Profesa Ndalichako aagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwachukulia hatua viongozi wa serikali ya wanafunzi

Profesa Ndalichako aagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwachukulia hatua viongozi wa serikali ya wanafunzi

Wewe andamana ndo utajua ikiwa baba yako huwa anakukata kodi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi si mwanafunzi.
Nilivyosoma sikutumia hata senti moja kutoka kwa serikali bali ilitoka mfukoni mwa wazazi wangu. Wanafunzi wanachodai ni stahiki yao! Hata kama njia waliyotumia ni mbovu lakini si kujibu kama alivyojibu Ndalichako!
 
Hivi tatizo huwaga ni nini jamani?
Hawa madogo wangeambiwa mchakamchaka wa HESLB wala wasingekomaa hivyo
Hawa madogo wanalilia moto, ila huo moto wanaununua kwa bei ghali isivyo kawaida
Waachane na maswala ya kuwafukuza hao watoto wataelewa tu wakikua
 
Kukopa ni harusi,sasa hivi wanalilia kupewa mikopo lakini washaanza kukatwa midomo juu, Waziri yuko sahihi,serikali inajua matatizo yao, huwezi kumuamuru baba yako mzazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Ile ni kauli ya kihaini sana unaipa serkal muda na kusema ikishindwa mtaitia adabu ningekuwa Rais Magufuli ningetimua wote

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameuagiza uongozi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam kuwachukulia hatua viongozi wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho DARUSO ambao wametoa tamko kwa serikali kwa kuipa masaa 72 iwe imetoa mikopo kwa wanafunzi waliokosa mikopo.View attachment 1295284

Sent using Jamii Forums mobile app
Malekela anawapoteza DARUSU tunaomjua ndani na nje hatukuruhusu awe hata time keeper secondary ni aibu UDSM kumpa Uwaziri wa mikopo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameuagiza uongozi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam kuwachukulia hatua viongozi wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho DARUSO ambao wametoa tamko kwa serikali kwa kuipa masaa 72 iwe imetoa mikopo kwa wanafunzi waliokosa mikopo.View attachment 1295284

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali kandamizi imezoea kusifiwa tu.
 
Waziri Ndalichako inaonekana kapotoka pakubwa anawatisha wadogo zetu wanaodai haki zao za kupewa mikopo.

Yeye anajua kabisa tatizo lipo kwa Serikali kushindwa kutoa mikopo sasa najiuliza kauli aliyoitoa leo akiwa Kigoma sio ya kiungwana hata kidogo anasema vijana watulie wasome sasa swali watasoma vipi wakati hawana pesa?

Serikali inakwepa majukumu yake kwanza yeye alisoma bure kipndi hicho.

Wadogo zetu hawawezi kusoma bila pesa kama mmeshindwa kuwapa pesa waambieni ukweli warudi nyumbani pesa zinazonunua ndege zinapatikana wapi ambapo pesa ya kuwapa wadogo zetu hakuna?
 
Back
Top Bottom