Professor Nabi anza na kikosi hiki kwenye mechi ya marudio dhidi ya Marumo Gallants

Professor Nabi anza na kikosi hiki kwenye mechi ya marudio dhidi ya Marumo Gallants

Hiyo game kama KISINDA hatoanza hatutoshinda.

Pamoja na mapungufu yake, ila Kisinda ana stamina na Speed huwezi linganisha na FARID MUSSA.

Kisinda ni muhimu kwa game zinazohitaji Counter attack, Kisinda ana ability kubwa ya kupiga chenga kuliko Moloko na Faridi.

Kisinda ana nguvu za kupiga hata nje ya Box.

Kwenye game muhimu Kisinda ametusaidia sana msimu huu, zile game tulizohitaji matokeo zaidi.
Nimemaanisha kipindi cha kwanza aanzishe walinzi na viungo wengi kwa lengo la kudhibiti mashambulizi ya Marumo Gallants kutokea eneo la kati na pembeni (hao jamaa ni bora sana katika maeneo hayo! Na ushahidi ni kwenye mechi iliyopita. Kiufupi kipindi cha kwanza pale kwa Mkapa, hali ilikuwa ni tete).

Kwa bahati mbaya akina Kisinda na Moloko ni viungo washambuliaji zaidi. Hivyo katikati pasipokuwepo na viungo wengi, timu itaruhusu mashambulizi na pia magoli. Halafu wakishadhibitiwa, ndipo kipindi cha pilo waingie sasa kwa ajili ya kumaliza mchezo.
 
Dah! Naona umeamua kunisagia kunguni. Kwenye ile mechi ukiondoa lile goli alilofunga, ni ukweli uliowazi Aziz Kii hakuwa na mchezo mzuri. Alipoteza pasi nyingi!! Na hakuendana kabisa na kasi ya mchezo kutoka kwa wapinzani.

Usisahau wakati anafunga lile goli, tayari alikuwa kwenye mpango wa mwalimu wa kumpumzisha. Maana alitolewa dakika chache tu baadaye.
Kumbe kama angetolewa mapema kama ulivyotaka inawezekana lile goli lisingepatikana, bado nakuona una kiburi sana kumfundisha kocha nini cha kufanya..
 
Kumbe kama angetolewa mapema kama ulivyotaka inawezekana lile goli lisingepatikana, bado nakuona una kiburi sana kumfundisha kocha nini cha kufanya..
Haya ni maoni yangu tu mkurugenzi nikiwa kama kocha mstaafu. Hayo mamlaka ya kumfundisha kocha nini cha kufanya nayatoa wapi? Kwanza nina uhakika hata jamii forums yenyewe haijui.
 
Kikosi
IMG_20230517_181158.jpg
 
1. Diarra
2. Dickson Job
3. Kibwana Shomari (umkumbushe huyu kijana wako! Mechi iliyopita alikuwa anajisahau sana)
4. Ibrahimu Abdallah (Bacca)
5. Bakary Mwamnyeto
6. Khalid Aucho
7. Abubakary Salum (Sure Boy).
8. Mudathir Yahaya Abbas
9. Fiston Kalala Mayele.
10. Stephano Aziz Kii
11. Farid Mussa Malick.

Sub: Metacha Mnata, Joyce Lomalisa, Juma Shaban, Kennedy Mudonda, Clement Mzize, Tuisila Kisinda, Jesus Moloko, na Yannick Bangala Litombo.

Hiki kikosi kitaisaidia timu kwenye umiliki wa mpira, kuzuia mashabulizi ya Marumo, na pia kwenye counter attack.

Chonde chonde Profesa!!
Moloko na Kisinda wasianze. Maana hawa jamaa siyo wazuri kwenye kumiliki mpira. Wao ni wazee wa mbio tu. Hivyo waingie kipindi cha pili.

Professor anajua anachokifanya
 
Back
Top Bottom