Profit ni kitu muhimu sana kwenye kuamua biashara ya kufanya, ukiwa na mtaji mdogo epukana na biashara zenye faida chini ya 10%

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Hii inawhusu zaidi ambao huiga biashara bila kutafakari kwa kina,

Ni muhimu sana kufuatilia asilimia ya profitability

Huwezi kuwa na mtaji wa milioni 1 uanze kufanya biashara yenye faida ya 5%

Utachelewa sana
 
Profit ya 10% kwa hiyo 1M uliyotaja hufiki popote unafunga virago unatafuta kibarua kubeba zege.

Labda iwe na profit ndogo ila mzunguko mkubwa, kwamba unaweka 1M baada ya wiki mbili hiyo hela yote inakuwa imezalisha faida ya 100k kisha unaendelea kuzungusha faida.
Unajikuta 100k kwa wiki mbili, kwa mwezi 200k. Kwa miezi 6 ni 1.2M faida ukitoa kodi labda 50k kwa mwezi ni 300k unabaki na 900k. Utoe umeme miezi yote 6, matumizi ya biashara sijui nauli kufuata kitu gani. So biashara yako inakuwa na ongezeko la kama 500k kwenye mtaji baada ya miezi 6.

Hapo usitegemee biashara kula, kuhonga, kupanga, kutuma kwa wazazi, kupendeza unaacha we unavaa kujistiri tu.
 
Kwangu Mimi mzunguko Mkubwa wa 5 % ni bora zaidi kuliko Mzunguko Mdogo wa 10 % !!!
Hata uwe na mzunguko mkubwa kiasi gani, mtaji mdogo na faida ni 5% unaishia kusifiwa na kuitwa majina uchwara ya Mgosi sijui Mzigua na huendelei.

Unakuwa na wateja njaa wasio na shukrani kukuhama ni kama kunywa maji, huwezi innovate, ukipigwa hasara moja ndogo tu unafunga unaenda kuhesabu maumivu kijijini kwenu.

Ukifanya biashara ukawazoesha wateja bei ndogo unaingia kwenye mtego mbaya unakuwa punda. Utafirisika uwaache wanaouza na reasonable price waishi. Sijawahi ona mtu anayeuza bei kubwa akifirisika, ila nimeshuhudia mavunjabei wakiishiwa upepo.
 
Je mwenye Mtaji Mdogo kama wa 1 M , auze kwa faida ya asilimia ngapi ?
. Kwa Maoni yako
Hata uwe na mzunguko mkubwa kiasi gani, mtaji mdogo na faida ni 5% unaishia kusifiwa na kuitwa majina uchwara ya Mgosi sijui Mzigua na huendelei.

Unakuwa na wateja njaa wasio na shukrani kukuhama ni kama kunywa maji, huwezi innovate, ukipigwa hasara moja ndogo tu unafunga unaenda kuhesabu maumivu kijijini kwenu.

Ukifanya biashara ukawazoesha wateja bei ndogo unaingia kwenye mtego mbaya unakuwa punda. Utafirisika uwaache wanaouza na reasonable price waishi. Sijawahi ona mtu anayeuza bei kubwa akifirisika, ila nimeshuhudia mavunjabei wakiishiwa upepo.
 
Inategemea hiyo asilimia kumi au Tano ya mtaji unaipata Kwa muda gani na mtaji ni kiasi gani. Kama umetia 1m Kwa week ukapata return milioni Moja na laki Moja sio mbaya.
 
Alichokisema mleta mada ni ukweli mtupu,wengi wameteketeza mitaji Kwa sifa za kujidai wanauza bei nzuri au wanajali mzunguko,tukumbushane tu kuwa biashara ni ubepali,msilete ujamaa kwenye mambo ya kibepari,vinginevyo uwe na viwanda kwamba unachouza unakizalisha Kwa bei ndogo sana
 
Hii inawhusu zaidi ambao huiga biashara bila kutafakari kwa kina,

Ni muhimu sana kufuatilia asilimia ya profitability

Huwezi kuwa na mtaji wa milioni 1 uanze kufanya biashara yenye faida ya 5%

Utachelewa sana
Labda tuiweke kwa kiingereza
Una maanisha Net profit au gross profit!??
 
Uncle bright unamaanisha 10% ya profit ukishatoa gharama za uendeshaji au just bidhaa.

Mfano nanunua bidhaa x kwa bei ya jumla ya Tsh 10,000 hafu naiuza Tsh 12,000 inamaanisha nna faida ya Tsh 2,000 ambayo ni 20% ya faida.

Sasa gharama za uendeshaji mfano fremu, umeme, usafi, kodi TRA & manispaa, kumlipa kijana wa dukani, nk nazihesabu au?

Ni muhanga wa hizi kitu, nimetoka kufunga duka June 2024 nataka nirudi Nov - December.
 
Ukinunua bidhaa X kwa bei ya jumla 10k, bei ya rejareja uza sio chini ya 15,000 kama ni bidhaa isiyotoka sana. Kinachoua biashara isiyotoka ni bidhaa kukaa stock, unaweka 1M alafu zinatoka mpaka zinaisha ni miezi minne. Hapo ukijumlisha bidhaa nyingine unakuta jumla ya duka labda 5M alafu almost ni 1M pekee inayotoka kwa mwezi, so una faida ya 400k monthly. Sasa hapo ulipe kodi ya pango maybe 100k, ule, uishi, upate hasara ufidie humohumo, ukuze mtaji. Ndio hapo mwaka ukiisha lazima ufunge.

Wauza nguo za mitumba kali hununua kwa @ 5,000 bei ya jumla mfano belo na kuuza @ 15,000 wastani. Watengeneza furniture zile nzurinzuri hutumia gharama za kila kitu labda 70k na kuuza bidhaa 100k hapo amekasirika umempa hela ndogo.

Kama bidhaa ina bei kubwa ya kununua mfano unanunua gari nje 16M ndio unauza around 19M, huwezi sema natafuta 40% profit. Mtaji mkubwa una changamoto chache na hela ya mauzo huonekana ila mtaji mdogo huwezi amini unakuta unaingiza hela ila 1000 ya juisi kwa siku kumbe inaharibu mahesabu pakubwa.

Ukienda
 
Uncle bright unamaanisha 10% ya profit ukishatoa gharama za uendeshaji au just bidhaa.

Mfano nanunua bidhaa x kwa bei ya jumla ya Tsh 10,000 hafu naiuza Tsh 12,000 inamaanisha nna faida ya Tsh 2,000 ambayo ni 20% ya faida.

Sasa gharama za uendeshaji mfano fremu, umeme, usafi, kodi TRA & manispaa, kumlipa kijana wa dukani, nk nazihesabu au?

Ni muhanga wa hizi kitu, nimetoka kufunga duka June 2024 nataka nirudi Nov - December.
profit ya kwenye bidhaa

mfano bidhaa unyojumua kwa elf 10 uuze kwa faida isiyozidi buku
 
Biashara Bongo ni pasua kichwa, watu wengi sifikirii kama wapo serious kabisa, yani mtu anatafuta faida kwenye bidhaa chini ya 10% nashindwa kuelewa malengo yake ni nini
 
Back
Top Bottom