Project funding sources


Brief imekuja kwa email umeipata?
 
Last edited by a moderator:
Dah bigup sana mkuu .watu walio wengi sana wana fikiria kuajiliwa bila kujiajili
 
Mkuu Mzuzu,

hebu tuma tena maana sijaipata email yako au imekuja kama spam. Nipo katika kupanga timu ingawa huenda tukaja kivingine.
Kwenye mkutano wa Diasporamwezi wa nane mwqka huu hapo Dar, nilikutana na Mzee mmoja Mtanzania anayeishi Nigeria na kawa huko kwa miaka 33. Mzee huyu inasemekana ndiyo kamleta Dangote hapo Tanzania. Alisema kuwa na yeye/wao wako kwenye mchakato wa kuzalisha hiyo starch. Sijui kama mnashirikiana naye au yeye yuko kivyake.

Hongera sana kwa bidii zenu.

Brief imekuja kwa email umeipata?
 
Moja ya Project Funding Sources ni kutumia Dar Es Salaam Stock Exchange (DSE). Kuna dirisha maalum limeanzishwa DSE kwa ajili ya kusaidia wajasiria mali, linaitwa Enterprise Growth Markets (EGM) au nchi nyingine dirisha hili linaitwa Alternative Investment Market (AIM). Dirisha hili lina masharti nafuu, haliangalii track record ya mradi, linaangalia zaidi uzuri wa project (future prospects), hamna collateral (security) kwa sababu unapata equity funding.
Unaweza kubadilishana mawazo nasi kama utataka. Kampuni yetu imeisaidia SWALA OIL & GAS (T) PLC kuingia sokoni. Kampuni hii ya SWALA tuliingiza sokoni DSE mwezi wa June/July 2014 kwa kuuza hisa zake kwa Tshs 500 per share. Huu ni mwezi Oktoba 2014, hisa za SWALA zinauzwa kwa Tshs 2110 kila hisa kwa bei ya jana.
Email yangu: nsemwa@archfia.or.tz. KARIBUNI WOTE TUBADILISHANE MAWAZO
 
Ilikuwa mawazo, utafiti, utendaji, sasa kiwanda na mashamba yanaonekana Bungu Rufiji. Mzuzu hongera sana.








Ufunguzi utafanyika lini mkuu tuje kujifunza na kununua bidhaa zako.

Thanks sana kiongozi. Tutakuwa operational mwezi November mwishoni na uzinduzi rasmi utakuwa mwishoni November hiyo hiyo
 
Mzuzu tani moja ya mhogo mnanunua kwa bei gani? na ni aina gani ya mhogo mnayopendekeza wakulima walime.

Kuanzia mwaka kesho kutakuwepo na uhaba mkubwa wa mihogo katika jiji la DSM, wakulima hii ndiyo fursa ya kuongeza ukubwa wa mashamba ya mihogo, kwani sasa soko la uhakika lipo.
 
Last edited by a moderator:
am very impresed with ur project lets join our hands and make something better
 

Tutaanza na Tsh 100 kwa kilo na itaflactuate kuendana na bei ya starch sokoni
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ebu tuchekiane kwenye emeail yangu (pamos@amend.org) tufanye kitu

 

mkuu nicheki kwa 0719168700,tufanye yetu
 
Hivyo vikali pia ni vizuri kwa ajiri ya kuextract compound itayoitwa Cs inTumika sana huko china kwa ajiri ya kutengenezea mabomu ya machozi yaani tear gas .Also pili pili kama pesa ipo hata Tanzania inawezekana
 
mkuu nicheki kwa 0719168700,tufanye yetu

mkuu kama umefanikiwa katika hili naomba unipe muongozo coz hata mimi nina project ya mambo ya ujenzi na ni very marketable and profitable.
 
Mkuu Mzuzu , Malila et al nawashukuruni sana kwa mawazo yenu ya kujenga. Hakika machozi yana nilenga lenga kwa kuona namna vijana wa kitanzania mlivyotumia sehemu ya akili na ujuzi wenu kuokoa kizazi hiki.
Natumai siku moja mtakuja toa ushuhuda wenu hapa jukwaani namna umoja wa dhati ulivyo wasaidia kufikia nia yenu.
Natamani nimtumie kopi ya wzo lako waziri mkuu , waziri wa kilimo, waziri wa viwanda na uwekezaji ili aone kuwa Tanzania imejaaliwa vijana wenye akili timamu, maono, nia, na maalifa ya kujenga nchi.
Hongereni sana kwa mawazo ya kujenga.
 

Asante Mkuu,

Naomba nimrudishie Mungu shukrani hizi kwa kuwa tumefanya hicho kidogo kwa uweza wake, naam namwomba Mungu atupe nguvu na uhai na afya ili tufikie malengo na hatimaye tuwe tumechangia maendeleo ya nchi yetu kwa kiasi fulani.

Be blessed mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…