TANZIA Professor James Shaba afariki dunia. Alifanyia postmortem mwili wa Hayati Sokoine

TANZIA Professor James Shaba afariki dunia. Alifanyia postmortem mwili wa Hayati Sokoine

Hivi umenisoma vizuri au umekurupuka tu. Ndiyo maana mnafeli mitihani kiboya.
Sawa mtoaa taarifa kwenye Hilo bichwa lako umejaza ujuaji mwingi by the way pita ivi na Mimi nipite vile.....

NB:
Mods nikijibishana na Huyu mjamaa nipigwe BAN ya LIFE hapa Jukwaani

Kalagabao

✌️✌️✌️✌️
 
Sawa mtoaa taarifa kwenye Hilo bichwa lako umejaza ujuaji mwingi by the way pita ivi na Mimi nipite vile.....

NB:
Mods nikijibishana na Huyu mjamaa nipigwe BAN ya LIFE hapa Jukwaani

Kalagabao

[emoji3577][emoji3577][emoji3577][emoji3577]
Kiherehere chako tu. Ndiyo maana una makalio makubwaaaa na ndiyo unayotumia kufikiri bwege wewe.
 
Dr Kasambala ni mjomba wangu toka kijijini.
1975 tumefanya kazi wote zahanati moja kati kati ya Jiji, Dr Kasambala akitokea Muhimbili.
Alikiwa mtu wa whiskey kwa sana.
Miaka hiyo uliingia ugonjwa wa Alto Cholera, ndugu yake na Cholera. Ugonjwa ulikuwa haujawahi kutokea Tanzania, na ulikuwa unatisha.
Mtu anaharisha na kutapika mfululizo hadi anakufa kwa kukosa maji mwilini.

Tukiwa tea break tukamuuliza, ugonjwa huu utaisha lini?
Dr Kasambala alijibu simply, "it is here to stay".

Ugonjwa huu ulileta tafaruki nchini hadi bungeni.
Kuna mbunge toka mikoa ya mwambao aliuliza kwa waziri wa Afya, wakati huo akiwa ni Dr Leader Stirling, mzungu toka Uingereza, "ugonjwa huu mbona uko mikoa ya pwani kwa wingi, na serikali haifanyi kitu"
Dr Stirling alimjibu, "ugonjwa huu unatokana na binadamu kula vyakula vilivyo changanyika na kinyesi chake mwenyewe"

Ikatokea valangati, watu wa pwani wakaona wametukanwa na mzungu, ati wanakula kinyesi.
Joto lilikuwa kubwa hadi Dr Stirling alijiuzulu.

Lakini kiukweli Dr Stirling alikuwa sahihi.

Watu wengi wa pwani walikuwa wanawaosha maiti wao waliokufa kwa cholera kwa mikono mitupu.
Vidudu vya echoli vikaingia kwenye kucha na mikono hivyo wakati wa kula mlipuko wa ugonjwa uliendelea.
Na walikufa watu wengi hadi elimu ya kutumia madawa kuwaosha wahanga ilipoanza kuenea, na ugonjwa kupungua.

That was in the 70s to 80s.
10 years kwa tabia hiyo ya ugonjwa ya mtu kuhara na kitapika Hadi kufa,watu pwani wangeisha wote...nasikia maji ya dafu yaliokoa jahazi
 
By that time, tulikuwa na pathologist wawili tuu!. Sisi tuliosoma Tambaza tulikuwa tunamuona sana mitaa ya around Muhimbili, alikuwa ni kichwa sana!,
Taarifa ya Familia
Wanajumuia,

Familia ya Professa James Shaba inasikitika kuwatangazia kuwa Mzee wetu Professa James Shaba amemaliza safari yake hapa duniani. Mzee wetu ametutoka jioni ya leo siku ya Jumanne tarehe 5 December 2023, muda wa saa 2:30 usiku saa za Marekani (Central Eastern Time) Chicago. Habari zaidi za maandalizi ya mazishi zitatumwa baadaye. Mzee alikuwa akiuguzwa na watoto wake Stella na Anale Shaba kwa muda mrefu. Mungu aipumzishe roho ya mzee wetu mahali pema peponi.

Kwa mtakawatoweza kuawasiliana au kwenda kuwaona Stella na Anale Shaba (Watoto wa Marehemu) na Wana Chicago wenzetu mnaweza kusailiana nao kwa kupitia namba ya simu hapo chini au kwenda kuwaona nyumbani kwao:

Anale Shaba: (847) 525-9224
4151 N. Richmond
Chicago, IL 60618

“Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.”

NB: Uongozi wa TCA tutaendelea kutoa updates.

ila pia...

RIP Prof. James Shaba.
P
By that time mimi nilikuwa Standard Four. Nilikuwa bado mvulana mbichi. Sasa nimekuwa babu nashinda na wajukuu zangu hapa nyumbani.

Itakuwa kweli alikuwa kichwa. Wamerekani hawawezi kumchukua daktari wa kiwango cha chini.

RIP Prof Shaba.
 
Duh huyu mzee inaonekana alikuwa mlevi tokea miaka ya 70 huko tena wa pombe kali sana maana anasemwa waziwazi. Najiuliza ikawaje aishi hadi leo 2020s. Kwa jinsi anavyosifiwa humu kwa kilaji basi alikuwa analewa kila siku tena chakariiiii...Najiuliza bado aliwezaje kudumu hivyo???
Na mimi nimejiuliza swali hili.

Inawezekana alipunguza au kuacha.

Kwa kasi ile ya miaka ya 1980s asingeweza kuishi miaka yote hii.

Mimi nilikuwa nafikiri alishafariki siku nyingi.

Sisi tuko wadogo miaka ya 1980s Professor Shaba alikuwa mzee tayari.
 
Dr Kasambala ni mjomba wangu toka kijijini.
1975 tumefanya kazi wote zahanati moja kati kati ya Jiji, Dr Kasambala akitokea Muhimbili.
Alikiwa mtu wa whiskey kwa sana.
Miaka hiyo uliingia ugonjwa wa Alto Cholera, ndugu yake na Cholera. Ugonjwa ulikuwa haujawahi kutokea Tanzania, na ulikuwa unatisha.
Mtu anaharisha na kutapika mfululizo hadi anakufa kwa kukosa maji mwilini.

Tukiwa tea break tukamuuliza, ugonjwa huu utaisha lini?
Dr Kasambala alijibu simply, "it is here to stay".

Ugonjwa huu ulileta tafaruki nchini hadi bungeni.
Kuna mbunge toka mikoa ya mwambao aliuliza kwa waziri wa Afya, wakati huo akiwa ni Dr Leader Stirling, mzungu toka Uingereza, "ugonjwa huu mbona uko mikoa ya pwani kwa wingi, na serikali haifanyi kitu"
Dr Stirling alimjibu, "ugonjwa huu unatokana na binadamu kula vyakula vilivyo changanyika na kinyesi chake mwenyewe"

Ikatokea valangati, watu wa pwani wakaona wametukanwa na mzungu, ati wanakula kinyesi.
Joto lilikuwa kubwa hadi Dr Stirling alijiuzulu.

Lakini kiukweli Dr Stirling alikuwa sahihi.

Watu wengi wa pwani walikuwa wanawaosha maiti wao waliokufa kwa cholera kwa mikono mitupu.
Vidudu vya echoli vikaingia kwenye kucha na mikono hivyo wakati wa kula mlipuko wa ugonjwa uliendelea.
Na walikufa watu wengi hadi elimu ya kutumia madawa kuwaosha wahanga ilipoanza kuenea, na ugonjwa kupungua.

That was in the 70s to 80s.
Asante mzee wangu , kuna kitu umenipa katika research yangu na ripoti yangu kuhusu jambo fulani huku Afya .

May God bless you

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu nilisha andika kitabu toka 2005, ila sijakitangaza sana kwa vile kinagusa maisha ya watu ambao bado wako hai.

Watu wanafikiri ufisadi umeanza sasa, ulikuwepo kitambo.
Duh!

Sasa unasubiri hadi hayo mafisadi yaondoke ndipo kitabu kichapishwe?
Kuna njia nyingi za kuwasilisha kitabu bila kujitambulisha mwenyewe waziwazi; na hasa siku hizi ndiyo imekuwa rahisi zaidi.
Na hata hivyo, kwa nini uyape heshima na hadhi kubwa hayo mafisadi yaliyovuruga matumaini ya waTanzania?
 
Rashid Mfaume Kawawa alikuwa waziri mkuu wa mwisho wa Tanganyika January 1962 mpk 9 December 1962.

Kuanzia 10 December 1962 mpk February 1972 nafasi ya waziri mkuu ilifutwa.

Mwaka 1972 February nafasi ya waziri mkuu ilirejeshwa na Rashid Mfaume Kawawa akawa waziri mkuu wa kwanza wa Tanzania mpk mwaka 1977.

Kawawa alifuatiwa na Sokoine
Asante.
Umelimaliza hili vizuri, na hao Habari Leo walipashwa kujua hivyo.
 
Alikuwa kichwa my foot!

Hakuchangia kukuza medani ya afya ndio maana wanapozeeka wanakimbia kutibiwa na kufia nje.

Angekuwa kichwa angefanya indelible good for his profession, for his country.

Always drunk like a skunk and smelling like a liqour still.
Aisee!
Watu type yako ni wachache hii Tanzania.

Truth never offend
 
Sisi tuko wadogo miaka ya 1980s Professor Shaba alikuwa mzee tayari.
No, actually he wasn't. Hardly 50 years by the time!

Atakuwa baadae alipunguza, la sivyo lile ini lisingehimiri muda wote huo. Kwenye ile picha inaonekana hata alikuwa kaongezeka uzito, tofauti na alivyokuwa Muhimbili.
 
50 years by 1984 kwa life expectancy ya Tanzania ni mzee.
 
Back
Top Bottom