Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hili wazo hujapataga wadau tuu mpaka leo?? Hebu tupe feedback hii dili kubwa sana.
Mkuu mzuzu napenda kujua kama mmeanza kununua Mihogo na kama mnanunua ni kwa bei gain?
Dah! Safi sana, nasikitika nilikuwa mbali na idea yenu! Kila la kheri wakuu!
labda ungenipatia nmbr zako ...tunaweza kusaidiana kwenye hili
mradi unaendeleaje? fursa ya kuuza mihogo ipo au tayari mshapata suppliers wa kutosha?
Tunafanya construction ya pilot sasa. Nilipata wadau tukaunganisha nguvu lakini inaonekana haitoshi vilivyo. Natafuta wadau zaidi maana ni biashara kubwa kuliko tulivyotarajia. Tuna plan ya 12 tones capacity production per day lakini inaonekana kwa soko la ndani hatufiki hata 20% na la nje kwa orders tunazopata sasa inahitajika expansion ya mara 15 kutoka tunapoprospect. Thanks na karibu sana
Elinanho.TIB pia wanafund kwa riba ndogo xana sawa na bure we tuwasiliane tujue watakusaidia vp but wanataka business plan iliyoshiba.
Heshima mbele wana JF,
Nimekuwa nahangaikia kupata habari au msaada wa mawazo kutoka sehemu mbalimbali nafikiri na hapa jamvini lazima kuna msaada mkubwa wa mchango naweza kupata kwani naamini hapa ni kitovu cha taaluma na ujuzi wa mambo.
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikifikiria na kutafuta njia mablimbali za kuweza kufanya sisi kama vijana wa kitanzania katika mambo ya kiuchumi (nikimaanisha kuwa na biashara kubwa) tunazoweza kuanzisha vijana na kutufanya kuondokana na mawazo ya kuajiriwa hasa kwa vijana wenye elimu ya chuo kikuu. Lakini ninasikitika sana kuona watanzania wengi tunagombea nafasi za kuajiriwa tu na serikali yetu haina msaada wowote wa kuwezesha kuleta mafanikio. Serikali yetu inatafafsiri ujasiriamali ni kumwezesha mtu kupata rizki, mi naamini bila viwanda vidogo vya kati huo ujasiriamali hautakuwa na manufaa yoyote, wazalishaji wanatakiwa wajue soko na processing ikifanyika thamani ya mazao yao inaongezeka kwenye masoko ya kimataifa.
Kwa mtazamo wangu nimekuwa nikiamini watu wenye elimu ya chuo kikuu wanatakiwa kuwa na mtazamo wa kuanzisha ajira kwani wao wamepevuka upeo tofauti na waliokosa elimu hiyo.
Kwa wanaJF wanaojua jinsi ya kupata resources jamani ninaomba msaada wa mawazo.
Nimefanya feasibility study kwa miaka kadhaa sasa na hatimaye nimeaandaa business plan ya kufanya processing ya cassava (mihogo) kutengeneza starch. Mali ghafi hakuna asiyejua inapatikana nchi kwetu popote pale unahitaji kuwahakikishia wakulima soko tu na watakufanyia mambo ya kutosha. Hii itainua uchumi wa wakulima wadogo sana na hasa kwenye maeneo ambayo kilimo cha pamba kimeanguka na mikoa kame kama ya kati isiyo na zao la biashara kwani popote inastawi
Soko lipo juu sana na lengo ku export tayari kuna watu wanahitaji sana kuimport kutoka Tanzania nimejaribu kutangaza na kupata response nzuri sana. Kuna soko kubwa sana nchini (yote inaagizwa toka nje esp SA) kuna soko kubwa sana pale TBL na viwanda vingine vinavyotengeneza madawa, nguo, bia, tambi, biscuits, noodles, almost viwanda vyote vinavyotengeneza vyakula (canned na bottled) vinahitaji starch.
Tatizo kubwa nililonalo ni kwamba natafuta source ya funds kuanzisha kamradi haka ambacho profit margin yake ipo juu sana. Nipo tayari kwa mazungumzo specific ya jinsi ya kufanya ili mradi niweze kutimiza hii ndoto. Mradi huu unaweza kuwa expanded katika muda wa miaka 2 au 3 ukawa na plant nyingine ya kuzalisha ethanol kwa kutumia waste materials baada ya kuprocess cassava na tayari nimeanza kudraft plan yake. Nimejaribu kupita Tanzania investment bank na kuongea nao wakawa na interest ya kusaidia ila nikawa sina colateral wala mdhamini mwenye assets nzuri (mimi mtoto wa mkulima tu hata elimu yangu ni ya kuungaunga tu) ninaweza kuraise kidogo tu. Nimepita na NBC ikawa vilevile tu na mradi unakubalika na tatizo siaminiki tu kwa vile sina historia ya kushika pesa kubwa.
Ninaweza kusimamia hii kazi na ikawa juu kiasi cha kuridhisha na kushindana na biashara kubwa tu hata kuanzisha zingine safi zaidi.
Haya wadau naomba reference kwenye source au tujiunege na kuona nini cha kufanya. Nipo kwa wazi nasikiliza mawazo yenu na ushauri! unaweza kuchangia au kuniPM vyovyote utakavyoona
Ahsanteni sana
Tunafanya construction ya pilot sasa. Nilipata wadau tukaunganisha nguvu lakini inaonekana haitoshi vilivyo. Natafuta wadau zaidi maana ni biashara kubwa kuliko tulivyotarajia. Tuna plan ya 12 tones capacity production per day lakini inaonekana kwa soko la ndani hatufiki hata 20% na la nje kwa orders tunazopata sasa inahitajika expansion ya mara 15 kutoka tunapoprospect. Thanks na karibu sana
nimependa sana project yako mkuu Mzuzu.naomba unitumie bussiness plan yako tushirikiane kurun hiyo project ninamfahamu jamaa mmoja anaweza kutusaidia kwa kupata mahitaji ya plant nzima.
nitumie hiyo kwa brjf_badilika@yahoo.com.
Mkuu Mzuzu,Nakukubali sana, nakutakia kila la heri ktk project yenu. Usisite ku-share na sisi changamoto utakazo kutana nazo.