TANZIA Profesa Tolly Mbwette afariki dunia

TANZIA Profesa Tolly Mbwette afariki dunia

Jibu ni watu wanapenda udaku..uzi ulijaa uzushi zushi na udaku[emoji1787]
Proff mashuhuli amefariki uzi hautembei kabisa ume-stuck...
juzi amefariki mke wa Tale uzi ulikuwa unakimbia speed 120.......
sijui tatizo liko wp!?
 
classroom engineers

hawana lolote

Wakitaka kujenga ghorofa tatu kwenda juu hapa Tanzania lazima wamwite civil engineer Mchina.

wakijenga daraja linasombwa na manyunyu

wakijenga ukuta unachanwa na mfinyanzi

wakijenga barabara inaota mawimbi
 
Hii sikuijua kuhusu vimbwete kumbe ni yeye ndio mwanzilishi hongera Sana.
 
Poleni wana familia, pole ya kupoteza, Mbwete apumzike pahali pema Peponi
 
Mazishi yatafanyika Jumatatu 6/7/2020 katika Kijiji cha Irambo, wilaya ya Mbeya vijijini.
 
Jumapili 5/7/2020 mwili utachukuliwa Aghakhan na kupelekwa nyumbani kwake Kimara Suka.
Halafu utapelekwa Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Baada ya taratibu za chuoni safari ya kwenda Irambo, Mbeya itaanza jioni ya siku hiyo hiyo ya Jumapili.
 
Hii hospitali ni gharama lakini hakuna lolote
Wataalamu wa kihindi vijana walio some a udaktari vyombo havieleweki wote wana degree za kuungaunga.
Ni vigumu kuona serikali imelifumbia macho hili
Ni hospitali inaajiri wahindi kuliko wataalamu
Ni bora Muhimbili kuliko hii hospitali
Usafi na uzuri wa majengo wengi wanaamini na waganga wana degree lukuki za kutoa huduma wakapona. Wajawazito wengi wanapoteza maisha hapo.

RIP Professor
Corona bado IPO SANA we kijana, usilaumu Wahindi wa Agakhan bure. Ilaumu Serikali yako kwa kupuuzia na kulaghai wajinga kama ninyi kwamba COVID-19 imekwisha.
 
Mbona umeandika kinyume mkuu? Ni mbwete kaacha vimbweta
Ni Professor Mbwete kaacha " Vimbwete". Ni mmojawapo wa WaTz Waliopata kusafiri Ughaibuni kujifunza, akaleta mazuri ya huko Kwa faida ya Wote. Bravo ViMbwete kwenye bustani zetu za Vyuo na Shule.
 
Sentensi hii ukiwa umefiwa na ndugu yako utaipenda? "mbapo ni mambo mawili tu kupata uzima wa milele au mauti ya milele, Bwana atupe hekima tulio hai kuzihesabu siku zetu" Yaishe kwaheri
Well said
 
Vimbwete,sisi wa Mlimani enzi za Prof. G. Mmari & Prof. M. Luhanga tunajua Vimbwete.
Watoto wa Mkandala na Anangyise na kina SAUT,SJUITS,UDOM,MUCCOBS,etc ndio mnajua Vimbweta.
Duh...uko sahihi...
 
Back
Top Bottom