Yah tunatazamia kuanza ujenzi soon doc za permits ndio zimechelewa sana. Kwenye maonyesho ya cassava week iliyopita walionyesha mbegu mpya ambayo inaweza kutoa hadi tani 40 kwa hekta na inakubali kwa ukanda wote wa Pwani. Nafikiri tutaitumia sana kwa hii project naona itasaidia watu wengi sana
Wakuu tumefikia hatua muhimu na partners na tunaplan kufanya pilot project in 12-18 months tumeshaajiri director kwa ajili ya kuanza. Tutaanza na mtambo mdogo utakaohitaji kama tonnes 40 hivi za mihogo kwa siku. Mbia ni mtaalamu mwenye viwanda vya bio-plastics na anataka raw materials kwa hiyo soko ni la uhakika tutaexport USA so kuingiza dola. Baadaye tutaweka kiwanda cha bio-plastics pia ila tuanza na starch production kwanza. Tunafanya pilot kwa mwaka 1 kuona viability na tutaexpand kutegemea response ya wakulima katika kuzalisha mihogo na support generally
Tutakuwa tayari kufanya kazi na member watakaokuwa tayari kuzalisha mihogo either kupitia vyama vya ushirika au binafsi na tutasaidiana kwa kila hali ili kujenga win-win situation. Lengo kama nilivyosema awali ni kuinua kipato cha wakulima wadogo wadogo kwa kupanua masoko ya mazao yao (tukianza na mihogo inayolimika kila mahali Tanzania) na kuongeza ajira kwa vijana wakati tukiliingizia taifa pesa za kigeni na pia kuitikia wito wa kuprocess mazao ya wakulima ili kuongeza thamani kabla ya kuuza.
Natumaini tukiwa pamoja tutaweza na hii iwe changamoto kwa vijana tufikirie miradi itakayobadilisha maisha yetu na wengine badala ya kuboresha maisha katika level ya familia zetu tu na pia tuangalie upande mwingine kuliko tulivyozoea, kuajiriwa tu hasa baada ya elimu ya chuo kwani kuna fursa nyingi tuzitazame na kufikiria tuzitumieje huku tukiumiza vichwa kupata resources.
Tuendelee na majadiliano zaidi tusaidiane mawazo wakuu
Ninahusika kwa karibu na mradi wa C:AVA unaofadhiriwa na USAID na kutekelezwa kwa ushirikiano kati ya CPE-UDSM na Greenwich University. Lengo lake ni ku-diversify na kupromote cassava in Africa. Kwa hapa Tanzania tayari kazi inaenda vizuri na viongozi wa kisiasa kukubali kupeleka mswada wa kutaka kila confectionery iwe na angalau 20% ya unga wa muogo ili kupanua soko la ndani.
Kwa ufupi, naomba tuwasiliane Mkuu
I have been impressed by the idea of strenghten entrepreneurial tendency especially for graduates, as an intellectual i have also a project in the position to be funded. iko powa hiyo idea yako. Mimi ni entrepreneurial chemist nipo tayari kukusaidia so that we can move our country forward na kwa wale wengine wote wenye idea kama hizo please let contact with me via <a href="mailto:safariwafungo@yahoo.com">safariwafungo@yahoo.com
Habari yako kiongoz, i am also much impressed na hii proposed project yako. Nilishawahi kufkiria kitu cha hivyo ila nilipofkiriaga wap pa kupata fund, nilikata tamaa. Nilichokifanya ni kufkiria kuanzia kwenye kilimo cha mihogo huko kigoma. Kule Kigoma wananchi wanalima sana mihogo na wateja wakubwa ni Burundi/Rwanda/Congo kwa matumizi hayo uliyoyataja.Wadau wengine wenye msaada wa mawazo na mtazamo jamani kama wapo....................
I have been impressed by the idea of strenghten entrepreneurial tendency especially for graduates, as an intellectual i have also a project in the position to be funded. iko powa hiyo idea yako. Mimi ni entrepreneurial chemist nipo tayari kukusaidia so that we can move our country forward na kwa wale wengine wote wenye idea kama hizo please let contact with me via safariwafungo@yahoo.com
Habari yako kiongozi, kwenye maeneo yako nimeona umeainisha kuwa umepata shamba wilaya ya mvomero. Naomba nikupe hongera sana kwa kupiga hatua hiyo muhimu kwenye maendeleo. Kilimo hapo nyumban kinalipa sana kama utainvest kwenye zao lenye soko zuri. Mimi napenda kilimo, nina mashamba ila hayafikii ukubwa wa hilo lako. Kitu ambacho ningetaka kujua kabla cjakushauri, je hilo shamba lipo karibu na mto????nimependa sana mchango wako katika wazo hili, kumbe wana JF wengi ni wajasiliamali na wanaweza kutoa mwanga katika wazo linalowekwa mezani. mimi pia nko interested sana na kufanya project hiyo ya Kilimo cha Mhogo, kwa kuanzia nimepata ekali 100 katika Wilaya ya Mvomelo, ambapo zote zipo kwenye mchakato wa kupata hati. naomba msaada wa mawazo namna ya kufikia ndoto zangu. kama inawezekana naomba ni PM mkuu ili nipate pa kuanzia.
Mkuu Mzuzu,
natamani kujua ulikofikia na hii project!?