Right on bro.. it is and strange enough would work right.
Mkuu wangu msome Shalom kisha fikiria nje ya box utanielewa. Ninajua mna makusudio mazuri sana lakini kama mtakavyoanza ni muhimu kuzingatia WATU wenyewe na katika MAZINGIRA yapi.. sasa hivi wananchi wote wanalia SOS, wanahitaji Nabii wa kuwaokoa kama alivyofanya Mussa. Baada ya kuwavusha toka hatarini ndipo alipowapa sheria za Amri 10. Ndicho nachokishauri.
Amini maneno yangu na mfikirie sana what is at stake right now, Swala la UONGOZI BORA ni muhimu kuliko mengine yote na hatuwezi kufanikisha hivyo pasipo kutumia njia ambazo wengi hawazioni umuhimu wake.
Kama nilivyosema hapo mwanzo UONGOZI BORA ni swala la Dharura, kama ilivyo Umeme na kuanzishwa kwa PPPT ni suluhisho la muda mrefu ambalo pia wananchi wanalisubiri. Right now mfanye kama ya Yesu kuwapa watu mkate na mvinyo kisha wafundisheni Gospel..akili zao haziwezi kufanya kazi wakiwa na njaa, machungu na adha isokuwa na kifani.
Kwa nini sikuwaomba mjiunge na CCM ni kwa sababu chama hicho ni sawa na Dowans, pamoja na dharura tulokuwa nayo hatuwezi kuchukua madudu ya CCM na kutegema vinginevyo, na hata kama mtaweza leta mabadiliko ndani ya CCM gharama yake kwa wananchi itakuwa kubwa sana. CCM itabadilishwa na viongozi wake wenyewe. Nimemsoma Rev. Kishoka na kila naposoma inanipa sura ya kwamba, PPPT haitegemei wala kupania Ushindi mwaka 2010. Wananchi can't wait that long, amini maneno yangu wakuu zangu.
Wekeni nguvu zetu kwa vitu vilivyopo kwani huwezi kuishinda CCM mkiwa mmegawanyika na hata siku moja msifikirie kuwafikia watu vijijini ni kazi ndogo. Ni kazi kubwa sana kuliko kukitangaza chama mjini kama ulivyo usafiri wetu. safari ya kwenda Ukerewe ni lazima ukatambikie kwanza na hujui utafika lini ndivyo habari za ujio wa PPPT utakavyochukua muda.
Sizungumzi hivi kwa sababu mimi ni mwana Chadema au nimetumwa na mtu yeyote isipokuwa ni mawazo yangu huru baada ya kuchanganua matatizo yetu na ipi njia rahisi ya kuyaondoa.. Hata hivyo shukran mkuu wangu kwa kunisoma.
N.B - Au tufanye hivi nipandisheni chat na mimi basi, kuwa Mkandara kaweza kuwavuta Wapiganaji toka ndani na nje kuja kuliokoa taifa! haa haaa haaa!
Bob Mkandara,
Mwaka 1992, Tanzania iliachana na mambo makubwa mawili. Mfumo wa Kijamaa na mfumo wa Chama Kimoja.
Watanzania tulishangilia kwa nderemo, lakini hatukujua wala kuelewa tulichokuwa tunakishangilia.
Mwaka 1995, tukafanya uchaguzi mkuu wa kwanza wa Vyama vingi, tukafuatilia tena mwaka 2000 na tukarudia tena mwaka 2005 na sasa tunajianda kwa mwaka 2010.
Kati ya mwaka 1992 hadi leo tumefanya chaguzi si chini ya tatu za Serikali za mitaa, chaguzi mdogo si chini ya 20 kwa ajili ya nafasi za ubunge ambazo ili kuwa ni kuziba mapengo kutokana na kesi kufuta matokeo au mauti kufikia Wabunge.
Sasa katika miaka yote hii, kumekuwa na Vyama si chini ya 10 vya Upinzani ambavyo vilikuja na kudai kuwa kuwa lengo lao ni kuking'oa CCM kutoka madarakani.
Lakini tofauti kubwa, hadi leo hii ukiviuliza vyama hivi vimefanya nini kuleta maendeleo ama kama vyama au kupitia wawakilishi wao Bungeni ili vipate uhalali na kukubalika kuwa vina uwezo wa kuongoza Tanzania na si kubahatisha, hakuna hata chama kimoja ambacho kitaorodhesha hata vitu vitatu!
Tatizo lao ni wote mpaka leo wanaamini kuwa ni lazima Waingie Ikulu kwanza au wapate viti vya kutosha bungeni, ndipo waanze kufanya kazi yao ya kuleta maendeleo. Kwa kifupi, nao wanakimbilia kugombea madaraka.
PPPT haikimbilii madaraka au kutaka kuongoza kwa mara moja au katika siku saba. PPPT kinataa kijijenge na si mijini bali ni vijijini, mikoani, mitaani na kujijenga kwa PPPT kutafanyika kwa kuishi na wananchi na kushirikiana nao katika kuwafundisha elimu ya Uraia, kuwafundisha mbinu bora za uzalishaji mali, kuwafafanulia umuhimu wa kuwa na uwezo wa kujitegemea na zaidi kuwa na Uhuru wa kujiamulia mambo, wa kuchagua na kudai uwajibikaji, bila hofu ya kudhulumiwa, kunyanyaswa au kutishiwa na dola au mbaya zaidi kunyimwa kwa makusudi nafasi ya kupiga hatua za maendeleo (mfano wa mkoa wa Kilimanjaro kutengwa na CCM kwa ajili ya kuchagua Upinzani na si CCM).
Ni kweli Tanzania inahitaji mabadiliko ya haraka ya uongozi, na hili si la kukataa au kulifumbia macho, lakini hilo ni lengo la muda mfupi (short term) na hatari yake ni kutumia mabua kuziba ufa kwenye msingi, ambapo kuna mchwa na wadudu wengine ambao watatafuna yale mabua na kuacha ule ufa ukiwa vile vile haujazibika na unaendelea kupanuka.
Kwa sasa hivi kila mmoja wetu anajaribu kutoa elimu ya maendeleo na kupigia kelele Uhujumu na kudai Uongozi Bora, lakini bado tupo katika mfumo ule ule, tuna watu wale wale na mbaya zaidi, kila chama kilichopo hata chama Tawala vina matatizo ya kifikra ndani ya uongozi na ndio maana kuna migongano kila siku.
Badala ya kuungana nao au kujiunga nao, sisi tunaamua kufanya kazi yetu kwa utofauti na kwa mtazamo mwingine.
Hatutaki kufanya makosa ya Mrema, CHADEMA, NCCR, Mtikila, UDP au CUF na zaidi ya CCM ya sasa katika kujenga Demokrasia, Uongozi bora na kuijenga upya Tanzania iwe ni kisiasa, kijamii au kiuchumi.
Ndio maana tutaomba radhi kwako na wengine wanaotaka tujiunge na CHADEMA, CUF au CCM!