Profesa Tibaijuka: Trump kusitisha misaada ARVs zitaadimika Afrika. African Union iitishe kikao maalum kuweka mkakati

Profesa Tibaijuka: Trump kusitisha misaada ARVs zitaadimika Afrika. African Union iitishe kikao maalum kuweka mkakati

BREAKING NEWS KUTOKA KWA RAIS TRUMP INAYOTUHUSU NI AFYA ZA MAMILIONI YA WATU KUWA HATARINI. Ikiwa uamuzi wake kusitisha misaada kwa mashirika ya afya duniani hasa PEPFAR na GLOBAL FUND yatatekelezwa ni kiama. Upatikanaji wa madawa ya kuongeza kinga za mwili ARVs utaathirika. Ninashauri Wizara ya Afya kuufahamisha umma wa waTanzania je ni hatua gani za haraka zinachukuliwa kutathmini jambo hili na kuchukua hatua stahiki?.

Ikibidi African Union waitishe kikao maalum kuangalia swala hili na kuweka mkakati wa pamoja. Waathirika wa gonjwa hili la UKIMWI ni waAfrika na ugonjwa haujulikani ulitoka wapi?. Tujitetee.

Aidha juhudi za kuthibiti maambukizi ya virus vya ukimwi ziwekewe nguvu mpya. Upatikanaji wa ARVs utakuwa mgumu. Na kununua ARVs kibiashara ni jambo litakalohitaji bajeti kubwa na uwezo wa taifa kwa ujumla ni mdogo. Na jambo limekuwa la ghafla. Waathirika wengi hawana uwezo kununua madawa hayo wenyewe maisha yao yote. Afya zao zikidhoofika itatumika gharama kubwa kuwauguza hivo kusababisha umaskini na vifo. Pia bila ARVs maambukizi yatashika kasi mpya. Tuwe macho
 
Back
Top Bottom