TANZIA Profesa Tolly Mbwette afariki dunia

Jamani ndiyo globalization hiyo...ina faida na hasara...Sasa Sina hakika Kama hasara zimetawala zaidi au kinyume chake....post modenism scholars watueleze..
 
Corona bado IPO SANA we kijana, usilaumu Wahindi wa Agakhan bure. Ilaumu Serikali yako kwa kupuuzia na kulaghai wajinga kama ninyi kwamba COVID-19 imekwisha.
Ni kweli Corona Bado ipo tena Sana...lakini serikali haijasema kuwa imekwisha...
 
Hawa ndio wasomi wanaotakiwa kwenye taifa maskini kama Tanzania! Yaani wanasoma, kisha wanasambaza elimu yao kwa Watanzania wengine badala ya hawa wehu ambao wakisoma, wanakimbilia kwenye siasa na wanacho-deliver huko, hakina tofauti na wanacho-deliver watu wa bachelor degree kushuka chini.

Rest In Peace Prof
 
Upumzike kwa amani Prof. Tolly Mbwette.
 
Sio ujinga.kukosa elimu sio ujinga.huwezi kumfaham mtaalam wa magali kama huna gali.huwezi kuwafaham mafundi wazuri kama hujajenga.huwezi kuujua ukuu wa Mungu kama hujaingia kanisani au msikitini.hvyo wewe unamjua kwa sababu umesoma university. Sasa MTU aliyeishia la saba atamjuaje.labda awe jilani au ndugu.wanamziki wanajulikana sana kuliko hata marais wa nchi
Hadi sasa hujajua tatizo lilipo?
Ujinga
Maradhi
Umasikini
Komaa na hilo la kwanza
 
Ni kweli Corona Bado ipo tena Sana...lakini serikali haijasema kuwa imekwisha...

Kwa kutoweka wazi takwimu za athari wala maeneo athirika, serikali imewatoa kafara wengi.

Kama ilivyoitishwa listi ya wanaotutoka kwa changamoto za kupumua inaendelea kuhuishwa.

Maeneo yapi, mikoa ipi wazee na wenye magonjwa mengine wayaepuke?

Serikali mnaweka siri kwa maslahi yenu. Yaja siku ile you shall be held to account.

Kila jina litasomwa mbele zenu.

Pumzika kwa amani Prof. Mbwette.
 
Hii Agakhan hiii!! Yaani wengi wanaolazwa hapo wanakufa Why? Mmarangu Coach, Mze Makoi wa TRC Enzi hiyo, Mke wa Tale na Leo Prof Mbwete!! RIP Professor. Umetuachia urithi wa ViMbwete
Ulishaa kaa karibu na chumba cha maiti muhimbili ukaona maiti zinazolerwa pale?
 
Sawa.....ila kutoa takwimu za Kila siku za Corona ni ujinga uliopitiliza...takwimu hazisaidii kuondoa Corona...virusi hivi vitaondolewa kwa kweka tahadhari namna ya kujikinga...kwa hili hata Mimi naona serikali ingeongeza bidii katika kutoa elimu...kwa mfano suala la uvaaji barakoa, kunawa mikono na sanitizing serikali. Iweke mkazo zaidi...Sasa hivi watu wengi hawavai barakoa...hapo hata Mimi naona serikali inakosea...lakini hili la takwimu it is a very stupid thing..mabeberu wanna ajenda zao...
 
Kufikiri beberu ana agenda na takwimu zetu ili tujikinge na kifo kwa maslahi yetu ni jambo la kushangaza kuliko.

Kwa nini beberu awe katika hili wakati tukiwa hai ni sisi na tukifa ni sisi?

Inaingia akilini kweli?

Beberu hasa kwenye hili ni nani?
 
Issue hapa ni kuwa kwanini wanakazania takwimu kuliko vingine...mabeberu au vicious, ni washenzi na savages...tunataka tupone...na siyo takwimu...mbona malaria watu wanakufa kwa siku kuliko Corona lakini hawasemi wanataka takwimu?
 
Jamaa kaandika Giggy money maarufu kwenye korido za vyuo vikuu kuliko marehemu Tolly
 
Issue hapa ni kuwa kwanini wanakazania takwimu kuliko vingine...mabeberu au vicious, ni washenzi na savages...tunataka tupone...na siyo takwimu...mbona malaria watu wanakufa kwa siku kuliko Corona lakini hawasemi wanataka takwimu?

Kuna kitu unakiruka mkuu. Kuna tofauti kubwa baina ya malaria na Corona. Hasa kwenye maambukizi.

Watu wakijua hali halisi na hasa maeneo athirika watachukua tahadhari hata za kutokwenda huko.

Kumbuka kuangalia Corona kwenye upande maambukizi zaidi kuliko hata kwenye kuugua. Wapo walio vulnerable zaidi hawa tunawalinda vipi bila takwimu na hali halisi?

Beberu? Hiyo ni janja janja tu mkuu ya kukwepa majukumu.

Wakufa ni sisi na wa kupona ni sisi. Beberu hana issue hapo tufe au tuishi that is upon us.
 
Ni kweli Corona Bado ipo tena Sana...lakini serikali haijasema kuwa imekwisha...
Acha upuuzi wewe, kazi kusifia ujinga ujinga tu. Hujawahi kumsikia magufuli anapongeza watu wasiovaa barakoa? Ungekuwa karibu yangu ningekunasana vibao, shenzy.
 
Sisi tunakufa sawa...sibishi...ila mibeberu inakufa zaidi...hakuna janja janja ..takwimu zinatisha...italeta hofu..uchumi utakufa na ndicho mabeberu wanachotaka yaani uchumi wetu ufe...
 
Acha upuuzi wewe, kazi kusifia ujinga ujinga tu. Hujawahi kumsikia magufuli anapongeza watu wasiovaa barakoa? Ungekuwa karibu yangu ningekunasana vibao, shenzy.
Kwani huwezi ukaweka comment yako na kujadiliana bila matusi na kejeli?! You can't do that??... Kwani wewe hujamsukia Magufuli amisema tuendelee kuchukua tahadhari??
 
Kwani huwezi ukaweka comment yako na kujadiliana bila matusi na kejeli?! You can't do that??... Kwani wewe hujamsukia Magufuli amisema tuendelee kuchukua tahadhari??
Tahadhari gani wakati amekataza watu wasivae barakoa? Acha ubishi wa kijinga aisee, sio kila jambo la kusifia tu kama uko Lumumba.
 
Sisi tunakufa sawa...sibishi...ila mibeberu inakufa zaidi...hakuna janja janja ..takwimu zinatisha...italeta hofu..uchumi utakufa na ndicho mabeberu wanachotaka yaani uchumi wetu ufe...

Mkuu suala la kufa au kuishi siyo mashindano ya nchi na nchi.

Hudhani kuwa wazee na wenye magonjwa mengine wako kwenye hatari zaidi na hii ya kukumbatia taarifa?

Pana simba mtaani wanazurura. Ungependa kujua ni mitaa ya mkoa gani au haina shida ukakutane nao tu mbele kwa mbele?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…