Mkuu naona siasa zimekolea sana sasa hapa! Sisi wajasiriamali pia tunaendelea na mikakati.
Update, wakuu tumemaliza mikataba na docs zote muhimu sasa tunaingia kwenye implementation. Mradi mzima utakuta $4M kwa investment ya miaka mitatu, sept hii tunaanza na kuagiza mitambo ya kuanzia tunaanza na pilot project kwa miezi 6 then tutafanya major expansion baada ya kudemonstrate viability.
Nashukuru sana wanaJF hiki kweli nikisima cha hekima, ilikuwa kama utani wakati naanza kuja kuomba ushauri hapa na leo hii ni hatua kubwa tumefikia
Sasa nimeamini kuwa waTZ hatujiandai kufanya plan tunazotaka na kama tunaandaa maandiko yanakuwa too theoritical. Hii proposal ilipata partners kwa kuisoma tu na kujustify uwezekano pia kwa kuwa feasiblity study nilifanya kwa muda mrefu na kujiandaa kutoa maelezo kwa maswali yote yatakayoibuka. Investor kasoma tu kapeleka University of California kwa Professor mmoja consultant akaikubali kila kitu kikaisha. Ukiandaa docs vizuri na kwa data sahihi bila usanii utapata funds bila hata hiyo colatera wanayopigia kelele kila siku, mi sina kitu maskini tu mtz wa kawaida huyu tajiri wala sikumjua na sikuunganishwa na mtu. Kapatikana online na hadi sasa tumeshachoma $20,000 kwa ground work
Tutakuwa na Cereplast inc ubia unaweza kuiona kwa
www.cereplast.com ambayo tutazalisha pamoja na itanunua products zote kufeed viwanda vyake US na France. Baadaye tutaweka viwanda hapahapa vya plastics, biofuels, spirits etc lengo ni kusaidia wakulima wasiuze mazao ghafi wananyonywa mno na hawana tumaini lolote
Tena nashukuru sana hili jamvi mchango wa watu si haba. Namshukuru kwa dhati Malila, Tiger, Sikonge, Lazydog, Ntemi, newmzalendo na wengine wote, japo tulianza kwa challenge na kufikiri haitawezekana, kwani kuna wengine walisema ni mradi wa kufikirika. Hii haitusogezi mbele kwani tunakatishana tamaa mapema kikubwa ni kuthubutu, bora ukakwame ulipojaribu na sio mtu akwambie nenda SIDO wakati SIDO yenyewe ilikufa, kweli kuna mtu anayetaka kujifunza kwa aliyefeli??? Mawazo haya hata SIDO wenyewe hawana, nimepita EPZ wakabaki wanashangaa wanauliza umesomea wapi?? Sielewi majengo ya shule yana mchango gani hapo?? Nikasema hapahapa sijawahi kwenda nje zaidi kuja kusign mikataba na hawa jamaa! Elimu inatafutwa na mtu kwa plan ya mtu anavytaka mwenyewe na sio majengo. Wapo wengi waliosomea shule zenye majina makubwa na wanafanya nini au wana impact gani kwa jamii zao?? Nikisema elimu yangu wengine watashangaa lakini haina contribution on this plan tena haina uhusiano hata kidogo
Pamoja tutafika tukiwa na uchungu na nchi yetu. Tunataka tulete $$$$$$ sio kutoa tu kila siku na kuingiza kwa mikopo, kama nilivyoplan tunaanza na mihogo then mazao mengine, walengwa wakubwa ni wakulima maskini na tuboreshe income ya vijijini vijana watarudi kuzalisha tu na sio kuuza vitambaa vya makamasi pale magomeni barabarani
More to come, lets learn and put in practice