Profesa Tibaijuka: Mikataba yote tunayoambiwa ni ya Siri ni mibovu. Ashangaa kwanini wananchi wapo kimya

Profesa Tibaijuka: Mikataba yote tunayoambiwa ni ya Siri ni mibovu. Ashangaa kwanini wananchi wapo kimya

Nasisi tunashangaa kwanini wasomi wapo kimya, wasomi nao wanashangaa kwanini wananchi wapo kimya, wananchi nao wanashangaa kwanini wazee wapo kimyaa, wazee nao wanashangaa kwanini vijana wapo kimya kwa ufupi tunashangaana.

Hakuna wa kulaumu hapa.sisi sote ni watanzania tunaopaswa kila mmoja wetu kwa nafasi yake achukue hatua kukemea maovu na kuunga mkono mazuri!
 
Inashangaza sana.

Alipokuwa kwenye system lile sakata la IPTL lilimhusu na hakuona huruma kwa wananchi, sasa ndio anaona.

Inakuwa kama mtu ukipewa madaraka akili unazifungia kwenye sanduku mpaka muda wa cheo uishe.
badala ya kumshambulia ka kejili ni vizuri kumpa pongezi maana yeye leo kapata uthubutu wa kusema hivyo ni heri yeye aliyesema na tufahamu kwamba siye yeye mwenyewe anayefahamu uovu uliopo ndani ya hiyo mikataba bali wapo wengine wengi tu wanaofahamu kwa sababu walishiriki katika kuipitisha lakini kati yao hayupo wa kuusema ukweli kama yeye.

na endapo wangekuwepo wengine wa kuusema ukweli kama yeye basi sauti zao zingetosha kukomesha vitendo hivi vya ushiriki wa viongozi kuandaa mikataba mibovu.

Hongera tibaijuka kwa kutueleza ukweli kuhusiana na mikataba mibovu inayosainiwa na serikali!
 
Akihojiwa na watangazaji wa Clouds fm ni kwanini licha ya kuwa na wasomi wengi lakini bado nchi inaingia hasara kwenye mikataba mbalimbali amesema kuna shida kubwa sana kuamini kwamba eti wasomi watatusaidia kwani hata hao wasomi hupitiwa na shetani na kuingia mikataba mibovu.

Amesema kiashiria cha mikataba kuwa mibovu ni hiyo mikataba kuwa ya Siri. Ukisikia tu mkataba wa Siri jua huo ni mibovu. Kama sio mibovu ni kwa maslahi ya umma kwa nini uwe Siri?

Aidha Profesa Tibaijuka anashangazwa sana na ukimya wa wananchi hasa wanapobaini kuna mikataba ya ovyo namna hii inayoitwa ya Siri.

Hongera Professa Anna Kajumulo Tibaijuka Kwa kutufungua macho na masikio
 
Tiketi za ubaya ubwela zimeisha. Jezi elfu 42 Hilo tunafuatilia kweli. Lakini mambo ya msingi Kwa faida ya watoto wetu na wajukuu wetu tukiulizwa tuna majibu mepesi et tutafanyaje Sasa! Aliyeturoga kafa angekuwapo tungemlazisha atutoe kwenye chupa!
Kama kuna uchawi nchi hiii imerogwa basi ni kuwekeza nguvu nyingi sana kwenye mipira ya simba na yanga badala ya kufikiri sana juu ya maendeleo ya nchi na wananchi
 
Mkuu Kuta, KUTATABHETAKULE , kwanza ni kweli kabisa mikataba mingi ina kipengele hicho cha non disclosure kwa ajili ya kulinda siri za biashara, lakini kwa mikataba kuhusu rasilimali za taifa, haipaswi kuwa siri kwasababu inahusu public property, wenye nchi ni wananchi na sio serikali, hivyo wenye mali has the right kujua kuhusu hatma ya mali zao, ndio maana tukaamua mikataba yote ya rasilimali za taifa lazima ipitishwe bungeni bunge liridhie, na ndicho kilichofanyika kwenye ile IGA ya DPW na Bandari zetu.

Nikaomba HGA pia iwe public isiwe siri, Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! nikatoa ombi hili Baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu, licha ya mapungufu, HGA yake inakuja. Ombi kwa Serikali yetu sikivu, tunaomba Maximum Transparency kwenye HGA halikusikilizwa!, ile HGA ni siri, ila ile IGA ya kimaghumashi iliwekwa pembeni for illegality!.
P
Ninyi kina Pasco mnafaa sana kutufungua macho wananchi niwaombee msinunuliwe na vyeo au pesa maana ni kama watawala hutamani sana kuwatawala wasiojua kitu na pia watu wakiwa mamlakani huzimwa vinywa.
 
Akihojiwa na watangazaji wa Clouds fm ni kwanini licha ya kuwa na wasomi wengi lakini bado nchi inaingia hasara kwenye mikataba mbalimbali amesema kuna shida kubwa sana kuamini kwamba eti wasomi watatusaidia kwani hata hao wasomi hupitiwa na shetani na kuingia mikataba mibovu.

Amesema kiashiria cha mikataba kuwa mibovu ni hiyo mikataba kuwa ya Siri. Ukisikia tu mkataba wa Siri jua huo ni mibovu. Kama sio mibovu ni kwa maslahi ya umma kwa nini uwe Siri?

Aidha Profesa Tibaijuka anashangazwa sana na ukimya wa wananchi hasa wanapobaini kuna mikataba ya ovyo namna hii inayoitwa ya Siri.

Alitaka Wananchi wafanye kitu gàni?
 
Wasomi wenye msaada kwa nchi .
 
Tibaijuka wewe kachore ramani za miji tu, Huna ulijuwalo katika mikataba ya kibisahra.

Kifafanuwe kifungu hiki tu, labda utatia akili" non-disclosure agreement".
 
Back
Top Bottom