Profesa Ndalichako aagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwachukulia hatua viongozi wa serikali ya wanafunzi

Profesa Ndalichako aagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwachukulia hatua viongozi wa serikali ya wanafunzi

Alikuwa lecturer pale udsm,mama ukweli anaujua mateso wanayopata wanafunzi,sikutarajia hiyo kauli yake kwakweli
wanafunzi wanasoma political science, kuandamana si ni moja ya masomo kwa vitendo? watoto wakitaka kwenda practical unasema watakiona halafu wakihitimu wakiwa watupu munawaita vilaza, hivi kweli mtu yuko udsm hawezi tofautisha kuandamana na kufanya vurugu? kwani ulisikia watabeba mawe?
 
Tatizo hawa wanafunzi walifeli
Sana, unatoaje tamko kama hilo
La amri, kuamrisha serikali
Ifanye wanavyoyataka kwenye
Uongozi huu?

Bora ata mngeandaman kimya
Kimya kuliko kutuna misuli kwa
John cena..

Nawaambia mkiandamana mtapigwa na hayo masomo
Mtaachishwa na pengine hizo
Hela hamtapewa so kipi ni
Bora?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pooleni sana
Kwenye kampeni nakumbuka alisema hili la mikopo litaisha kumbe ndo linaanza.

Mi nawashauri msirudi nyuma komaeni mpaka kieleweke maana baada ya kumaliza hilo deni litawaumiza sana na mtajuta kwanini mlikopa.
 
Wanafunzi wamesema wataandamana kwenda bodi ya mkopo kujua sintofahamu ya wanafunzi kukosa mikopo na sio kufanya vurugu. Hilo la kufanya vurugu ni kiherehere chake sidhan kama daruso wamesema watakwenda kufanya vurugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania hatuna uzalendo kabisa na hao wanaoambiw haya Ndio wanyonge wa kweli lakn sis hatuoni haki yao . Hawa adi wanaamua Kutaka kugoma maana yake jitiada zingne washafnya zimeshndkna
 
[QUOTE="Luqman mohamedy,
Hii Wizara ya Elimu, Waziri wake angepewa Mh Joseph Musukuma, Mbunge wa Geita vijijini, angeweza na Tanzania ingesonga mbele kuliko alivyopewa huyu mama anayejiita Prof. na uProf wake Haina faida kwa Watanzania tena Watanzania wanyonge.
 
technically,
Huwa nashangaa kwamba elimu ya msingi na secondary ni bure kwamba wazazi hawajiweiz sasa huyo huyo mzazi atajwezaje kimsomesha mtoto chuo kikuu ambacho ni gharama zaidi .
 
Habari wana JF

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na msemakweli ni mpenzi wa Mungu, Dr. John Pombe Magufuli imekuwa ikijinasibu kuwa na pesa nyingi kutokana makusanyo makubwa ya kodi.

Ushahidi wa hili ni miradi mikubwa iliyoanzishwa na kuendeshwa na serikali, mfano ni ununuzi wa madege kwa pesa taslimu, ujenzi wa SGR, umeme wa Stiglers Gorge, flyovers, daraja Busisi nk.

Kama vyote hivi vinafanyika kwa uwezo wetu, nini kimetokea mpaka wanafunzi wa elimu ya juu wakose mikopo yao?

Waziri Prof. Ndalichako kunukuliwa ukijimwambafai kumiliki kiberiti kilichojaa na uko tayari kukitumia ili kuwadhibiti wanafunzi wasidai haki yao ni fedheha kwako wewe na serikali unayoitumikia!

Picha mnayotupa sisi wananchi huku ni kuwa Serikali yetu imejaa ulaghai, haina pesa imefilisika! Serikali tajiri haiwezi kutishia kiberiti wanafunzi!

Serikali wapeni wanafunzi mikopo yao ili mlinde heshima yenu mnayotuaminisha!
 
Mh. Ndalichako, mkopo wa Elimu si lazima ni ahadi, na ahadi si shuruti inahitaji uvumilivu na mawasiliano, vijana wetu wanalishwa kichaa cha elimu mbovu na baadhi ya watu wasioitakia mema Nchi, wanahitaji elimu ya mzazi kwa mtoto, wewe ni Mama, watoto wanakosea sana lakini tunalazimika kuwafundisha kwa upendo wakinyea viganja hatuvikati.

Uamuzi wowote utakaochukua au chuo kuchukua kutawaathiri si watoto tu bali wazazi wao pia, chonde Mama usipaniki wasikilize waelimishe na pale penye uwezo wa kuwasaidia fanya hivyo. Sijui kama unafahamu kwamba kwakukosa mikopo watoto wetu wanalala na njaa wengine wemewekwa kinyumba wanafanyishwa mambo yasiyopasa, Taifa lijalo litakuwa na raia wenye makovu mengi mioyoni. Mama "
 
ruaharuaha,
Tafuta thread inahusu mitaala IPO huku utanielewa vizurii..Kama tungekuwa serious mpaka sasa tungekuwa tumetuma vijana wetu mataifa makubwa kuiba technical ata za kutengeneza betri za simu na mambo mbalimbali ni kazi ya usalama wa taifa kama tungekuwa tunajielewa..kuna Nchi azina ata madini lakin Wana vyuo Bora vya madini sisi wenye kila kitu Tunafanya siasa..
 
USSR,
Hivyo ni vyuo vya wale wenye ufaulu wa kati na wa chini, usifananishe udsm na mambo ya kijinga pale ni home of intellectuals. Angalau wameweza kupaza sauti zao lakini hakuna chuo chengine chochote kinachoweza kutetea haki zao walau kwa kutoa tamko.
 
1576651740553.png

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameuagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kuwachukulia hatua viongozi wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO), waliotoa tamko la kuipa serikali saa 72, kulipa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, vinginevyo wataandamana.

Juzi Daruso walitoa saa 72 kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kuhakikisha inatoa mikopo kwa wanafunzi waliokosa, vinginevyo watakutana nje ya ofisi za bodi hiyo zilizopo Mwenge jijini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma jana, Profesa Ndalichako alisema tamko hilo limetolewa kinyume cha utaratibu wa kutoa malalamiko na utovu wa nidhamu wa kiwango cha juu, ambacho hakiwezi kuvumilika, hivyo ametoa saa 24 kwa UDSM, kuwachukulia hatua na apewe taarifa hatua iliyochukuliwa.

Alisema kwa mujibu wa taratibu, uongozi wa Daruso unapaswa kuwasiliana na Mshauri wa Wanafunzi, ambaye anachukua malalamiko yao na kuyapeleka kwa Makamu Mkuu wa chuo.

Lakini, taratibu hizo zote hazijafuatwa na uongozi wa chuo hicho kikongwe nchini haujui chochote kuhusu madai na malalamiko hayo. Aidha, alisema wanafunzi 45,000 wa mwaka wa kwanza, walipaswa kupewa mikopo, lakini serikali imeongeza idadi na kufikia 49,485, na Sh bilioni 172 zimetolewa kwa ajili yao na wameshapata mikopo wote waliokidhi vigezo.

Alisema jumla ya wanafunzi 128,697 wa elimu ya juu, wanatarajia kunufaika na mikopo mwaka huu, ambayo kiasi cha Sh bilioni 447 zimepangwa kwa mikopo, na hadi sasa Sh bilioni 202 sawa na asilimia 45 zimeshapelekwa HESLB.

Katika madai ya wanafunzi hao, alisema zipo taratibu za uhakiki wa vigezo na nyaraka wanazopaswa kuwasilisha wanafunzi na hivyo bodi ilikuwa inapitia vigezo na kujiridhisha, ikiwamo uwepo wa wanafunzi yatima, walemavu na uwepo wa wanafunzi waliokata rufaa, ambao taarifa zao zinafanyiwa kazi ili wakikidhi vigezo wapatiwe mikopo.

“Wakati taratibu za uhakiki zinaendelea, wanafunzi wamekuja na tamko ambalo ni utovu wa nidhamu mkubwa tena wanaipa serikali masaa 72 watekeleze madai yao vinginevyo wataandamana, nasema hivi masaa 72 ni mengi waanze maandamano leo, wanatingisha kiberiti, lakini nawaambia kiberiti kimejaa,” alisema Profesa Ndalichako.

Alisema amezungumza na Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo, lakini hajapata malalamiko yoyote rasmi, zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari, hivyo tamko hilo ambalo halikufuata taratibu ni batili na utovu wa nidhamu.

“Wanafunzi wasiotaka kusoma, waondoke na kuwaacha wanaotaka kusoma, kwa sababu tamko hili kama lina jambo lingine zaidi ya masomo, tamko hili linalenga kuleta vurugu na kuvuruga masomo, tutalishughulikia kikamilifu,” alisema waziri huyo wa Elimu.

Wakati waziri akitoa uamuzi huo, HESLB imesema hadi sasa jumla ya wanafunzi 49,485 wa mwaka wa kwanza, wameshapata mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 169.4 na kuvuka lengo la kutoa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 45,000.

Imesema kati yao, wanafunzi yatima waliopoteza mzazi au wazazi wote wawili ni 10,383, wenye ulemavu 397, waliofadhiliwa masomo ya sekondari 3,128 na wengine wahitaji 35,577.

Aidha, wanafunzi 78,337 wanaoendelea na masomo, wamepata mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 272.1. Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema pamoja na malipo hayo, kwa sasa bodi hiyo inakamilisha malipo ya fedha za wanafunzi waliobadilisha kozi, ambayo imepokelewa na HESLB kutoka Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) mwishoni mwa wiki na fedha hizo zitawafikia wanafunzi ifikapo kesho.

Alikuwa akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya Menejimenti ya HESLB, Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na wawakilishi wa viongozi wa wanafunzi wa chuo hicho juzi jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Makamu Wakuu wa UDSM, Profesa Killian Bernadetha (Utafiti), Profesa David Mfinanga (Utawala), wawakilishi wa serikali ya wanafunzi na watendaji wengine wa UDSM na HESLB.

“Kuna kundi la wanafunzi waliobadilisha kozi wakiwa vyuoni na taarifa hizo zilikuwa hazijatufikia, tumezipokea mwishoni mwa wiki na tu

nakamilisha malipo ambayo yatawafikia siku mbili zijazo,” alisema Badru.

Alieleza kuwa kundi lingine linahusu malipo ya vitabu na viandikwa, ambapo malipo ya awamu ya kwanza ya jumla ya Sh bilioni 13.3 yameshafanyika na awamu ya pili ya Sh bilioni 1.1 itawafikia wanafunzi ifikapo Jumamosi ijayo, Desemba 21, mwaka huu, kwa kuwa wataalamu wanakamilisha uchambuzi.

Profesa Anangisye alisema wanafunzi wote wa taasisi za elimu ya juu wanapokutana na changamoto, wasisite kuziwasilisha kwa menejimenti za vyuo ambavyo vitaziwasilisha HESLB au kwa taasisi sahihi.

“Hata nyie (Daruso) mlipaswa kuanzia kwetu na tungeyafanyia yote kazi badala ya kutoa maelekezo ya saa 72,” alisema Profesa Anangisye na kulieleza gazeti hili jana saa 12:04 jioni kwamba walikuwa kikaoni kushughulikia haraka agizo hilo la waziri wa Elimu.

Chanzo: Habari Leo
 
Back
Top Bottom