Professor Nabi anza na kikosi hiki kwenye mechi ya marudio dhidi ya Marumo Gallants

Professor Nabi anza na kikosi hiki kwenye mechi ya marudio dhidi ya Marumo Gallants

1. Diarra
2. Dickson Job
3. Kibwana Shomari (umkumbushe huyu kijana wako! Mechi iliyopita alikuwa anajisahau sana)
4. Ibrahimu Abdallah (Bacca)
5. Bakary Mwamnyeto
6. Khalid Aucho
7. Abubakary Salum (Sure Boy).
8. Mudathir Yahaya Abbas
9. Fiston Kalala Mayele.
10. Stephano Aziz Kii
11. Farid Mussa Malick.

Sub: Metacha Mnata, Joyce Lomalisa, Juma Shaban, Kennedy Mudonda, Clement Mzize, Tuisila Kisinda, Jesus Moloko, na Yannick Bangala Litombo.

Hiki kikosi kitaisaidia timu kwenye umiliki wa mpira, kuzuia mashabulizi ya Marumo, na pia kwenye counter attack.

Chonde chonde Profesa!!
Moloko na Kisinda wasianze. Maana hawa jamaa siyo wazuri kwenye kumiliki mpira. Wao ni wazee wa mbio tu. Hivyo waingie kipindi cha pili.
Umejipa kazi ya kumfundisha samaki kuogelea.
 
Niwakumbushe tu, Nabi alishasema hatakagi kupangiwa timu na mashabiki! Kwa hiyo tumpe nafasi Professa Nabi. Mimi vyovyote atakavyopangwa sawa tu!
 
Mauya wa sasa hivi amebadilika sana
Mauya kabadilika toka siku nabi amewafokea mauya, ambundo na ngushi kuwa hawaongezeki viwango....kweli timu apange kawaida then tuwe na morali na mbinu ya kushinda kuliko kuzuia....lkn ni muhimu tuwaheshimu gallants na first half tuhakikishe hawapati goal. Me naamini mayele atafunga km tukicheza kawaida bila kupack bus lkn nidhamu iwe juu sana...amini
 
Mleta mada, nafkiri Joyce Lomalisa anaweza akaanza game hii. Namuona yupo vizuri zaidi kwa kila eneo kuliko Kibwana.

Tunategemea Yanga kutumia Counter attacts zaidi hapo kesho. Counter unahitaji watu wenye accuracy ya pass, wanaoweza kujiposition ktk eneo la hatari, wanaojua kukimbia na kudribble mpira vizuri.

Katika hili eneo, Tuisila na Moloko walau wameonesha wana huo uwezo. Timu ikiwa inamiliki mpira ndipo wanapoharibu.

Bangala amekuwa na upepo fulani hivi mbaya ktk siku za karibuni. Pengine akitokea bench anaweza akaleta mabadiliko hiyo second half.
 
KAMA NINGEKUWA KOCHA WA YANGA.

1. Digui Diara.
2. Dickson Job.
3. Joyce lomalisa.
4. Ibrahim Baka.
5. Bakari Nondo.
6. Yanic Bangara.
7. Juma shaban.
8. Khalid Aucho.
9. Fiston Mayele.
10. Mudadhiri yahaya.
11. Kibwana Shomari.
Ondoa kibwana weka Musonda. Musonda anaweza akarud kukaba nyuma na Lomalisa.

Hapo kwa Djuma shaban sio kwamba kwenye mipira ya Counter atazingua huyu maana sio winga.
 
KAMA NINGEKUWA KOCHA WA YANGA.

1. Digui Diara.
2. Dickson Job.
3. Joyce lomalisa.
4. Ibrahim Baka.
5. Bakari Nondo.
6. Yanic Bangara.
7. Juma shaban.
8. Khalid Aucho.
9. Fiston Mayele.
10. Mudadhiri yahaya.
11. Kibwana Shomari.
Nimekielewa Sana kikosi chako
 
Hapo nabi kipindi cha kwanza aende na mfumo wa 3-5- 2 , mabeki watatu job, nondo na baka

Hapo kwenye wachezaji watano Lomalisa na djuma wawe kulia na kushoto kama wingback na wahimizwe kupanda na kushuka kwa wakati alafu mudathiri,aucho na sure boy kati

Mbele hapo hao wawili waanze musonda na mayele ila hapa nabi anatakiwa amtumie musonda kama striker wa mwisho na mayele awe nyuma ya musonda tukiwa tunamiliki mpira na tukiwa hatuna mpira wawe wana press kwa nguvu wote wawili kuanzia kwenye box la adui. Kutoka na kasi ya mayele na uwezo wa kumiliki mechi nabi anapaswa kumuhiz mayele kutoa pasi haraka kwa musonda.

Mechi hii mayele awe nyuma ya mshambiaji wa mwsho na ahimizwe acheze kama kiungo mshambuliaji.

Tukicheza hivi tuna shinda huko huko kwa madiba
 
Back
Top Bottom