Profesa Shivji: Mkataba wa Bandari unaegamia zaidi upande mmoja na hauna ukomo wa muda. Hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile

Profesa Shivji: Mkataba wa Bandari unaegamia zaidi upande mmoja na hauna ukomo wa muda. Hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile

Najiuliza sana!

Inawezekanaje Profesa Shivji awe mwanasheria na azijue sheria kumzidi mbobezi wetu wa sheria ndugu Zembwela?!

Kwamba mnataka niamini Shivji ni nguli wa sheria kumzidi Maulid Kitenge!

Eti Profesa Shivji ana mzidi kudadavua sheria za mikataba mwana sheria mbobezi wa sheria za mikataba ndugu Msigwa?!

Acheni kuniaminisha ujinga atiii!

NB: Mod, andiko langu ni swali tafadhari msiuunganishe ili niweze kupata majibu.
Dah![emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Shivji haoni ndani kwa Professor Zembwela na Dr. Kitenge hawa ni wabobevu kwenye sheria za mikataba ya kimataifa.View attachment 2672113
haya machawa ya kijinga nayafananisha na sabaya, makonda na mnyeti. awamu tofauti ikiingia yatakosa cha kufanya, watakosa wa kuwachezea na kuwakebehi, yatanyooshwa na kujifungia ndani kwa kukosa cha kufanya. hivi kweli wanafikiri watanzania tu wajinga kiasi cha kutuletea unafiki na kebehi kama wanazoleta, kwenye issue inayohusu maslahi ya taifa? na huko uarabuni walikoenda wakirudi wafanyiwe vipimo kama vya yule afande wa zanzibar
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila JF Haiboi, wala haichoshi.
 
Wale kenge waliokuwa hawasikii mpaka masikio yao yatoke damu naamini sasa watasikia, mjomba wao amesema.Samia ni msaliti.
 
Poteleambali kama wewe huwez tuache ss tuandamane Kwa ajir ya vizazi vijavyo sio vya Sasa maana ss tushajichanganya Tyr
Ungekua na akili ya kufanya mambo kwa ajili ya vizazi vijavyo basi ungeenda kupanda miti hizo hela unazopewa baada ya kupumuliwa choko wewe, iwe mwanzo na mwisho kuni-quote
 
Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD

View attachment 2671928

Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji

Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika

Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa.

Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidiplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)

Chanzo: Jambo Tv
Duuh
 
Mlisema bandari zote kapewa DP World, mbona tunaona na wengine wanapewa bandqr7 zingine wazijenge kisasa na kuziendesha?

Kulikoni?
 
Back
Top Bottom