Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 9,504
- 20,293
Najua Waafrica wengi tumekuwa tukiamini sababu ya sisi kutokuendelea imesababishwa na wazungu
nimeona chapisho mtandaoni kuhusu maadhimisho ya kitabu cha How Europe underdeveloped Africa by Walter Rodney, hii ni nadharia ya bwana Rodney
Moja kati ya maelezo aliyoyatoa Prof Shivji ni kuhusu kuuawa kwa Ghadafi na kusema kuwa hao wazungu walimuua Ghadhaffi kwa sababu alikuwa na mpango wa kuwezesha Africa kuwa na sarafu moja, ndio nataka tujadili hili
Kwa watu wenye uelewa wa uchumi na fedha (economics and finance) ni kuwa huwezi kuwa na sarafu moja kama hampo economically intergrated, yaani namaanisha uchumi wenu haujachangamana sana, haujaingiliana sana, kuingiliana kwa uchumi ni pale mnapofanya biashara na kuuziana bidhaa nyingi kwa pamoja
Mfano tungeukuwa tuna import bidhaa karibu zote tunazozitumia hapa hapa Africa na kuuza bidhaa karibu zetu tunazozalisha hapa hapa Africa, uchumi wetu ungekuwa umechangamana sana, na hivi ndivyo nchi za EU zilivyokuwa zimechangamana hadi zikaamua kutumia sarafu ya EURO, na sio zote
Sasa tukija kwetu aFRICA tunauziana bidhaa gani? bidhaa tunazouziana ni bidhaa ndogondogo tu za chakula kama unga, mchele, nyama na tunazuiana majirani tu... Bidhaa za thamni kubwa kama magari, simu, mitambo ya viwandani, mafuta, vifaa vya umeme, ujenzi, nguo n.k tunaagiza kutoka China na Ulaya. Na sisi exports zetu za thamani kama madini, mazao ya misitu, vyakula ghafi n.k tunavipeleka Ulaya
Sasa hapa unaona kabisa economic intergration ni kidogo sana, mfano Tanzania tupo karibu zaidi na China kiuchumi na kibiashara kuliko tulivyo na nchi kama Nigeria,
Sasa tukiwa na sarafu moja itatusaidia nini? italeta tu migogoro sababu kila mtu ana mipango yake tofauti na mwingine, na siasa zetu pia zimekaa mbali sana kuwa na sarafu moja. Tunajaribu kuiga Ulaya ambao uchumi zao zimefanana sana na hata siasa zao zimefanana sana
Nafikiri Maprofesa wetu kama kweli tuna nia ya dhati ya kuendeleza bara letu la Africa tungekuja na hoja zenye ukweli na uhalisia kuliko hizi za kuokoteza