Profesa Shivji: Wasomi wanaogopa kukosoa Serikali ili wapate teuzi. Hawana msaada tena kwa jamii ya Watanzania

Wakati wa mjadala wa katiba ya Warioba yeye mwenyewe alitupiga.
 
Alichosema ni sahii. Njaa imezidi kwa wasomi wetu.
 
Tanzania sisi bado sana, unakuta unakosoa kwa takwimu. Lakini majina ya ovyo ovyo ndiyo yanatawala. Tumeishia kufaatilia udaku na umbeya wa kufikirika. Tulipandikizwa chuki mbaya sana!
 
Rais aongoze na kubadilisha mitizamo mindset kwa kuteua wasomi wanaotoa mawazo mapya na wanaokosoa serikali kwa mawazo mbadala ili wasomi wajifunze na kuona umuhimu wa kukosoa bila woga. Kinyume cha kuteua wenye kusifia na kutosema au kokosoa
 
Hii habari haipo balanced imeungwaungwa. Ukimsikiliza vizuri na kumuelewa Prof. Shivji anachokiongelea ni wasomi kuacha jukumu lao la msingi la kitaaluma na kuigeukia siasa. Kwa maana ya siasa ndo inayolipa zaidi kuliko usomi. Hivyo wasomi wengi wameamua kuweka maslahi yao mbele kuliko maslahi ya umma. Huyu Aviti yeye kaongelea kitu kingine kabisa, kwamba wasomi walikua wanazibwa mdomo wasiongee tena kwa vitisho. Kwahiyo, kwa maoni yake wasomi walishindwa kutekeleza majukumu yao siyo kwa kupenda bali kwa kushinikizwa na wenye mamlaka. Ukimsikiliza vizuri, utagundua ndo hawa wasomi ambao shivji anawaongelea kwamba wameacha usomi wamegeukia siasa.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Prof. Shivji apewe ulinzi
 
Rof. Shivji yupo sahihi sana. Japo hajaeleza ukweli kuwa kwa sasa, hawa wanaoitwa wasomi, wamegawanyika sehemu mbili:

1) Wapo wasomi, ambao ni wasomi, lakini wanagiki, waongo, wachumia tumbo. Mfano mzuri wa kundi hili ni Prof. Kabudi.

2) Wapo wasomi, lakini siyo wasomi, ni wasomi fake. Hawa ni wale walioununua usomi ili tu waitwe wasomi, wakiamini wakiitwa wasomi, watakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kujaza matumbo, japo ukweli ni kuwa siyo wasomi. Hawa ni wevi wa taaluma, wanafiki, wazandiki, waongo ja watu wenye hila. Mfano mzuri wa kundi hili ni Mwigulu, Biteko, Musukuma.
 
wasomi walikuwa zamani.Siku hizi profesa anazidiwa kila kitu na mtu wa darasa la saba si wamazo wala uchumi.
 
... kaongea ukweli tena ukweli tupu! Bila Katiba Mpya itakayohakikisha haki ya kila mwenye sifa kupata kazi sio upendeleo au hisani ya wenye mamlaka taifa halitakaa lipige hatua. Wasomi wa ukweli wasiopenda kujipendekeza wamebaki watazamaji tu.
Prof kastuka kumekucha au? Hakuwepi 2016-mwanzoni mwa 2021?
 
Ukimkosoa mama, tunakulambisha chuma tu
 
Hv kwann unalazimisha ulivyoelewa ww na wengine waelewe hvyohvyo????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…