TANZIA Professor James Shaba afariki dunia. Alifanyia postmortem mwili wa Hayati Sokoine

Profesa mtambuzi wa vifo llkn kashindwa kujua yeye lini atakufa.
Allah akbar.
Mtume Muhammad watu walimuuliza kuhusu kifo. AKAWAAMBIA ANAOJUA KIFO NI ALLAH PEKEE YAKE
Sidhani kama imekusudiwa kuwa anatambua siku ya kufa mtu. Ni daktari aliyekuwa anashughulika na maiti ili kutambua sababu za kifo chake. Kwa hivyo yeye ni mpaka mtu afe ndiyo afanye uchunguzi.
 
Proffessor akameza fundo la Konyagi akawajibu wale vijana,
Wewe jamaa...., ulisha andika kitabu watu wakusome?
Umri umekwenda, lakini wakati ndio mzuri huu wa kutumia kipaji chako kumalizia zilizobaki.

Mimi napendekeza kitabu kinachofaa ukiandike: Jinsi mlivyoyaua mashirika ya wananchi (mashirika ya Umma).

Naahidi kukununua nakala ya kwanza ya hicho kitabu niisome kwa makini.

Ulivyo mwelezea hapo Profesa Shaba, hasa kuhusu hayo maneno aliyowapa hao vijana akina George Mazula; huyo ndiye aliyekuwa Profesa Shaba mwenyewe, katika mazingira ya aina hiyo ulivyo yaelezea wewe.
 
Mkuu nilisha andika kitabu toka 2005, ila sijakitangaza sana kwa vile kinagusa maisha ya watu ambao bado wako hai.

Watu wanafikiri ufisadi umeanza sasa, ulikuwepo kitambo.
 
Hakuwa na baya na mtu, yeye ni taaluma yaka na kawiski kale basi.
 
Sidhani kama imekusudiwa kuwa anatambua siku ya kufa mtu. Ni daktari aliyekuwa anashughulika na maiti ili kutambua sababu za kifo chake. Kwa hivyo yeye ni mpaka mtu afe ndiyo afanye uchunguzi.
Huyo mpuuzi ametoa negative opinion kwa vile Profesa alikuwa siyo Muislam mwenzake malaria sugu ana upuuzi mwingi sana
 
Hivi nyerere hakuwahi kuwa waziri mkuu?

Mh. Julius Kambarage Nyerere​

Waziri Mkuu Mstaafu
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni Waziri Mkuu wa Kwanza wa Serikali ya Tanganyika Huru kuanzia tarehe 9 Desemba, 1961 hadi tarehe 22 Januari, 1962 alipojiuzulu na kumwachia wadhifa huo Mheshimiwa Rashid Mfaume Kawawa ili yeye aende kuiimarisha TANU mikoani.
 
Pumzika Prof Shaba. Nakumbuka siku moja ulitukuta pale mtaani Shaaban Robert na Ghana Avenue ukiwa umelewa ukatuomba tukupeleke nyumbani kwako kule Ocean Road usiku kama wa saa tatu, nilikuwa mimi na marafiki wawili wa mtaani.

Njiani tukiwa tumekushika mikono yote miwili tukaanza kukuuliza maswali ya uchokozi, kwamba Pombe na Bangi kipi kina madhara kwenye mwili wa binadamu?, ulikuwa umelewa lakini ukiwa na akili yenye kuweza kutupa elimu, ukatuambia kwamba Bangi inakwenda moja kwa moja kichwani na kuharibu ubongo wakati Pombe inakwenda kwenye mifumo ya damu.

Ukasema tukitaka kuchanganyikiwa mapema zaidi basi tuvute bangi kwa wingi, tukabaki tunacheka tu. Tulipokufikisha nyumbani kwako bahati nzuri Mama Hamish [Marehemu Mke wako] akaja kutufungulia na kutushukuru kwa kukufikisha salama nyumbani.

Upumzike kwa amani Profesa Shaba, nitakumbuka mchango wako wa kuutunza mwili wa hayati Edward Sokoine mpaka alipopelekwa kuzikwa kwao Monduli Juu.

Nitaendelea kukumbuka namna tulivyokuwa tukikutana Chinese Restaurant, IFM na Kilimanjaro Hotel ukiwa unayumba huku ukichekesha wazee wanywaji wenzako ambao wengi wao walikuwa ni wazee wa mitaa ile ile tuliyoishi miaka ile.

Maisha ni mafupi na wote juu ya uso wa dunia tunapita tu. RIP Profesa Shaba.
 
Wakati anaitumikia nchi hii wewe pengine ulikuwa unatembea kwenye viuno vya Baba yako mzazi, huna mamlaka ya kimaadili ya kumhukumu.
 
Kwani wewe ulidhani nani?
Mwalimu Nyerere, ni wa Tanganyika.

Kawawa ni wa Tanzania? Hebu cheki hiyo! Mi nadhani naye ni wa Tanganyika.
Rashid Mfaume Kawawa alikuwa waziri mkuu wa mwisho wa Tanganyika January 1962 mpk 9 December 1962.

Kuanzia 10 December 1962 mpk February 1972 nafasi ya waziri mkuu ilifutwa.

Mwaka 1972 February nafasi ya waziri mkuu ilirejeshwa na Rashid Mfaume Kawawa akawa waziri mkuu wa kwanza wa Tanzania mpk mwaka 1977.

Kawawa alifuatiwa na Sokoine
 
Wakati anaitumikia nchi hii wewe pengine ulikuwa unatembea kwenye viuno vya Baba yako mzazi, huna mamlaka ya kimaadili ya kumhukumu.
wapi kamhukumu? nyinyi vichwa panzi ndio mnasababisha unafiki na uchawa utamalaki hamtaki kusikia negative views za mnaohisi mnawapenda.
u have to be open minded if u want to progress in all aspects.
 
Kaka Mayala hv huyu the late Proffessor alikuwa na undugu na yule former minister na colleague wa Mwalimu Nyerere kwenye serikali yake Mzee Austin Shaba?
 
wapi kamhukumu? nyinyi vichwa panzi ndio mnasababisha unafiki na uchawa utamalaki hamtaki kusikia negative views za mnaohisi mnawapenda.
u have to be open minded if u want to progress in all aspects.
Profesa Shaba alikuwa ni mtu mwenye heshima kubwa sana hapa nchini na alisomesha watoto wake, akawa akila matunda mpaka siku anaaga dunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…