Profesa Nonga: Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport

Profesa Nonga: Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport

View attachment 2466447
Vifaranga vilivyozuiliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 22, 2022, ni mali ya Kampuni ya Phoenix Farms Limited iliyopo Mkuranga mkoani Pwani.
Vifaranga hivyo vilivyofungwa kwenye maboksi 697 yenye thamani ya Sh200.262 milioni, vilikamatwa wakati wa ukaguzi walipokuwa wakiingizwa nchini kutoka Ubelgiji.

Mwananchi imebaini kuwa Kampuni ya Phoenix Farms Limited iliwasilisha barua ya maombi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuomba kibali cha kuagiza vifaranga kutoka nchi hiyo ya Ulaya.
Pia, imethibitishwa kuwa waagizaji walikuwa wamepewa cheti cha mifugo na mamlaka ya Ubelgiji.
Baadhi ya wadau katika sekta hiyo wameishutumu wizara hiyo kwa kushindwa kutoa leseni za uagizaji bidhaa kutoka nje na kuchukua hatua za ziada kuwalinda wawekezaji wa ndani.
“Mamlaka zimeshughulikia suala hilo kwa njia isiyo ya haki. Walitakiwa kutoa kibali hicho kwa kuzingatia kwamba nchi haina uwezo wa kuzalisha kuku wa kukidhi mahitaji yake,” alisema mdau kwa sharti la kutotajwa jina.
“Vifaranga hivyo vingeweza kupelekwa kwenye shamba la kampuni hiyo na kuwekwa karantini humo. Vingegundulika kuwa na afya njema mwekezaji angeweza kuadhibiwa na vifaranga virudi kwake,” kiliongeza chanzo hicho.
Alipotafutwa, Ofisa Mkuu wa Phoenix Farms Limited, Irfan Mitha alikataa kutoa maoni yake kuhusu uhalali wa hati mbili zilizotajwa hapo juu.
“Niko busy leo; nipigie simu kesho, nitakuwa kwenye nafasi ya kutoa maoni yangu,” aliliambia gazeti hili.
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS) katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Hezron Nonga alisema ombi la kibali cha kuagiza cha Desemba Mosi, 2022, halijafika ofisini kwake wala wizarani.

“Tuliona barua ya maombi ya vibali kutoka nje ya nchi, muda mfupi baada ya vifaranga kukamatwa JNIA. Kadhalika, cheti cha mifugo kilichoandikwa na Shirikisho la Ubelgiji la Usalama wa Mnyororo wa Chakula (FACFAS),” alisema Profesa Nonga.
Akitoa taarifa ya vifaranga hivyo, Profesa Nonga alisema vyote 62,730 vimekufa baada ya kutelekezwa kwenye uwanja wa ndege.
“Mwagizaji ana kesi nyingine ya kujibu mbele ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwa mipango ya uteketezaji wa kuku inaendelea,” alisema.
Makaratasi yanasababisha hasara kwa viumbe hai,Roho mbaya haijengi.
 
Nchi hii ina wapuuzi wengi sana,ndio maana Proffesa Asad alisema watumishi wengi na viongozi serikalini wana uwezo mdogo sana

Ndio maana hatuendelei, maana wenye uwezo na akili wengi wakipata nafasi wanakimbilia nje,kuanzia wawekezaji, wanasiasa na wasomi,tunabaki na wapumbavu watupu

Wanaofaa kuwa maraisi wazuri na wabunge wamekimbia nchi,wafanyabiashara wakubwa wanawekeza nje,wasomi nao wakipata shavu nje hawarudi.
Umesema kweli Sana!
 
Kesi za namna hii huwa ngumu kwa kuzisikiliza upande mmoja tu. Je baada ya kuomba kibali Wizarani alipata majibu gani? Kama hakupata jibu lolote, hana wa kumlaumu.
Hii ndio cancer ya nchi yetu, inachukua within 7days kwa Botswana 🇧🇼 kupata permit ya uwekezaji, inachukua within 30days kwa Botswana kupata au kupewa majibu ya maombi ya permit ya ukaaji, hayo yote ni ndoto kwetu hapa, issue ya vifaranga hivi ilishakuwemo humu almost 7days ago sio issue ngeni, hapo kuna urasimu mkubwa, watu wana vibali vya kuingiza cheap chicken meat kutoka Brazil nchini, mwekezaji huyu wa ndani inaonekana ni tishio kwao, kama kawaida tutalalama humu na itaisha kama lile la moto kariakoo ,ajali ya ndege ziwani
 
Haya mambo yasikie kwa jirani tu, yakikukuta utaona kama dunia imekuelemea mkuu. Unapoomba kibali cha shughuli yako ni kama umewaambia una hela za kugawa. Swali, tutalia hivi mpaka lini????????
 
Kuna kipindi flani nilikua nafatilia nipate leseni ya ku-export cowries, nilikua nakutana na watu wa ajabu sana huko serikalini. Nilicho gundua ni kwamba huko wamejazana watu wenye uwezo mdogo sana kiakili hivyo hata utendaji wao lazima uakisi uwezo wao wa kiakili. Ili upate kazi huko lazima uwe mjinga mjinja mwenzao
 
Kesi za namna hii huwa ngumu kwa kuzisikiliza upande mmoja tu. Je baada ya kuomba kibali Wizarani alipata majibu gani? Kama hakupata jibu lolote, hana wa kumlaumu.
Unachekesha. Kwa hiyo kwa kutokujibiwa ndio anakosa mtu wa kumlaumu? Au kinyume chake?
 
Back
Top Bottom