TANZIA Professor James Shaba afariki dunia. Alifanyia postmortem mwili wa Hayati Sokoine

TANZIA Professor James Shaba afariki dunia. Alifanyia postmortem mwili wa Hayati Sokoine

Kumbe huyu mwamba alikuwa hai mimi nilijua alishavuta kitambo
Mkuu wewe kama mimi, hususan kwa kile kilaji alichokuwa anapiga miaka ile.

Ukimkuta huyo na Mwalimu Ndosi Center lazima ufurahi mwenyewe. Sasa wote wametutoka.

Ila tulikuwa tunampa udhuru kwamba kazi yake ni kucheza na maiti, hivyo lazima azingue akili kidogo kabla ya kuingia kazini.

RIP Prof. Shaba.
 
tulikuwa tunamuona sana mitaa ya around Muhimbili, alikuwa ni kichwa sana!,

Alikuwa kichwa my foot!

Hakuchangia kukuza medani ya afya ndio maana wanapozeeka wanakimbilia kutibiwa na kufia nje ya nchi.

Angekuwa kichwa angefanya indelible good for his profession, for his country.

Always drunk as a skunk and reeking like a liquor still.
 
Pamoja na yote postmortem ya Edward Moringe Sokoine hakuandikwa au kuwekwa wazi.

Na ndiyo maana wanae walipoamua kuhamisha mwili pale ulipozikwa ulisimamiwa na wabeba mtutu.

All in all asingewezza kupingana na Mwalimu
 
Alikuwepo pia dr sijui Prof yule kssambala naye alikuwa vzr na alikuwa mtu wa kinywaji pia
Alikuwa anaishi upanga pia

Ova
Dr Kasambala ni mjomba wangu toka kijijini.
1975 tumefanya kazi wote zahanati moja kati kati ya Jiji, Dr Kasambala akitokea Muhimbili.
Alikiwa mtu wa whiskey kwa sana.
Miaka hiyo uliingia ugonjwa wa Alto Cholera, ndugu yake na Cholera. Ugonjwa ulikuwa haujawahi kutokea Tanzania, na ulikuwa unatisha.
Mtu anaharisha na kutapika mfululizo hadi anakufa kwa kukosa maji mwilini.

Tukiwa tea break tukamuuliza, ugonjwa huu utaisha lini?
Dr Kasambala alijibu simply, "it is here to stay".

Ugonjwa huu ulileta tafaruki nchini hadi bungeni.
Kuna mbunge toka mikoa ya mwambao aliuliza kwa waziri wa Afya, wakati huo akiwa ni Dr Leader Stirling, mzungu toka Uingereza, "ugonjwa huu mbona uko mikoa ya pwani kwa wingi, na serikali haifanyi kitu"
Dr Stirling alimjibu, "ugonjwa huu unatokana na binadamu kula vyakula vilivyo changanyika na kinyesi chake mwenyewe"

Ikatokea valangati, watu wa pwani wakaona wametukanwa na mzungu, ati wanakula kinyesi.
Joto lilikuwa kubwa hadi Dr Stirling alijiuzulu.

Lakini kiukweli Dr Stirling alikuwa sahihi.

Watu wengi wa pwani walikuwa wanawaosha maiti wao waliokufa kwa cholera kwa mikono mitupu.
Vidudu vya echoli na/au vibrio cholera vikaingia kwenye kucha na mikono hivyo wakati wa kula mlipuko wa ugonjwa uliendelea.
Na walikufa watu wengi hadi elimu ya kutumia madawa kuwaosha wahanga ilipoanza kuenea, na ugonjwa kupungua.

That was in the 70s to 80s.
 
Kumbe huyu mwamba alikuwa hai mimi nilijua alishavuta kitambo
Tofauti kidogo na wewe, katika "kujuwa", taarifa hii imenifanya nami nidhani kuwa alisha ondoka, kumbe alikuwa yungali hai!

Jambo linalosikitisha na taarifa za namna hii ni kwamba, mtaalam kama huyu, 'pioneer' wa eneo lake la kitaaluma, taarifa ya kifo chake inahusishwa na umaarufu wake katika kumhudumia kiongozi tu, tena kwa kiongozi aliyeaga dunia!

Kuna njia nyingi za kumuelezea Profesa Shaba zikihusisha umaarufu wake kikazi na kulitumikia taifa lake kiujumla.

Hii inaonyesha tabia ya siku hizi inayowapa viongozi wa kisiasa kipaumbele katika kila jambo, na kusahau michango ya waTanzania mbalimbali katika kazi zao maeneo mbalimbali.

Sasa sijui kama hii nimeiweka sawa, kama nilivyotaka kuiwasilisha.

Nilimfahamu Profesa Shaba Muhimbili. Hakuwa na nenobaya na mtu yeyote.
Mungu Amweke Mahali Pema.
 
Tha
Dr Kasambala ni mjomba wangu toka kijijini.
1975 tumefanya kazi wote zahanati moja kati kati ya Jiji, Dr Kasambala akitokea Muhimbili.
Alikiwa mtu wa whiskey kwa sana.
Miaja hiyo uliingia ugonjwa wa Alto Cholera, ndugu yake na Cholera. Ugonjwa ulikuwa haujawahi kutokea Tanzania.

Tukiwa tea break tukamuuliza, ugonjwa huu utaisha lini?
Dr Kasambala alijibu simply, "it is here to stay".
Ugonjwa huu ulileta tafaruki nchini hadi bungeni.
Kuna mbunge toka mikoa ya mwambso aliuliza kwa waziri wa Afya, wakati huo ni Dr Leader Stirling, "ugonjwa huu mbona uko mikoa ya pwani kwa wingi, na serikali haifanyi kitu"
Dr Stirling alimjibu, "ugonjwa huu unatokana na binadamu kula vyakula vilivyo changanyika na kinyesi chake mwenyewe"

Ikatokea valangati, watu wa pwani wakaona wametukanwa ati wanakula kinyesi.
Joto lilikuwa kubwa hadi Dr Stirling alijiuzulu.

Lakini kiukweli Dr Stirling alikuwa sahihi.Watu wengi wa pwani walikuwa wanawaosha maiti wao waliokufa kwa cholera kwa mikono mitupu.
Vidudu vya echoli vikaingia kwenye kucha na mikono hivyo wakati wa kula mlipuko wa ugonjwa uliendelea.
Na walikufa watu wengi hadi elimu ya kutumia madawa kuwaosha wahanga ilipoanza kuenea, na ugonjwa kupungua.

That was in 1975.
Thank old person, a very interesting story that shows where we came from
 
Back
Top Bottom