Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa Reverend, huyo member namba 1 mbona ana majibu ya kiswahili swahili, kila kitu anakurushia wewe usawazishe? lol.
Mimi naomba kadi namba ya mwisho, na ningeomba nipate nafasi nigombee ubunge kupitia PPPT katika jimbo la Nyamagana au Mwanza mjini. I just wanna grab the bull by its cojones!
Kuhusu kusimikwa kwa jadi, masharti nimeambiwa nipeleke ngozi (bila tone la damu) of 69 virgin gay mosquitoes with mateges (preferably wawe na kigugumizi) kutoka mto wa Mbu.
Nyana'eebe!
Ngoja niulize hivi mtu aliyeikimbia nyumba yake na kwenda kuhamia nyumba ya mwenzake eti kwa sababu mwenzie alikuwa na uwezo wa kuthubutu na kufanya maamuzi sahihi na kuijenga nyumba yake anakuwa na uwezo wa kurudi kwa mbwembwe?
Nyie wazamiaji kwa sababu mbali mbali ebu acheni kutusanifu jamani badala yake muendelee kumshukuru Mungu kwa kuwapa nafasi ya kufaidi maamuzi ya watu wengine. Sisi wenzenu ambao tuna uwezo wa kuzamia kama nyinyi na kuwa huko lakini tumechagua kubaki na kupigana humu hatuitaji hizo kejeli zenu.
Kwa kweli laiti kama mngejua maisha yetu yakoje kwa sasa huku mtaani nadhani huu utani usinge pewa nafasi
Right on bro.. it is and strange enough would work right.
Mkuu wangu msome Shalom kisha fikiria nje ya box utanielewa. Ninajua mna makusudio mazuri sana lakini kama mtakavyoanza ni muhimu kuzingatia WATU wenyewe na katika MAZINGIRA yapi.. sasa hivi wananchi wote wanalia SOS, wanahitaji Nabii wa kuwaokoa kama alivyofanya Mussa. Baada ya kuwavusha toka hatarini ndipo alipowapa sheria za Amri 10. Ndicho nachokishauri.
Amini maneno yangu na mfikirie sana what is at stake right now, Swala la UONGOZI BORA ni muhimu kuliko mengine yote na hatuwezi kufanikisha hivyo pasipo kutumia njia ambazo wengi hawazioni umuhimu wake.
Kama nilivyosema hapo mwanzo UONGOZI BORA ni swala la Dharura, kama ilivyo Umeme na kuanzishwa kwa PPPT ni suluhisho la muda mrefu ambalo pia wananchi wanalisubiri. Right now mfanye kama ya Yesu kuwapa watu mkate na mvinyo kisha wafundisheni Gospel..akili zao haziwezi kufanya kazi wakiwa na njaa, machungu na adha isokuwa na kifani.
Kwa nini sikuwaomba mjiunge na CCM ni kwa sababu chama hicho ni sawa na Dowans, pamoja na dharura tulokuwa nayo hatuwezi kuchukua madudu ya CCM na kutegema vinginevyo, na hata kama mtaweza leta mabadiliko ndani ya CCM gharama yake kwa wananchi itakuwa kubwa sana. CCM itabadilishwa na viongozi wake wenyewe. Nimemsoma Rev. Kishoka na kila naposoma inanipa sura ya kwamba, PPPT haitegemei wala kupania Ushindi mwaka 2010. Wananchi can't wait that long, amini maneno yangu wakuu zangu.
Wekeni nguvu zetu kwa vitu vilivyopo kwani huwezi kuishinda CCM mkiwa mmegawanyika na hata siku moja msifikirie kuwafikia watu vijijini ni kazi ndogo. Ni kazi kubwa sana kuliko kukitangaza chama mjini kama ulivyo usafiri wetu. safari ya kwenda Ukerewe ni lazima ukatambikie kwanza na hujui utafika lini ndivyo habari za ujio wa PPPT utakavyochukua muda.
Sizungumzi hivi kwa sababu mimi ni mwana Chadema au nimetumwa na mtu yeyote isipokuwa ni mawazo yangu huru baada ya kuchanganua matatizo yetu na ipi njia rahisi ya kuyaondoa.. Hata hivyo shukran mkuu wangu kwa kunisoma.
N.B - Au tufanye hivi nipandisheni chat na mimi basi, kuwa Mkandara kaweza kuwavuta Wapiganaji toka ndani na nje kuja kuliokoa taifa! haa haaa haaa!
Sasa Reverend, huyo member namba 1 mbona ana majibu ya kiswahili swahili, kila kitu anakurushia wewe usawazishe? lol.
Mimi naomba kadi namba ya mwisho, na ningeomba nipate nafasi nigombee ubunge kupitia PPPT katika jimbo la Nyamagana au Mwanza mjini. I just wanna grab the bull by its cojones!
Kuhusu kusimikwa kwa jadi, masharti nimeambiwa nipeleke ngozi (bila tone la damu) of 69 virgin gay mosquitoes with mateges (preferably wawe na kigugumizi) kutoka mto wa Mbu.
Rev. Kishoka, Mkuu wanenoi mazito sana...duh kama namwona Che vile!
Aaaah ndugu yangu Dunia yenyewe inakwisha December 2012 kulingana na utabiri wa Nostradamus!Mkandara:
Naona wanamapinduzi mmekutana. Mimi nawachungulia tu wala mguu sitihi.
Mkandara:
Naona wanamapinduzi mmekutana. Mimi nawachungulia tu wala mguu sitihi.
Zakumi,
Usihofu, kadi yako nambari 11, tunakuhitaji na uzoefu wako wa masuala ya Biashara na Uchumi!
Hili la PPPT si mambo ya Ujamaa hivyo usitie shaka!
Aaaah ndugu yangu Dunia yenyewe inakwisha December 2012 kulingana na utabiri wa Nostradamus!
Halafu basi ndio nipo ktk 10 la mwisho unajua tena life expectancy ya mtu mweusi..Mimi ni mtia maji tu, kama yule Yohana Mbatizaji pengine Rev. anaweza kunifufua kifira.
Mkandara:
Naona wanamapinduzi mmekutana. Mimi nawachungulia tu wala mguu sitihi.
Duh, hii kali sana mkuu wangu yaani umetoa hukumu pasipo hata kuskia kesi yenyewe!Hivyo kabla ya kujiunga, ningependa kujua muundo wa hicho chama. Kama kutakuwepo kamati kuu, Halmashauri kuu, please count me out
Rev. Kishoka:
Nimeona kuna kitu kimoja kikubwa ambacho tumerithishwa bila kufahamu.
Miundo ya taasisi nyingi za kijumuia na kisiasa zina katiba inayofanana na CCM, Simba na Yanga.
Na hata kama watakuwa na tofauti kidogo ya kimuundo, ki-mentality watafanya kazi kwa kutumia muundo wa CCM. Kutakuwepo na mwenyekiti au president. Katibu. Katibu mwenyezi. Kamati ya nidhamu. Na vitu kama hivyo.
Hivyo kabla ya kujiunga, ningependa kujua muundo wa hicho chama. Kama kutakuwepo kamati kuu, Halmashauri kuu, please count me out.
Zakumi,
Halmashauri na Kamati kuu za nini? kupikana majungu na kuoneana haya kama yanayotokea CCM na CHADEMA?
Shalom,
Kwanza namshukuru Mungu aliyenipa nafasi na ujasiri wa kuondoka nyumbani na kwenda Ugenini Ughaibuni, mbali na jamaa na nyumbani na kwa nafasi hiyo, nimejifunza mengi kutokana na mazuri ya maamuzi ya hawa watu wengine au majirani.
Sisi si wakimbizi au wazamiaji. Tuliondoka kwa hiari na tunaishi kwa hiari yetu na ni kutokana na na kuwa na hiari ya kujifunza yaliyo bora kwa majirani na huku ughaibuni, ndio maana tunapatwa na msukumo wa kuleta mabadiliko ambayo yanamjali Mtanzania na kumpa nafasi ya kufurahia Utanzania wake na kuishi maisha bora.
Hatuna maana ya kutaka kujenga majengo ya ghorofa na ya vioo eti tufanane na Ughaibuni. Tunachotaka kuleta Tanzania ni kitu ambacho Babu na Baba zetu na hata Kaka zetu wakubwa waekijaribu kwa muda lakini wamekuwa wakipata shida kufanikiwa kutokana na kuingiliwa na majaribu na kukosa kutuumia vizuri upeo waliopewa na nafasi za kuishi huko Ughaibuni kuelewa mfumo wa maisha na kiuchumi achilia mbali wa kisiasa.
Kauli zako zinaonyesha umeridhika na maisha yako, ikiwa na maana ama ni masikini wa kutupa ambaye umeshakata tamaa kama sivyo, basi wewe ni mmoja wa wale wachache waliobaatika kuendelea "ku-neemeka" na kujaliwa na "neema" ilhali wengi hawana hata uwezo wa kujua kesho itafika namna gani.
Ni kutokana na Taswira yako kuwa ama ya mtu aliye Fukara au Tajiri asiyejali jirani yake anavyoishi, ndio maana sisi tunaungana na kusema, Tanzania inaweza kuwa kisiwa cha maendeleo nakuondokana na Ufukara na Utajiri wa kuvimbiwa ambao umejaa dhuluma.
Hivyo basi, usituonee wivu kwa sisi kuamua kuleta mapinduzi ya kuondoa Ufukara na kumpa mtu Uhuru wa haki na utu kwa kuwa wewe uliye tajiri na kuwanyonya wengine wote na kuwanyima haki zao, unataka kuendelea kunenepeana kama kupe au minyoo.
Kama tungekuwa hatuna uchungu na uzalendo kwa nchi yetu, tusingepoteza muda kujadili hatima ya Tanzania yetu na Watanzania. Tungefurahia sana masufuria ya Pharao ughaibuni na kuwasahau mbakie na dhuluma na ufukara wenu!
Sikonge,
Kuhusu maadili au ni nani awe mwanachama, tutaangalia kwa undani kuwa ni mtu wa namna gani anayekuja jiunga na chama chetu.
Mkandara,
Kwanza umeuliza kwa nini tusijiunge CHADEMA, pili ukaongezea kwa kuuliza kwa ni ntusijiunge na Chama kingine na kuleta mabadiliko ikiwa suala ni Uongozi Bora.
CCM, CHADEMA, CUF, TLP, NCCR, UDP, na wengine, tayari wana Sera zao, Itikadi zao na Katiba zao ambazo zimeundwa kukidhi nia ya Waliounda vyama hivyo.
Sisi tunaunda Chama chetu, chenye Itikadi, Sera na Katiba ambayo ni tofauti na hivyo vyama vingine.
Lengo si kukimbilia Uchaguzi Mkuu au kupigiwa kura mwaka 2010, lengo ni kujenga Chama kitakachokubalika kwanza na wanaotaka kujiunga nacho, Wanachama wake na Watanzania. Lengo la PPTL la muda mfupi si kupata Ubunge wa haraka haraka wa kiti kimoja kimoja, kugombea ruzuku au kugombea Urais ili kuking'oa CCM au kuwa chama maarufu cha Upinzani kwa jina.
Lengo letu litaoana sana na Waraka wa Mchungaji kwa Mtanzania. Nia si kupewa dhamana ya haraka kuongoza kisa tumeichoka CCM. La hasha, nia ni kuwaelimisha Watanzania kwa vitendo kuwa Chama chetu ni chama Mbadala ambacho kiko kwa ajili yao kwa kutumia vitendo na si kauli na hotuba kwenye majukwaa au kujivunia historia ya waasisi wa kuliongoza Taifa letu kuwa ndio kigezo cha PPPT kuaminika na kupewa dhamana ya kuongoza Tanzania.
PPPT kitakuwa chama chenye msukumo na mvuto wa kuchapa kazi na uzalishaji mali. Tutayatimiza haya kwa vitendo na si vijitabu au ilani zenye tenzi nyingi na maneno mengi.
Ndio maana tunakataa kujiunga na vyama vilivyopo ambavyo vimeshajenga usugu wa mawazo kuwa walicho nacho katika Katiba zao, Ilani na Sera zao ni mwanzo na mwisho na hakuna atakayeweza kubadilisha au kuleta mapinduzi mapya ya kuamsha Sera na Itikadi mpya au kuzifanyia marekebisho.
Mchungaji,
Nimekupata. Nasubiri kwa hamu kukiona. Wanasema siku zote shetani huwa amelala kwenye details. Ila kama kitakuwa kweli chama cha Watanzania bila ya Wajanja wachache kuwa WENYE CHAMA, basi andaa kabisa kadi yangu.
PPPT haikimbilii madaraka au kutaka kuongoza kwa mara moja au katika siku saba. PPPT kinataa kijijenge na si mijini bali ni vijijini, mikoani, mitaani na kujijenga kwa PPPT kutafanyika kwa kuishi na wananchi na kushirikiana nao katika kuwafundisha elimu ya Uraia, kuwafundisha mbinu bora za uzalishaji mali, kuwafafanulia umuhimu wa kuwa na uwezo wa kujitegemea na zaidi kuwa na Uhuru wa kujiamulia mambo, wa kuchagua na kudai uwajibikaji, bila hofu ya kudhulumiwa, kunyanyaswa au kutishiwa na dola au mbaya zaidi kunyimwa kwa makusudi nafasi ya kupiga hatua za maendeleo (mfano wa mkoa wa Kilimanjaro kutengwa na CCM kwa ajili ya kuchagua Upinzani na si CCM).