Project kubwa ya kilimo RUVU!

Project kubwa ya kilimo RUVU!

Kuweka Irrigation system ekari 20 inarange kwenye 60M.. so as your planning try to do a thorough research kwenye estimations zako. Kwa haraka sana naona it is good to start small and grow big....!!

Mkuu Ndenga,
Naomba kuelimishwa zaidi hapo, hizo gharama za irrigation system ni za system ya mabomba na sprinklers, au ni system ya mifereji ya kutiririsha maji shambani ?
Naomba elimu zaidi hapo,
Asante.
 
Kuweka Irrigation system ekari 20 inarange kwenye 60M.. so as your planning try to do a thorough research kwenye estimations zako. Kwa haraka sana naona it is good to start small and grow big....!!

I hope you are talking of drip irrigation
 
Ruvu matikiti yanakubali sana. Kule kwenye kijiji ambacho sisi tuna mashamba, kuna jamaa wanalima matikiti na wanapata sana.
Ardhi ya kule in ya udongo mweusi wenye rutuba sana.
Changamoto ni maji tu, ndio maana jamaa wale kule Ruvu wanapendelea kukodi mashamba yaliyo karibu na mto Ruvu.
Ukiwa tayari, unaweza kunishtua nikakuunganisha na wanavijiji wenye mashamba yaliyo karibu na mto.

Thanks mkuu ntakucheki!
 
Kuweka Irrigation system ekari 20 inarange kwenye 60M.. so as your planning try to do a thorough research kwenye estimations zako. Kwa haraka sana naona it is good to start small and grow big....!!
Ahsante kwa ushauri kaka.
 
Ruvu matikiti yanakubali sana. Kule kwenye kijiji ambacho sisi tuna mashamba, kuna jamaa wanalima matikiti na wanapata sana.
Ardhi ya kule in ya udongo mweusi wenye rutuba sana.
Changamoto ni maji tu, ndio maana jamaa wale kule Ruvu wanapendelea kukodi mashamba yaliyo karibu na mto Ruvu.
Ukiwa tayari, unaweza kunishtua nikakuunganisha na wanavijiji wenye mashamba yaliyo karibu na mto.

Na vipi usafiri wa kupeleka mazao sokoni?
 
Kama 2km na unalipa 40,000 kwa eka kwa mwaka...manpower ya pale sio nzuri sana vizuri ulete yako.......nilichukua eka 6 mwaka jana zikiwa 900,000 na nimelima vitunguu na matikiti hela yote imerudi

mkuu faida ilikuwaje na soko zuri ni wapi?...
 
Na vipi usafiri wa kupeleka mazao sokoni?

Usafiri toka shambani mpaka sokoni (Dar es Salaam) ni rahisi sana.
Mashamba hayo ninayozungumzia yako kijiji kinaitwa Kitomondo, kipo kata ya Ruvu, kutoka Mlandizi unafuata barabara inayoenda Mzenga. Kijiji kipo kilometa 30 toka Mlandizi, (kilometa 100 toka Dar es Salaam). Barabara ni nzuri kwa ujumla, isipokuwa wakati wa masika ndio kunakuwa na changamoto chache za usafiri.
 
Thanks mkuu.
But naomba niendelee kukusumbua.
Na vp nyumba za kupanga kwa ajiri ya man power?

Na vp samadi jee inapatikana ya kutosha?
 
Huko kijijini hamna nyumba za kupanga kwa ajili ya wafanyakazi.
Tunachofanya sisi ni kuwajengea wafanyakazi vibanda vya kukaa. Mfano mimi nina vibanda viwili vya kukaa wafanyakazi wanaonilindia shamba langu. Wafanyakazi wangu hao nimewapa baiskeli ya kuwarahisishia usafiri wa hapa na pale.
Ni gharama ndogo zaidi kuwajengea vibanda vya kukaa.
Ila unaweza kuwaajiri wanakijiji wenyewe wawe wafanyakazi ili kupunguza gharama.

Kuhusu mbolea, mimi naona haitahitajika, maana udongo wa kule una rutuba saana.
Jamaa wote wanaolima matikiti na mpunga hawajawahi kutumia mbolea na wanavuna sana.
 
Hela yote imerudi, faida je?
Watu mnakomaaa vibaya kuuliza faida; faida mbona iko wazi, hata kama amerudisha millioni 6 zake na gharama za kulima bila ziada bado ana faida kuubwa mno ya ardhi!
 
Huko kijijini hamna nyumba za kupanga kwa ajili ya wafanyakazi.
Tunachofanya sisi ni kuwajengea wafanyakazi vibanda vya kukaa. Mfano mimi nina vibanda viwili vya kukaa wafanyakazi wanaonilindia shamba langu. Wafanyakazi wangu hao nimewapa baiskeli ya kuwarahisishia usafiri wa hapa na pale.
Ni gharama ndogo zaidi kuwajengea vibanda vya kukaa.
Ila unaweza kuwaajiri wanakijiji wenyewe wawe wafanyakazi ili kupunguza gharama.

Kuhusu mbolea, mimi naona haitahitajika, maana udongo wa kule una rutuba saana.
Jamaa wote wanaolima matikiti na mpunga hawajawahi kutumia mbolea na wanavuna sana.
Thanks mkuu kwa msaada wako.
Na vipi soko lake kama nikitaka kuuzia shambani?
Na bei imekaaje kutegemea na msimu?
Na kwasababu wewe una idea kidogo jee kwa zao la tikiti ni muda gani navuna?
 
Mimi sijawahi kulima tikiti, ila kuna jamaa wanalima sana.
Mimi sijalima kwa sababu msimu wa ulimaji tikiti huwa ni baada ya mavuno ya mpunga mwezi July hadi August.
Wakulima wanafanya hivyo kwa sababu tikiti linahitaji maji mengi, na jua kali ili kustawi vizuri.
Watu wengi huku wanalima karibu na mto ruvu ili kuwa na uhakika wa maji.

Kuhusu bei sijafahamu wanauzaje yakiwa shambani, ila wengi wao wanapeleka Dar wenyewe.

Ila naweka hapa article ya ukulima wa tikiti, labda inaweza kuwa mwongozo mzuri wa kuanzia.

Pamoja sana Mkuu.
 
Attachments

Ahsante kaka kwa msaada wako!
 
Ahsante kaka kwa msaada wako!

Msaada mwingine huu hapa,

Nina shamba eka kumi, lina nyumba tatu za wafanyakazi, linafaa kwa matikiti maji. Lina maji ya kutosha sana mwaka mzima. Wanaolima karibu hapo wanatumia mbolea ya kuku na ng`ombe. Bei kwa eka ni Tsh 60,000/ kwa msimu mmoja. Manpower iliyopo si ya kuaminika sana. Shamba lina rutuba nzuri.

Ni km 45 hivi ukianzia Tazara, lipo Marogoro Mkuranga. Pia Kitunguu kinamea ktk ardhi ile. Changamoto za pale ni nguruwe/nguchilo/nyani.
 
Ningekuwa sijahama Dar lingenifaa sana hilo shamba bei yake sio mbaya kama maji yapo nalitamani sana sema nipo mbali management itanishinda kwa walio huko ukiwa na ekari kumi zenye maji ya uhakika huwezi juta kama una usimamizi mzuri
 
Msaada mwingine huu hapa,

Nina shamba eka kumi, lina nyumba tatu za wafanyakazi, linafaa kwa matikiti maji. Lina maji ya kutosha sana mwaka mzima. Wanaolima karibu hapo wanatumia mbolea ya kuku na ng`ombe. Bei kwa eka ni Tsh 60,000/ kwa msimu mmoja. Manpower iliyopo si ya kuaminika sana. Shamba lina rutuba nzuri.

Ni km 45 hivi ukianzia Tazara, lipo Marogoro Mkuranga. Pia Kitunguu kinamea ktk ardhi ile. Changamoto za pale ni nguruwe/nguchilo/nyani.
Ahsante kaka.
Sasa hao nguruwe/nguchilo na nyani ntawadhibiti vipi?si watanimalizia matikiti yote mkuu?

Kwa kifupi nimepapenda lakini nijulishe juu ya ulinzi,na pia Miundombinu ya barabara.
 
Msaada mwingine huu hapa,

Nina shamba eka kumi, lina nyumba tatu za wafanyakazi, linafaa kwa matikiti maji. Lina maji ya kutosha sana mwaka mzima. Wanaolima karibu hapo wanatumia mbolea ya kuku na ng`ombe. Bei kwa eka ni Tsh 60,000/ kwa msimu mmoja. Manpower iliyopo si ya kuaminika sana. Shamba lina rutuba nzuri.

Ni km 45 hivi ukianzia Tazara, lipo Marogoro Mkuranga. Pia Kitunguu kinamea ktk ardhi ile. Changamoto za pale ni nguruwe/nguchilo/nyani.
Mkuu malila naomba kujua kama season ya kuanzia mwezi feb-march inafaa kwa matikiti?
 
Ruvu matikiti yanakubali sana. Kule kwenye kijiji ambacho sisi tuna mashamba, kuna jamaa wanalima matikiti na wanapata sana.
Ardhi ya kule in ya udongo mweusi wenye rutuba sana.
Changamoto ni maji tu, ndio maana jamaa wale kule Ruvu wanapendelea kukodi mashamba yaliyo karibu na mto Ruvu.
Ukiwa tayari, unaweza kunishtua nikakuunganisha na wanavijiji wenye mashamba yaliyo karibu na mto.
Habari ya siku mkuu!
Vp mchakato wako wa kilimo unaendeleaje?
 
Kama 2km na unalipa 40,000 kwa eka kwa mwaka...manpower ya pale sio nzuri sana vizuri ulete yako.......nilichukua eka 6 mwaka jana zikiwa 900,000 na nimelima vitunguu na matikiti hela yote imerudi

Tunaomba more info kama una contacts za wahusika plz PM ili tuwatafute watupe mwelekeo.
 
Back
Top Bottom