TANZIA Professor James Shaba afariki dunia. Alifanyia postmortem mwili wa Hayati Sokoine

TANZIA Professor James Shaba afariki dunia. Alifanyia postmortem mwili wa Hayati Sokoine

Kweli wahenga walisema, muda unaongea, na wenzetu walisema, Time Heals!
Ni mwaka 1984, ndiyo kwanza kijana mtanashati, msomi na nimepata kazi nzuri shirika la umma!
Ndio kwanza nimehamishiwa Dar toka mkoani, sasa niko makao makuu ya shirika langu.
Kwa sheria za kazi miaka hiyo nilikuwa -entitled" kupatiwa nyumba.
Kwa vile nilikuwa bado sijapatiwa nyumba, mwajiri wangu aliniweka hotel kubwa ya kisasa, New Africa Hotel,
Siku hiyo ilikuwa week end mimi niko Bandari Grill, na girlfriend wangu, ambaye atakuja kuwa mke wangu.

Pembeni yangu kama meza ya tatu ,nikamwona mzee mmoja yuko peke yake, akinywa Konyagi, kavu na huku yuko kimya.

Mara wakaingia vijana, kaka zangu, mmoja namfahamu ni Pilot, Captain wa Air Tanzania, lakini yeye hanifahamu.
Nilimfahamu Kapteni George Mazula kwa vile nilikuwa na safari nyingi Mwanza , Arusha na Musoma miaka hiyo na ndege aina ya Fokker Friendship, F50.

Sasa wale vijana kaka zangu, wakaingia wakaanza kumzonga yule mzee.
Wakaanza kumcheka wanamwambia "Profesa uko njwii, uko njwii....acha Konyagi Profesa Shaba"

Nikageuka kumtazama huyo mzee, na nikajiuliza, kumbe huyu ndiye Profesa Shaba?
Jina lilikuwa linajulikana sana, lakini mtu mwenyewe mfupi na mwembamba na ndevu za kutosha usoni, nilikuwa sijawahi kumwona.

Proffessor akameza fundo la Konyagi akawajibu wale vijana,
"Ninyi vijana, ninyi vijana" na huku akionyesha wazi kuwa kinywaji kimekolea.
"Ninyi vijana mtakuja tu mortuary, mtakuja tu. Nimemwona Sokoine nanyi mtakuja tu"

Mwaka huo ndo kwanza amefariki Waziri Mkuu Edward Sokoine, na bado msiba ule wa kitaifa uko fresh mioyoni mwa watu wengi.

Wale vijana na Capt Mazula, walitoweka pale kama wamefukuzwa au kugusa umeme, wote wakaogopa na kutokomea haraka haraka.

Nami nilipigwa butwaa ,lakini nikamsalimia kwa adabu, "shikamoo Proffessor Shaba"

Tukaanza maongezi, lakini kwa jinsi nilivyo mchukulia kiheshima nikagundua kuwa amekulia Tukuyu na alikuwa anaifahamu familia yangu toka babu yangu.

RIP Proffessor James Shaba, Mungu akuweke mahali pema peponi.
Aisee Kuna Raha kupata stories kama hizi
 
Dr Kasambala ni mjomba wangu toka kijijini.
1975 tumefanya kazi wote zahanati moja kati kati ya Jiji, Dr Kasambala akitokea Muhimbili.
Alikiwa mtu wa whiskey kwa sana.
Miaka hiyo uliingia ugonjwa wa Alto Cholera, ndugu yake na Cholera. Ugonjwa ulikuwa haujawahi kutokea Tanzania, na ulikuwa unatisha.
Mtu anaharisha na kutapika mfululizo hadi anakufa kwa kukosa maji mwilini.

Tukiwa tea break tukamuuliza, ugonjwa huu utaisha lini?
Dr Kasambala alijibu simply, "it is here to stay".

Ugonjwa huu ulileta tafaruki nchini hadi bungeni.
Kuna mbunge toka mikoa ya mwambao aliuliza kwa waziri wa Afya, wakati huo akiwa ni Dr Leader Stirling, mzungu toka Uingereza, "ugonjwa huu mbona uko mikoa ya pwani kwa wingi, na serikali haifanyi kitu"
Dr Stirling alimjibu, "ugonjwa huu unatokana na binadamu kula vyakula vilivyo changanyika na kinyesi chake mwenyewe"

Ikatokea valangati, watu wa pwani wakaona wametukanwa na mzungu, ati wanakula kinyesi.
Joto lilikuwa kubwa hadi Dr Stirling alijiuzulu.

Lakini kiukweli Dr Stirling alikuwa sahihi.

Watu wengi wa pwani walikuwa wanawaosha maiti wao waliokufa kwa cholera kwa mikono mitupu.
Vidudu vya echoli vikaingia kwenye kucha na mikono hivyo wakati wa kula mlipuko wa ugonjwa uliendelea.
Na walikufa watu wengi hadi elimu ya kutumia madawa kuwaosha wahanga ilipoanza kuenea, na ugonjwa kupungua.

That was in the 70s to 80s.
Duuh Doctor 40 yrs ago
 
Pamoja na yote postmortem ya Edward Moringe Sokoine hakuandikwa au kuwekwa wazi.

Na ndiyo maana wanae walipoamua kuhamisha mwili pale ulipozikwa ulisimamiwa na wabeba mtutu.

All in all asingewezza kupingana na Mwalimu
Mwalimu Kwa Nini alipenda kuhifadhi mambo mabaya ,ambayo yanaleta picha mbaya Sana Kwa nchi
 
Mazingira ya kufanya Kazi ni magumi jamani hacheni kuwasema madakitari kuwa ni walevi,

Kama wakiamua kuyasema yanayo wasibu kazin, basi watu wangekata tamaa kusoma mambo ya AFYA
 
Yes they are brothers, na wana Dada yao kifaa kweli kweli!, Mzee Mayalla akiwa RSO wa Mtwara, (Wazee wa Kisukuma hawazeekagi), si macho ya Dingi yakaispot, kufunga kufungua kabinti kakajiriwa Idara, mara papa!, kadunga!, kikazaliwa kidume kilapewa jina la Eric, Dingi akahamishiwa Mwanza, huko ikamkuta ile soo ya 1976!, baada ya soo kuisha 1980 si dingi akatia timu kumdai mwanae!, ndipo akaambiwa hao ni wa Makua, ni matrilinier, watoto ni mali ya Mama na wanatumia jina ubini wa kikeni!. Hata che Nkapa ni ubini wa kikeni!. Katika vitu vingumu Msukuma kuelewa ni damu yake kuibiwa na Mwanamke!. Hivyo mimi tuna undugu na kina Shaba, huyo Erick wetu tutamsaka kumkomboa tumpeleke Usukumani!.
P

"kufunga kufungua kabinti kakajiriwa Idara, mara papa!, kadunga!, kikazaliwa kidume kilapewa jina la Eric".
Gone too far young bro.
 
Dr Kasambala ni mjomba wangu toka kijijini.
1975 tumefanya kazi wote zahanati moja kati kati ya Jiji, Dr Kasambala akitokea Muhimbili.
Alikiwa mtu wa whiskey kwa sana.
Miaka hiyo uliingia ugonjwa wa Alto Cholera, ndugu yake na Cholera. Ugonjwa ulikuwa haujawahi kutokea Tanzania, na ulikuwa unatisha.
Mtu anaharisha na kutapika mfululizo hadi anakufa kwa kukosa maji mwilini.

Tukiwa tea break tukamuuliza, ugonjwa huu utaisha lini?
Dr Kasambala alijibu simply, "it is here to stay".

Ugonjwa huu ulileta tafaruki nchini hadi bungeni.
Kuna mbunge toka mikoa ya mwambao aliuliza kwa waziri wa Afya, wakati huo akiwa ni Dr Leader Stirling, mzungu toka Uingereza, "ugonjwa huu mbona uko mikoa ya pwani kwa wingi, na serikali haifanyi kitu"
Dr Stirling alimjibu, "ugonjwa huu unatokana na binadamu kula vyakula vilivyo changanyika na kinyesi chake mwenyewe"

Ikatokea valangati, watu wa pwani wakaona wametukanwa na mzungu, ati wanakula kinyesi.
Joto lilikuwa kubwa hadi Dr Stirling alijiuzulu.

Lakini kiukweli Dr Stirling alikuwa sahihi.

Watu wengi wa pwani walikuwa wanawaosha maiti wao waliokufa kwa cholera kwa mikono mitupu.
Vidudu vya echoli vikaingia kwenye kucha na mikono hivyo wakati wa kula mlipuko wa ugonjwa uliendelea.
Na walikufa watu wengi hadi elimu ya kutumia madawa kuwaosha wahanga ilipoanza kuenea, na ugonjwa kupungua.

That was in the 70s to 80s.
Kwa hiyo Nyerere alikubali Dr Stirling ajiuzulu, Huku akijua kasema ukweli, basi Haya 👆 mambo ya hovyo , yeye ndio mwanzilishi, hawa wa ss wanaiga Tu
 
Waziri mkuu wa Kwanza Nyerere Des.1961 Hadi Feb.1962 alipomwachia Kawawa na kurejea Kama Rais Mtendaji Des.1962 chini ya Katiba ya Jamhuri.Alijiuzulu kwa kufarakana na Wana TANU wenzake juu ya Africanisation kwa spidi ya kutisha wakati Taifa lilikuwa halijajitosheleza ki-manpower akiliita pia zoezi Hilo Ukaburu sawa na wa Afrika Kusini wa chama chake.Na kwa kuwa alikuwa ndiye Rais wa Chama akarejea kijijini kukijenga Chama nje ya Ukaburu huo tayari kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 1962,akapeta dhidi ya Mtemvu aliyedai Tanganyika no kwa Waafrika wenye ngozi nyeusi tu.
 
Waziri Mkuu Edward Sokoine alipofariki Aprili 1984, mwili ulilazwa Bungeni ili watu waende kutoa heshima za mwisho. Matarajio yalikuwa kwamba shughuli hiyo itafanyika kwa masaa kadhaa tu, nadhani kuanzia saa 11 jioni hadi saa 4 usiku. Baada ya hapo mwili ungepelekwa mortuary. Idadi ya watu ilikuwa kubwa sana, na ikabidi kutoa heshima kuendelee mpaka asubuhi.
Kama mkuu wa kitengo kinachohusika, Prof. Shaba ilibidi kupita kuukagua mwili kila baaada ya muda fulani, usiku kucha. Wajuzi wa habari wakawa wakiteta kwamba leo Profesa hakukitendea haki kinywaji kwa kuachana nacho kila baada ya muda fulani.
Duh
 
Back
Top Bottom