Profesa Ndalichako aagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwachukulia hatua viongozi wa serikali ya wanafunzi

Profesa Ndalichako aagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwachukulia hatua viongozi wa serikali ya wanafunzi

lengo boss, Serikali ijipange kuwasaidia. Wengi wetu, wao serikalini wamesomeshwa bure. Tuaangalie Bajeti inasemaje na kuwaaambia ukweli.
 
Uongozi Ni hekima na busara maisha ya chuo Ni magumu hatuna elimu bure ya migomo cc tusifanye Mambo kwa kupaniki fedha Kama ipo wapewe na Kama haipo wambiwe wasije wakaanza kujiuza bure

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi huwa nahisi huenda ndio maana asilimia kubwa tukiwakuta kazini, huwa wananyodo sana kwakuwa wanajua msoto. Simaanishi wote wanaoringa huwa wanalipa kisasi, wengine huwa ni uoimbukeni tu wa maisha.
 
Chapa kabisa msaidiwe pesa zichelewe mzidai kama zenu

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, hata pesa ya mkopo ni yako kwakuwa kuna siku utatakiwa kuirejesha. Binafsi siungi mkono maandamano lakini nawaza, mbona serikali ikitaka kuwakata hizo pesa huwa zoezi linaanza punde tu mtu apatapo kazi?
 
ndayilagije, Hao wanaowapampu wanaujua moto na walipoambiwa hajaribiwi walielewa anamaanisha nini, sasa wameenda kufanya lobbying kwa wavulana wa chuo na wameuingia mkenge maskini, wasamehe mama, walisahau Rais Magufuli hajaribiwi. Fungeni mikanda vijana, kama ulitegemea boom ushawishi ka'1st year chuo utakisahau.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamuonea bure fikiria kwa utulivu utajua tatizo liko wapi?? Kuhusu mitaala ya Elimu ubadilishaji wake siyo rahisi hivyo mkuu ni mchakato wa miaka kama 20+ fikiria tu kuhusu kuandaa wakufunzi na miondombinu mingine??
Hautaji miaka mingi ukijua umuhimu wake na kwa mustakabari wa Taifa. Kwanini unafanya mchakato mpya kwa ajili ya nani.

Ni kwa ajili ya watoto wetu wote. Wajiamini, wajue historia yao, geography yao, opportunities zilizopo, tangu wakiwa darasa ya kwanza,pili tatu, nne. Futa kabisa historia ya sasa hivi tuanze kabla ya utumwa, ukoloni.

Unawaita wataalamu wote wa ndani, wa Africa, Dunia yote. Unasikiliza maoni yao unafanya uamuzi. Kusaidia vizazi vyetu vijao.

Watoto wa Ulaya hata sasa hawajui hao watu wapumbavu tunaofundishwa kwenye historia yetu.

Wanafundishwa heshima kwa kila mtu, kujitegemea, uhumuhimu wa elimu, kusafiri, afya, kazi, biashara, kilimo, chakula.

Linganisha na elimu yetu.
 
Zamani wakati tunasoma enzi hizo, tulijua kuwatuliza mawaziri kama huyo. Nakumbuka wakati ule alikuwa ni William Shija. Aliupata fresh. Siku hizi vitoto vyetu vikitikiswa kidg tu badala ya kupambana na serikali wao wanakimbia kupambana na wazazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na wewe ni tatizo kubwa. kama unaunga mkono udhalimu, basi wewe ni sehemu ya tatizo la vitoto vyetu
 
Hili la riba kwenye loan board waliangalie vizuri jamani limekaa vibaya,
Kuna watu hawana kazi na kwahiyo hawana uwezo wa kuanza kulipa deni lakini cha ajabu deni linapaa kila kila siku
Kuna mtu namjua deni limefika milioni 10 na linaendelea kuongezeka.
Mtu mwenyewe ni yatima.

Wabunge fanyieni kazi hii hoja tafadhali hali ni mbaya ya riba ya madeni,

Zamani ilikuwa mtu anaanza kulipia mara baada ya kupata ajira na hakukuwa na riba hizo za kibiashara kubwa kiasi hicho jamani!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wazazi wanafunga mkanda ili watoto wakose mikopo ya elimu ya juu ni vema wakafungua hiyo mikanda tu.
 
Arts ni wengi sana na vyuo vimekuwa vingi tofauti na miaka yetu ilikuwa UDSM na Mzumbe tu, saizi vyuo mpaka vichochoroni serikali inajipa mzigo,ingefanya review......japo linafanyika kisiasa sana ndiyo maana linawapa shida
Kwani KUKOPESHANA ni Lazima?
Serkali inajipa mzigo wa kijinga tu. Isomeshe wanaohitajika hata kwa gharama wengine wajisomeshe wenyewe, halafu unalazimisha huku unaita MKOPO . Anayekukopesha kasema hakupi, ndio maana kuna allication za % kama vipi wengine wapewe % wakiwa kwenye hayo maandamano.
Hizo hela wangepewa ili wajiajiri

Hii grease niliyojipaka uje na POVU jingi, ili unisafishe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemsikia Ndalichako akiongea jana, Sikuamini kama ni yeye!
 
Sasa watoto wana njaa wanapanga kuandamana mnawatishia.aisee hii nchi hii. Wapeni basi hiyo mikopo
 
Ukwaju, Sasa watakula nini huko chuoni kama hawajapewa hela ya kujikimu.au wafunge hicho chuo mpaka hela zitakapopatikana.
 
Mkuu usilazimishe kisa ulitembea pekupeku wakati unasoma na watoto wako watembee ivyoivyo,kila jambo na wakati wake acha mawazo mgando na ya kishamba,yaani unacomment kabisa hapa kwa kujiamini "eti mbona sisi tulisoma bila smartphone na laptop?
Mkuu umesoma mpaka level gani na mwaka gani?

Watu wa karibu yako hasa wadogo zako nawaonea huruma sana
vile ni vitendeankazi vya lazima kwa sasa, jamaa inaonekana hajui maana ya kulala na njaa. Ndalichako watoto wetu wanasiasa wapate hela ya kula, watoto nendeni mkazifunge hizo barabara magari yatawasaidia kufikisha ujumbe Halafu hii serikali ni wangapi sana vitisho vya kishamba wanasahau kuwa hata hao wanaowategemea wana watoto na ndugu
 
Nawaunga mkono vijana wa UDSM kwa kudai haki zao bila kupepesa macho. Hiyo ndiyo jadi yetu tuliopita hapo, hata huku makazini ndo tunaoongoza harakati za kudai haki. Hiki chuo kina historia yake ktk harakati, kina Walter Rodney walikuja hapo kufanya kazi sababu chuo kilikuwa sehem harakati za ukombozi kusini mwa Afrika. Thank you for keeping that hope alive.

Prof. Ndalichako asitake kufunika uzembe wa watendaji wake kwa vitisho. Kama uongozi wa chuo ndo umezembea kupeleka taarifa HESLB basi uwajibishwe. Kama tatizo ni HESLB nao wawajibike.

Tusiwabeze hawa vijana, leo kwao kesho kwako. Ugumu wa maisha ukiwafanya waanze wizi na ukahaba chuoni, jamii nzima itaathirika.
 
Back
Top Bottom