Profesa Tibaijuka: Mikataba yote tunayoambiwa ni ya Siri ni mibovu. Ashangaa kwanini wananchi wapo kimya

Profesa Tibaijuka: Mikataba yote tunayoambiwa ni ya Siri ni mibovu. Ashangaa kwanini wananchi wapo kimya

Akihojiwa na watangazaji wa Clouds fm ni kwanini licha ya kuwa na wasomi wengi lakini bado nchi inaingia hasara kwenye mikataba mbalimbali amesema kuna shida kubwa sana kuamini kwamba eti wasomi watatusaidia kwani hata hao wasomi hupitiwa na shetani na kuingia mikataba mibovu.

Amesema kiashiria cha mikataba kuwa mibovu ni hiyo mikataba kuwa ya Siri. Ukisikia tu mkataba wa Siri jua huo ni mibovu. Kama sio mibovu ni kwa maslahi ya umma kwa nini uwe Siri?

Aidha Profesa Tibaijuka anashangazwa sana na ukimya wa wananchi hasa wanapobaini kuna mikataba ya ovyo namna hii inayoitwa ya Siri.

Ameshamaliza bilioni 1 yake ya mboga, sasa anaaza kuwashwa washwa.
 
Muogope sana mtu ambaye anaongea vitu ambayo tunachukulia poa ila baada ya miaka kadhaa mbele, tunarejea kusikiliza tena na tena kile alichomaanisha....muogope sana huyo mtu
 
Back
Top Bottom