Profesa Tibaijuka: Trump kusitisha misaada ARVs zitaadimika Afrika. African Union iitishe kikao maalum kuweka mkakati

Profesa Tibaijuka: Trump kusitisha misaada ARVs zitaadimika Afrika. African Union iitishe kikao maalum kuweka mkakati

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mbunge wa zamani wa Muleba, Prof Tibaijuka amesema kitendo cha Rais Trump wa US kusimamisha msaada ya kimataifa kitaleta Kiama Tanzania na Afrika

Pia soma > Trump asimamisha misaada kwa nchi nyingine kwa siku 90 ili kupitiwa upya. Tanzania nayo kuathirika

Trump amezuia misaada ya sekta za afya nk Ili Kufanya ukaguzi kama misasda hiyo inatumika kwa usahihi au fedha zinaishia mifukoni mwa eahuni wachache

Ahsanteni sana

---
Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Prof. Tibaijuka amesema “Upatikanaji wa madawa ya kuongeza kinga za mwili ARVs utaathirika, ninashauri Wizara ya Afya kuufahamisha umma wa Watanzania je ni hatua gani za haraka zinachukuliwa kutathmini jambo hili na kuchukua hatua stahiki?, ikibidi African Union waitishe kikao maalum kuangalia suala hili na kuweka mkakati wa pamoja, Waathirika wa gonjwa hili la UKIMWI ni Waafrika na ugonjwa haujulikani ulitoka wapi?, tujitetee”

“Aidha juhudi za kuthibiti maambukizi ya virusi vya UKIMWI ziwekewe nguvu mpya, upatikanaji wa ARVs utakuwa mgumu na kununua ARVs kibiashara ni jambo litakalohitaji bajeti kubwa na uwezo wa taifa kwa ujumla ni mdogo na jambo limekuwa la ghafla, Waathirika wengi hawana uwezo kununua madawa hayo wenyewe maisha yao yote”

“Afya zao zikidhoofika itatumika gharama kubwa kuwauguza hivo kusababisha umaskini na vifo, pia bila ARVs maambukizi yatashika kasi mpya, tuwe macho”
 
Mbunge wa zamani wa Muleba, Prof Tibaijuka amesema kitendo cha Rais Trump wa US kusimamisha msaada ya kimataifa kitaleta Kiama Tanzania na Afrika

Pia soma > Trump asimamisha misaada kwa nchi nyingine kwa siku 90 ili kupitiwa upya. Tanzania nayo kuathirika

Trump amezuia misaada ya sekta za afya nk Ili Kufanya ukaguzi kama misasda hiyo inatumika kwa usahihi au fedha zinaishia mifukoni mwa eahuni wachache

Ahsanteni sana
Wee profesa nilijua una ukili kumbe huna akili hata chembe ,wacheni kuwa PARASITE .Trump sawa sawa asimamishe misaada ,nchi zina kila kitu lkn UFISADI UMEZIDI .Tanzania ina Majirani zaidi ya nchi tano vp Tz tutegemee USA wacheni UJINGA huo.Serikali hamna VISIONS.
 
Hiyo misaada atawapa mama yenu Samia.

Maana daraja likijengwa utasikia mama ametoa bilioni kadhaa ujenzi wa daraja, huyo mama ananunua kila goli milioni 5-10 Simba na Yanga wakifunga.

Nimewahi kuuliza sana humu hizo pesa anatoa wapi na analipwa mshahara kiasi gani nikaishia kujibiwa mama anazo pesa nyingi maana hata Magufuli alikuwa anagawa mtaani pesa zote ni za rais.

Hivyo dawa na vitu vingine vyote basi awanunulie mama yenu Samia msitusumbue.
 
Mbunge wa zamani wa Muleba, Prof Tibaijuka amesema kitendo cha Rais Trump wa US kusimamisha msaada ya kimataifa kitaleta Kiama Tanzania na Afrika

Pia soma > Trump asimamisha misaada kwa nchi nyingine kwa siku 90 ili kupitiwa upya. Tanzania nayo kuathirika

Trump amezuia misaada ya sekta za afya nk Ili Kufanya ukaguzi kama misasda hiyo inatumika kwa usahihi au fedha zinaishia mifukoni mwa eahuni wachache

Ahsanteni sana

Trump yupo sahihi, kila nchi ianze kujitambua na kuanza kujitegemea wao wenyewe Sasa, wasiendelee kuitegemea Marekani. Safi Sana hii, hii itawalazimisha Watu wengine waliopo duniani kote hususani Watu weusi kuanza kujitambua na kupata akili nzuri ya kuweza kujitegemea. Hatua hizi za Utawala wa Trump ni Kama 'Black Consciousness Campaign' kwa Watu weusi wote kabisa hapa duniani ili waache kutegemea Misaada kutoka Marekani. Ni mwanzo mzuri.

Kwanza Watawala wengi sana wa kutoka katika nchi za Afrika pamoja na Vibaraka wao daima wamekuwa wakiwasema vibaya sana Wazungu hususani Watu wa Marekani kuwa ni Mabeberu na Wapenda Ushoga, Sasa kwa hatua hizi za Utawala wa Trump zitasaidia Sana kukomeshwa kwa hiyo Misaada inayodaiwa kuwa eti 'imetoka na Mabeberu na Wapenda Ushoga.'
Watu wa Afrika (Watu weusi) hususani waTanzania sasa wanatakiwa waelekeze maombi yao ya Misaada kwenda kwa Marafiki zao wa nchi za Mashariki ambao wanawaona kuwa siyo Mabeberu na Wasiopenda Ushoga, nchi za China, Urusi, Korea ya Kaskazini, Belarus, n.k ili waweze kupatiwa Misaada kutoka huko.
 
Kiama gan wakati asilimia kubwa ya hela ya misaada inaishia mifukoni mwa viongozi. Nashangaa kuendelea kutupa misaada huku wakijua hela zao zinaliwa. Na mataifa mengine makubwa yafuate mfano wa Trump.
Acha kuwa na akili fupi kuna taasisi kibao wameajiri watz zipo bongo. Marekani aki pull out watu wanakosa ajija kuna water read nk
 
EO imesema anaangalia kama inaendana na foreign policy ya US ,kwahiyo ni usimamishaji wa mda pia wanaangalia namna ya kuitoa hiyo misaada ,inaonekana kuna watu wanajinufaisha kuanzia huko kwao hadi nchi kadhaa.

EO zake zinaathari kubwa kwa uchumi na uhusiano wa kimataifa wa dunia.
 
Watakoumia ni watu wa chini wanaonufaika moja kwa moja na misada hyo
Wa chini ni wa wapi kama kujifungua tu mama mjamzito kama huna hela 50k unaambiwa ukamzalishe mke/dada/mama/shemeji nyumbani?!
Tembelea hosptital nyngi huduma ni mbovu na gharama zipo juu sana.

Trump akaze ivo ivo turudi kwenye mitishamba na tiba mbadala!
 
Back
Top Bottom