikakope hata kwenye mabenki ya kibiashara watoto wasome.
 
Wanaocomment kuponda hao, vijana either hawajafika chuo kikuu kujua umuhimu wa hilo bòom kwa wanafunzi,...hivi mwanafunzi 2months hajapewa pesa kwa maisha ya hapa jijini ataishi vipi,unategemea huyu kijana atasoma?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
17 Dec 2019
Waziri Ndalichako amesema kwa kuzingatia uhitaji wa wanafunzi waliojiunga na masomo kwa mwaka 2019/2020 pamoja na kwamba katika bajeti lengo ilikuwa kutoa mkopo kwa wanafunzi elfu 45, lakini hadi kufikia Desemba serikali ilikuwa imetoa mkopo kwa wanafunzi elfu 49, 485 ambao wamepata mkopo wenye thamani ya shilingi bilioni 172 na milioni 400. - Pia Waziri Profesa Ndalichako, ametoa saa 24 kwa chuo kikuu cha Dar es Salaam kuhakikisha kuwa kinachukua hatua kwa wanafunzi waliotoa tamko ambalo limekiuka taratibu na kutoa taarifa ni hatua gani zimechukuliwa.
Source:

N.B
Hii serikali tajiri inashindwa vipi kuwalipa wanafunzi stahiki zao, waache vitisho wajibu hoja za msingi za wanafunzi lini watalipwa.

Huku kila mtazania na wanafunzi wanajua ndege Bombadier ilinunuliwa kwa cash na kukombolewa huko Canada kwa kishika uchumba inakuwa vipi serikali ishindwe hela hii ndogo ya wanafunzi?!
 
Usiwajaze ujinga wanafunzi wakafukuzwa chuo halafu uje hapa uanze oohh "enzi zetu tukifukuzwa chuo tunaenda kulima mahindi".

Use the internet wisely. Usichochee watu ukawaponza!

Halafu tangu lini mtu akashindana na serikali na akashinda?

Wanaweza kulitatua hili kwa njia za amani tu! Ninaamini walishapewa majibu kuhusu madai yao lakini wakakaza vichwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Only in Tanzania serikali ikainvest mamilioni kwenye ndege halafu isi invest kwenye elimu ya wananchi wake... pathetic!
Wana kamsemo kao cha ujanja ujanja cha "vigezo vya mkopo".

Wanafunzi wote tu wangepatiwa mikopo bila hivi viwango vya kitapeli vilivyowekwa ambavyo wakati mwingine havina uhalisia kabisa!

Ndio shida ya serikali zetu hizi. Elimu inaonekana kama luxury.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…