Project funding sources

Project funding sources

jamani mimi nina contact ya kusambaza magunia ya jute, yaani yale ya katani mimi ni agent wa hayo magunia ujazo wowote tufauti na yale ya kamba za plastic haya yana dumu ni re usable na kwa wale watakaofanya export wanarudishiwa hela zao kwa hiyo guarantee scheme japo zinachelewa, lakini kodi yake ni ndogo kama yakionyesha kuwa ni kwa ajili ya export, bei zetu ni affordable please ni pm kama una interest, nyie wa vitunguu mihogo wote nyie ni wateja wangu p
 
mkuu hata mi nahitaji sample sijui unaweza nisaidia
Mkuu Barabita, nimeona uzi wako huu wa November, 2012. Binafsi nina interest ya namna ya kuandika BP, hivyo nami naomba sample kama bado umo humu JF. Kama ikikupendeza kufanya hivyo, basi ni PM au niletee moja kwa moja via emaili hii: trsde2002@yahoo.com
 
Tayari mkuu tunaanza mambo next week baada ya muda mrefu wa kufuatilia documentations..

Karibu sana
Mkuu Mzuzu hamjapanga bei ya manunuzi say kwa tani moja katika USD kama ulivyosema huko nyuma? Bei itatuhamasisha sisi wakulima. Tupo hapo Jaribu Mpakani.
 
Mkuu Mzuzu hamjapanga bei ya manunuzi say kwa tani moja katika USD kama ulivyosema huko nyuma? Bei itatuhamasisha sisi wakulima. Tupo hapo Jaribu Mpakani.

Tutaanza na USD 50 kwa tani then tutaendelea kuadjust accordingly. Tutanunua aina zote za muhogo hatuchagui na tutapima uzito kila unapoletwa
 
Tutaanza na USD 50 kwa tani then tutaendelea kuadjust accordingly. Tutanunua aina zote za muhogo hatuchagui na tutapima uzito kila unapoletwa

Sasa tunaotegemea mhogo kama kitafunio mjini Dsm inabidi kufikiri mara mbili sasa,yawezekana mhogo wa Bungu/Jaribu usiingie Dar tena kama siku za karibuni.

Big up Mzuzu.
 
Sasa tunaotegemea mhogo kama kitafunio mjini Dsm inabidi kufikiri mara mbili sasa,yawezekana mhogo wa Bungu/Jaribu usiingie Dar tena kama siku za karibuni.

Big up Mzuzu.

Malila kuna eka 5000 tunataka zote ziwe shamba kaka njooni tuwape mlime tutapiga kwa mashine kulima, kupanda, kumwaga dawa za magugu na kuvuna hlf costs tutakatana kwenye mauziano ya muhogo. Tukiweza hili tutapata muhogo wa kutosha kula na kuprocess
 
Tumetangaza tena watu watume tena expression of interest kwenye gazeti la Mwananchi la leo tunaomba wote walituma warudie tu tunaongeza wigo wa wakulima. Tunaanza upya ili kuweka uwanja mpana zaidi kwa wasiofika kwenye mtandao

Okay sawa mkuu tutatuma tena jana nilijaribu kupita ofisini kwenu pale EPZ nikapata abcs inatia moyo
 
Mzuzu, bei ya USD 50per tonne ni makopa ama mhogo ambao ni fresh haujakaushwa?
 
Last edited by a moderator:
Hii ni kwa ajili ya fresh/raw cassava toka shambani tu na unatakiwa usizidi siku 2 tangu kuvunwa
 
Bravoo mzuzu. Nimesikia graduators wengi wameplan na wako supported na serikali kupitia tanzania investimate jaribu kuwaona
 
Heshima mbele wana JF,

Nimekuwa nahangaikia kupata habari au msaada wa mawazo kutoka sehemu mbalimbali nafikiri na hapa jamvini lazima kuna msaada mkubwa wa mchango naweza kupata kwani naamini hapa ni kitovu cha taaluma na ujuzi wa mambo.

Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikifikiria na kutafuta njia mablimbali za kuweza kufanya sisi kama vijana wa kitanzania katika mambo ya kiuchumi (nikimaanisha kuwa na biashara kubwa) tunazoweza kuanzisha vijana na kutufanya kuondokana na mawazo ya kuajiriwa hasa kwa vijana wenye elimu ya chuo kikuu. Lakini ninasikitika sana kuona watanzania wengi tunagombea nafasi za kuajiriwa tu na serikali yetu haina msaada wowote wa kuwezesha kuleta mafanikio. Serikali yetu inatafafsiri ujasiriamali ni kumwezesha mtu kupata rizki, mi naamini bila viwanda vidogo vya kati huo ujasiriamali hautakuwa na manufaa yoyote, wazalishaji wanatakiwa wajue soko na processing ikifanyika thamani ya mazao yao inaongezeka kwenye masoko ya kimataifa.

Kwa mtazamo wangu nimekuwa nikiamini watu wenye elimu ya chuo kikuu wanatakiwa kuwa na mtazamo wa kuanzisha ajira kwani wao wamepevuka upeo tofauti na waliokosa elimu hiyo.

Kwa wanaJF wanaojua jinsi ya kupata resources jamani ninaomba msaada wa mawazo.

Nimefanya feasibility study kwa miaka kadhaa sasa na hatimaye nimeaandaa business plan ya kufanya processing ya cassava (mihogo) kutengeneza starch. Mali ghafi hakuna asiyejua inapatikana nchi kwetu popote pale unahitaji kuwahakikishia wakulima soko tu na watakufanyia mambo ya kutosha. Hii itainua uchumi wa wakulima wadogo sana na hasa kwenye maeneo ambayo kilimo cha pamba kimeanguka na mikoa kame kama ya kati isiyo na zao la biashara kwani popote inastawi

Soko lipo juu sana na lengo ku export tayari kuna watu wanahitaji sana kuimport kutoka Tanzania nimejaribu kutangaza na kupata response nzuri sana. Kuna soko kubwa sana nchini (yote inaagizwa toka nje esp SA) kuna soko kubwa sana pale TBL na viwanda vingine vinavyotengeneza madawa, nguo, bia, tambi, biscuits, noodles, almost viwanda vyote vinavyotengeneza vyakula (canned na bottled) vinahitaji starch.

Tatizo kubwa nililonalo ni kwamba natafuta source ya funds kuanzisha kamradi haka ambacho profit margin yake ipo juu sana. Nipo tayari kwa mazungumzo specific ya jinsi ya kufanya ili mradi niweze kutimiza hii ndoto. Mradi huu unaweza kuwa expanded katika muda wa miaka 2 au 3 ukawa na plant nyingine ya kuzalisha ethanol kwa kutumia waste materials baada ya kuprocess cassava na tayari nimeanza kudraft plan yake. Nimejaribu kupita Tanzania investment bank na kuongea nao wakawa na interest ya kusaidia ila nikawa sina colateral wala mdhamini mwenye assets nzuri (mimi mtoto wa mkulima tu hata elimu yangu ni ya kuungaunga tu) ninaweza kuraise kidogo tu. Nimepita na NBC ikawa vilevile tu na mradi unakubalika na tatizo siaminiki tu kwa vile sina historia ya kushika pesa kubwa.

Ninaweza kusimamia hii kazi na ikawa juu kiasi cha kuridhisha na kushindana na biashara kubwa tu hata kuanzisha zingine safi zaidi.

Haya wadau naomba reference kwenye source au tujiunege na kuona nini cha kufanya. Nipo kwa wazi nasikiliza mawazo yenu na ushauri! unaweza kuchangia au kuniPM vyovyote utakavyoona

Ahsanteni sana

safi sana mkuu kwa mchango wako binafsi nimependezwa na article yako mbali ya kuwa mdau wa kilimo.

nimeku pm.
 
Hebu waone IITA wako Mikocheni barabara ya cocacola opposite Konoike wanashgughulika na mazao na hasahasa mihogo, vilevile wanatoa fund kwa vikundi mbalimbali......nadhani waone, ingia kwenye website yao PAN IIT utapata details zao.
 
Kazi imeshaanza tayari nashukuru sana wadau wote waliochangia ss kilichobaki ni kutafsiri hii ndoto kwenye vitendo. Planning na utafutaji wa resources umechukua muda mrefu sana lakini ndio kujifunza lakini mradi huu ni zao la JF na pia ni mfano wa jinsi tunavyoweza kulitumia jukwaa kwa manufaa yetu.
 
Mzuzu tunashukuru kwa habari nzuri sana. Tunatakutakia kila la heri lakini pia tunaomba itakapofika stage ambayo unafeel comfortable kutukaribisha tukutembelee usisite kufanya hivyo kwa wale watakaoweza kwa ajili ya kujifunza na kupata inspiration. Ahsante!
 
Definitely sir, nitawaalika JF members kuja kutembelea na kuona translation ya mawazo na michango yao yote. Nataka iwe kama somo la kujifunza na kufanya inspiration kwa wote kwamba handwork, endurance na tolerance mwisho wa siku vinaleta matunda unayoyatafuta kwa nguvu zote na sacrifice.
 
Back
Top Bottom