Profesa Nonga: Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport

Profesa Nonga: Vifaranga 62,730 kutoka Ubelgiji vilivyokamatwa JNIA vyote vimefia Airport

Mamlaka za kibongo zina ukiritimba sana!!??
so vifaranga vimekufa kwa njaa!!?
Hakuna ukiritimba, ni ujinga na wizi na kujidai misheni tauni kwa biashara za TZ. Unawezaje kutafuta kibali baada ya vifaranga kufika nchini? Huko Ubelgiji hata ukitua na embe mkononi ingawa hawalimi maembe, litatupwa!!

Huyo mtu anatakiwa kupigwa kibano!! Ni mshenzi tu!
 
Ni Lini Huyu mama ataongea na kundi la wafanyabiashara live Ili awasikilize? Au anaonaga aibu kuongea mbele Za watu?
Tusipo jitokeza kwa mwingi 2025 kupiga Kura kumuondoa imekula kwetu maxima.
 
Acha ujinga,hivi vitasisi vya Serikali kuna baadhi ya Watendaji ni wapumbavu sana TRADE BARRIERS hasa Wizara ya Kilimo.
Sasahivi mnamlaumu tasisi sio Rais, kipindi cha Magufuli vifaranga 2000 kutoka Kenya,vilipochomwa kelele zote zilielekezwa kwa Magufuli sio tasisi, kweli Tanganyika kuna watu wanafiki.
 
Prof umekula per Diem kiasi gani ziara ya kutembelea vifaranga?
 
Team walamba asali wamekaa kimya , kipindi cha magu kuchomwa wale vifaranga sidhani ata kama buku wanafika waliimba kila nyimbo za kumkashifu jpm ,hili la vifaranga zaidi ya elfu sitini imewabidi walamba asali wafunike makalio yao na kuacha mbupu zinaning'ia kwa aibu.
Yaani Wewe wacha Mungu hawaumbue, wakati wa Magufuli vifaranga 2000 tu kelele zote zilielekezwa kwa Magufuli sio tasisi au mamlaka,leo usikii Samia akitajwa.
 
Kwan wangeviweka quarantine kwenye shamba la muagizaji na kumchapa fine zingine zingine ingekuwaje?
 
Ivi Magu alichoma vingapi, na situliambiwa haikuwa sawa kuchoma??

Ooh, Ok. Kumbe hivi vimekufa vyenyewe let me shutdown ma trumpet.
 
Kosa la maafisa wa airport nini? Mlitaka waruhusu vifaranga viingie bila vibali? Yani mijitu inatanguliza vifaranga bila hata vibali,,alafu muje muwalaumu maafisa
Nakubaliana na wewe mkuu, tena Kuna harufu ya rushwa hebu somatena hapa chini, inamaana baada ya kukamatwa ndio wakaanza kufanya process first first ilikuweka mabo sawa.

[emoji116][emoji116]

Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS) katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Hezron Nonga alisema ombi la kibali cha kuagiza cha Desemba Mosi, 2022, halijafika ofisini kwake wala wizarani.

“Tuliona barua ya maombi ya vibali kutoka nje ya nchi, muda mfupi baada ya vifaranga kukamatwa JNIA. Kadhalika, cheti cha mifugo kilichoandikwa na Shirikisho la Ubelgiji la Usalama wa Mnyororo wa Chakula (FACFAS),” alisema Profesa Nonga.
 
Ni ujinga mtupu unaofanywa na watumishi wa Serikali. Mpaka siku Serikali itakapoamua kila sehemu kuajiri the best best, ndiyo matatizo kama haya yataisha.

Kuna watemdaji wa Serikali ambao ni wajinga kupindukia. Wanadhani Serikali kazi yake ni kuumiza wananchi. Wanashindwa kuelewa kuwa Serikali inatakiwa kuwa mwezeshaji.

Hao maofisa wa Serikali walitakiwa kujiuliza wafanye nini ili muingizaji vifaranga asiingie hasara lakini pia nchi iwe salama.

Wangeweza kuruhusu vifaranga kuingia wakapelrkwa shambani kwake kwa ysimamizi maalum. Na huko wawekwe karantini, na walindwe kwa gharama ya mwingizaji. Wapimwe kwa gharama ya mwingizaji. Wakionekana hawana tatizo, aendelee na ufugaji, lakini apigwe faini.

Lakini kwa upande mwingine ilitakiwa kuangalia kama aliomba kibali cha kuingiza, aliomba lini, kwa nini watoa vibali hawakutoa vibali. Na kama walishindwa kutoa vibali kwa sababu ya uzembe au kutengeneza mazingira ya rushwa, basi hao maofisa wa wizara ya kilimo, wafukuzwe kazi na kupoteza stahiki zao zote.
Shida ipo hapo kwa watoa vibali hapo ndipo tatizo lilipo,sababu muwekezaji hawezi kupata ujasiri kuingiza vifaranga bila kibali wakati Anajua kabisa kunasheria inazuiya.

Kunamtu amemdanganya sio bure.
Otherwise wanadhani lawama zilizo tolewa vilipochomwa vifaranga vya Kenya na kauli ya madam kulaani ingempa nafuu baada ya kukamatwa na mzigo wa aina hiyohiyo.

"Sheria ziki heshimiwa ndio mwanzo wa uwajibikaji, that's all.
 
ndicho cha kushangaza na vingepita vikaja leta madhara ungesikia tena maofisa wa hovyo waondolewe.Tararatibu zipo wazi na siyo Tanzania tu na nje ya Tanzania huwezi ingiza bidhaa za nyama bila vibali hata kama ni nyama choma.Tumeshasikia sana mafua ya ndege sasa mlitaka mtu ajiletee tu vifaranga bila pewa kibali?
Mpumbavu tu ndio atawalaumu maafisa wa airport.
 
Aliyevizuia naye afe kifo kama vya hao vifaranga!
 
Sasahivi mnamlaumu tasisi sio Rais, kipindi cha Magufuli vifaranga 2000 kutoka Kenya,vilipochomwa kelele zote zilielekezwa kwa Magufuli sio tasisi, kweli Tanganyika kuna watu wanafiki.
Taasisi ikivuruga inalaumiwa na ikifanya vizuri inapongezwa,kiongozi akivuruga ni mwendo wa kila mtu kumlaumu na akifanya vizuri atapongezwa tu.
 
VIFARANGA ARE SO DELICATE, WANGEWAHISHWA KWANZA SHAMBANI MENGINE YAKAFUATA, WAKO WATU KAMA HAWANA UBONGO VILE.
Huna akili,
Huko shambani kuna waTanzania wenzako, Ulitaka wafe kwa magonjwa ya ndege?.

Acheni sheria zilinde uhai wa wananchi.
 
Sheria ziko wazi jamani ,ukiangiza wanyama kutoka nje lazima uwe na import permit na inalipiwa ,kwahyo ukishaipata Kule unakovitoa watakupa export permit and the viceversa is true

Sasa unaagizaje vifanga bila kibali chochote? Nini kimekupa jeuri ya kufanya hivyo ? Hii vita ni kubwa na inahitaji watu wenye msimamo kama profesa nonga ( veterinary doctor huyu) maana hapo angeweza chukua rushwa hata ya millioni 30 au 50 lakin kasimama kwenye sheria ,huwa wanasema ni bora kufuata utaratibu ili uwe na ujasiri wa kusimama na kukemea . watu jamii ya kina profesa nonga ni muhimu sana kwenye hili taifa ni bora kufa maskini kwa kutenda haki

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Well said indeed,

Angekuwa amefuata utaratibu angeweza hata kufungua kesi ya madai.
 
Back
Top Bottom